Ushauri: Chadema ijiondoe kwenye vikao vya Maridhiano na CCM

Ushauri: Chadema ijiondoe kwenye vikao vya Maridhiano na CCM

Nani anashida ya kuonana na wapuuz na toka lini tanzania kuna mahakama au genge la wapumbavu wa ccm linaloitwa mahakama mapoyoyo kama wewe ndio unaliita mahakama yani toka lini mahakama ikapigiwa simu?
Wapumbavu ni hao magenge yenu mnaotaka kupotosha , sasa mumegaragazwa mchana kweupee
 
Wakuu natanguliza Salamu , na baada ya salamu hii naingia moja kwa moja kwenye hoja.

Turudi nyuma kidogo ili tufahamu msingi mkuu wa kuanzishwa kwa hiki kinachoitwa maridhiano kati ya CCM na CHADEMA.

Maridhiano kati ya vyama hivi viwili , kimoja cha dola na kingine cha Wananchi, yalianzishwa kwa ghilba na ccm ili kuudanganya umma kwamba aliyekuwa anafanya unyama kwenye utawala wa awamu ya 5, yaani kuteka, kuua , kubambika kesi na kunyanyasa watu ni Dr Magufuli peke yake, na sasa kwa vile hayupo basi sisi tuliobaki turidhiane, kwamba wale waliokamatwa, waliofungwa, walioonewa, waliodhulumiwa, basi waachiwe ama mali zao zirejeshwe (NEVER AND NEVER AGAIN), na kwa kweli baadhi ya Wahanga wakaanza kuachiwa , wakiwemo viongozi wa Chadema Tunduma.

Nataka kuuthibitishia umma kwamba CHADEMA iliujua huu mpango wa ghilba na ilijua tu kwamba hautadumu, kutokana na ukweli kwamba Unyama uliotendwa haukuwa wa Magufuli peke yake, ulikuwa ni mpango wa ccm yote na vyombo vyao vya dola na watendaji wake, Isipokuwa kilichomponza Magufuli na wachache ni kuwa Front line kwenye unyama huo, huku wengine wakifanyia unyama wao nyuma ya Pazia.

Ushahidi wa karibu wa Jambo hili ni ule wa Kumbambikia Freeman Mbowe kesi ya Ugaidi, Mbowe alibambikwa kesi hii Wakati Magufuli hayupo, hii maana yake ni kwamba Katili ndani ya ccm hakuwa Magufuli peke yake, Ushahidi mwingine wa wazi kabisa ni kupandishwa vyeo watu wote kuanzia Polisi hadi wanaccm waliotumika kufanya unyama kwenye serikali ya awamu ya 5, IGP Wambura, huyu ndiye alikuwa mtengeneza kesi zote za uongo dhidi ya Wapinzani wa serikali, Kingai Byakanwa, Humphrey Polepole, Dr Mahera, Ramadhan Kailima, Kagurumujuli na wengine wengi waliotumika kwenye unyama na kuminya Demokrasia, wamepewa vyeo vya heshima na Serikali ya Samia.

Maridhiano siyo hongo ya kunyamazisha watu wasijadili uchafu wa Bandari na DP WORLD au uchafu mwingine, sasa kwa vile CCM imeamua kutumia watu wale wale waliotumika awamu ya 5 kubambikia watu kesi za Ugaidi na Uhaini ili kuiuzia DP WORLD bandari za Tanganyika, hapa maridhiano hakuna tena.

Nashauri Chadema ijiondoe kwenye Maridhiano hayo haraka, turudi kule kule tulikokuwa, turudi kwa Wananchi ambao ndio wenye nchi, hii ni kwa sababu HAKUNA KITABU CHOCHOTE CHA MUNGU AMBACHO KIMEAGIZA WANADAMU WARIDHIANE NA SHETANI.

