Ushauri: Hospitali gani Jijini Dar wanapima Covid-19?

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,739
2,242
Wapendwa habari ya majukumu.

Naomba mwenye kujua aniambie, Nihitaji kujua hospitali inayo pima au kushugulika na matatizo ya COVID -19 nikapime mwenyewe kwa hiari yangu.

Nahitaji kupima maana, Wiki iliyopita Tar.10 nilikuwa kwenye msiba wa kaka yangu aliyefariki kwa matatizo haya ya upumuaji. Sasa mimi ni mmoja kati ya watu walioshiriki msiba kwa hatua zote na lazima nikiri kwamba hakukuwa na tahadhari za kutosha na mimi sikujali kabisa kulingana na maumivu niliyokuwa nayo ya kumpoteza kaka yangu.

Sasa leo ni siku ya nne mimi nasikia maumivu ya kifua yaani kama nina kitu kizito hivi nyuma ya mgongo pamoja na maumivu ya mwili kama dalili ya Malaria hivi, Cha ajabu wife nae anadai maumivu ya kifua tena yeye na kikohozi kigumu sana anakohoa sana tumepiga tangawizi, Malimao na kujifukiza pamoja na mazoezi saana lakini inapoa kidogo ina rudi hali vile vile.

Kilicho niogopesha zaidi leo dada wa kazi ameamka anadai mafua makali na muwasho kwenye koo nimeogopa sana, Mkumbuke juzi nilienda hospital mimi na wife tukapewa dawa za kifua ikiwemo Amoxicillin pamoja na dawa fulani za maji lakini wapi.

Sasa mimi nataka nikapime tu ili niokoe ndugu zangu maana wanakuja tu hapa home wala hawaelewi ukiwaambia wakae mbali. Mama yangu nae anakuja sana na umri yeye umeenda isitoshe nae tangu jana anadai anatapika mara kwa mara na mwili kuchoka sana Nachanganyikiwa kabisa mdugu zangu.
 
Kwa sasa kupima sio muhimu mkuu. Kwa mazingira haya uliyosema nawashauri anzeni matibabu tu. Pamoja na malimao sijui maembe mnayokula muende hospitali kabisa mkapatiwe tiba!
 
Nilienda nikamweleza Dr. hali halisi lakini nikapewa dawa za kifua tu yaani kiufupi hizi hospital za kawaida changamoto ndio maana nataka niende hosptal inayo shughulikia ikiwemo kupima
 
Yabidi ufanyiwe X-ray ya kifua

kuna dawa moja inauzwa 150,ooo (chupa ndogo kama ya dawa ya kikohozi)
 
Sasa unataka ukapime ili iweje kwenye tatizo ambalo halina dawa?

Dalili na mazingira vyote vinakueleza tatizo lako.

Sasa bado unaangaika na kujua tatizo?

Ushauri wangu hapo ni kuchukua hatua tu.,
Pambana kupiga nyungu ya kutosha maana katika hatua hiyo hata chanjo haina umuhimu tena kwako..

Na pia mkuu ONDOA hofu juu kufa,.
Kama haujanielewa vile:
Nakwambia hivi ONDOA hofu juu ya kufa.
Kifo kipo tu na hakikimbiwi.
 
Ukifanya X-ray ikionyesha una nimonia

Nunua hizi dawa tajwa hapa, Utanishukuru
IMG_20210218_122137_080.jpg
 
Wapendwa habari ya majukumu.

Naomba mwenye kujua aniambie, Nihitaji kujua hospitali inayo pima au kushugulika na matatizo ya COVID -19 nikapime mwenyewe kwa hiari yangu.

Nahitaji kupima maana, Wiki iliyopita Tar.10 nilikuwa kwenye msiba wa kaka yangu aliyefariki kwa matatizo haya ya upumuaji. Sasa mimi ni mmoja kati ya watu walioshiriki msiba kwa hatua zote na lazima nikiri kwamba hakukuwa na tahadhari za kutosha na mimi sikujali kabisa kulingana na maumivu niliyokuwa nayo ya kumpoteza kaka yangu.

Sasa leo ni siku ya nne mimi nasikia maumivu ya kifua yaani kama nina kitu kizito hivi nyuma ya mgongo pamoja na maumivu ya mwili kama dalili ya Malaria hivi, Cha ajabu wife nae anadai maumivu ya kifua tena yeye na kikohozi kigumu sana anakohoa sana tumepiga tangawizi, Malimao na kujifukiza pamoja na mazoezi saana lakini inapoa kidogo ina rudi hali vile vile.

Kilicho niogopesha zaidi leo dada wa kazi ameamka anadai mafua makali na muwasho kwenye koo nimeogopa sana, Mkumbuke juzi nilienda hospital mimi na wife tukapewa dawa za kifua ikiwemo Amoxicillin pamoja na dawa fulani za maji lakini wapi.

Sasa mimi nataka nikapime tu ili niokoe ndugu zangu maana wanakuja tu hapa home wala hawaelewi ukiwaambia wakae mbali. Mama yangu nae anakuja sana na umri yeye umeenda isitoshe nae tangu jana anadai anatapika mara kwa mara na mwili kuchoka sana Nachanganyikiwa kabisa mdugu zangu.
 
Attachments

  • FullSizeRender.mov
    58.3 MB
Nilienda nikamweleza Dr. hali halisi lakini nikapewa dawa za kifua tu yaani kiufupi hizi hospital za kawaida changamoto ndio maana nataka niende hosptal inayo shughulikia ikiwemo kupima
Pamoja na mengine .... Chemsha maji yachemke kabisa Kama ya kunywa, kamulia Malimao 3, weka na chumvi robo kijiko kidogo. Kunywa ikiwa ya Moto.
 
Back
Top Bottom