Shamkware
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 1,740
- 2,244
Wapendwa habari ya majukumu.
Naomba mwenye kujua aniambie, Nihitaji kujua hospitali inayo pima au kushugulika na matatizo ya COVID -19 nikapime mwenyewe kwa hiari yangu.
Nahitaji kupima maana, Wiki iliyopita Tar.10 nilikuwa kwenye msiba wa kaka yangu aliyefariki kwa matatizo haya ya upumuaji. Sasa mimi ni mmoja kati ya watu walioshiriki msiba kwa hatua zote na lazima nikiri kwamba hakukuwa na tahadhari za kutosha na mimi sikujali kabisa kulingana na maumivu niliyokuwa nayo ya kumpoteza kaka yangu.
Sasa leo ni siku ya nne mimi nasikia maumivu ya kifua yaani kama nina kitu kizito hivi nyuma ya mgongo pamoja na maumivu ya mwili kama dalili ya Malaria hivi, Cha ajabu wife nae anadai maumivu ya kifua tena yeye na kikohozi kigumu sana anakohoa sana tumepiga tangawizi, Malimao na kujifukiza pamoja na mazoezi saana lakini inapoa kidogo ina rudi hali vile vile.
Kilicho niogopesha zaidi leo dada wa kazi ameamka anadai mafua makali na muwasho kwenye koo nimeogopa sana, Mkumbuke juzi nilienda hospital mimi na wife tukapewa dawa za kifua ikiwemo Amoxicillin pamoja na dawa fulani za maji lakini wapi.
Sasa mimi nataka nikapime tu ili niokoe ndugu zangu maana wanakuja tu hapa home wala hawaelewi ukiwaambia wakae mbali. Mama yangu nae anakuja sana na umri yeye umeenda isitoshe nae tangu jana anadai anatapika mara kwa mara na mwili kuchoka sana Nachanganyikiwa kabisa mdugu zangu.