Nakala: Freeman Mbowe, John Mnyika
Kitendo cha serikali kukamata wananchi wa Mbeya ambao wakichoka kitu huwawanabishana na Mungu kusimamia wanachoamini wametangaza vita ambayo ni zaidi ya ile iliyomsumbua sanaJK enzi za utawala wake hadi akapopolewa mawe Tunduma na hakuwahi kukanyaga tena Mbeya mpaka anaondoka madarakani ndicho kinaenda kutokea kwa sasa
Wenye maombi waombe maana huko tuendako siko we are totally lost as vengeance shall not freeze

Spika Tulia amejiharibia kuamuru kufuatilia wananchi wanaompinga na kupinga madudu ya serikali hawawezi kumchagua hata kwa kitu gani kuanza sasa atarajie kususiwa kila kitu
 
chadema ni muhimu sana kuingia kwenye vikao ili wajifunze.

ukweli ni kwamba bado sana chadema wana mengi ya kujifunza kwenye siasa safi na shule pekee ni ccm
 
Kitendo cha serikali kukamata wananchi wa Mbeya ambao wakichoka kitu huwawanabishana na Mungu kusimamia wanachoamini wametangaza vita ambayo ni zaidi ya ile iliyomsumbua sanaJK enzi za utawala wake hadi akapopolewa mawe Tunduma na hakuwahi kukanyaga tena Mbeya mpaka anaondoka madarakani ndicho kinaenda kutokea kwa sasa
Wenye maombi waombe maana huko tuendako siko we totally lost as vengeance shall not freeze

Spika Tulia amejiharibia kuamuru kufuatilia wananchi wanaompinga na kupinga madudu ya serikali hawawezi kumchagua hata kwa kitu gani kuanza sasa atarajie kususiwa kila kitu
Atavuna anachopanda
 
Hakuna mwenye shida ya kuridhiana na nyie. Nyie ndio mlikua na kuherehere Cha maridhiano.
 
chadema ni muhimu sana kuingia kwenye vikao ili wajifunze.

ukweli ni kwamba bado sana chadema wana mengi ya kujifunza kwenye siasa safi na shule pekee ni ccm
Na kwa ushauri wangu huu subiri tamko la chama tu kuanzia sasa
 
Hayo maridhiano ya kitapeli tulisema toka mwanzo anayafahamu Mbowe na Samia + CCM. Hakuna haja ya maridhiano na majizi ya kura. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi pekee ndio yataleta maridhiano ya kweli. Ule utapeli wa kufundishwa uoga abaki nao Mbowe na wanaccm waliomuingiza mjini.
Kuna watu ni matapeli kuliko chadema?
 
Amani ya nchiii inalindwa kikamilifu na nchi itabaki salama siku zote. Wala usihofu, anayetamani nchi ichafuke, atachafuka yeyee
Nape alikuwa na akili kama yako lakini yalipomkuta alirudi kutupigia magoti
 
Wapumbavu ni hao magenge yenu mnaotaka kupotosha , sasa mumegaragazwa mchana kweupee
There should be an international appeal to blacklist the Tanzanian administration as the most transgressive regime that doesn't deserve to be supported and funded for anything
 
Mwalimu Nyerere,hakuwachekea wanaotaka kuvuruga amani.Hata aliodai nao uhuru,wakileta ujinga chamoto walikiona.Kina bibi Titi,Kina Fundikira,kina Kambona na wengineo.
Kwasababu Nyerere alikuwa anapenda kusujudiwa. Lakini Nyerere ndio aliyesababisha nchi hii tukavaa hadi viraka, na ndiye muasisi wa siasa za woga na kujipendekeza. Hawa chawa wa sasa ni zao la siasa mbovu za Nyerere.
 
Mwalimu Nyerere,hakuwachekea wanaotaka kuvuruga amani.Hata aliodai nao uhuru,wakileta ujinga chamoto walikiona.Kina bibi Titi,Kina Fundikira,kina Kambona na wengineo.
Kama vile walivyoshikishwa adabu masheikh wa Uamsho mpaka Mpemba mwenzao Samia ndio kaja kuwatowa.
 
Back
Top Bottom