Ushauri: Bunge lipitishe bajeti kuu ya Serikali haraka

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,732
11,725
Kwa mujibu wa katiba yetu, bunge ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kuidhinisha bajeti ya serikali, na katika vikao vinavyoendelea huko Dodoma wamekua wakijadili bajeti ya wizara moja moja.

Katika hali halisi sote tunajua kuwa bunge letu ni 'rubber stamp' tu ya serikali, hakuna bajeti yeyote iliyowahi kupingwa na bunge hili, chochote kinachowekwa mezani kinapita.

Sasa kuna haja gani ya kuendelea kuuana kwa corona kwa kuendelea na vikao ambavyo kiuhalisia havitakua na mchango wowote kwenye mgawanyo wa bajeti? Nashauri waziri Mpango awasilishe bajeti kuu ya serikali haraka na ipitishwe kisha bunge livunjwe. Achaneni na mijadala ya bajeti za wizara mojamoja.

Kama shida ni posho basi lipaneni zote ambazo mgelipana kwa kipindi chote, hatuwezi kuwazuia na hutujawahi kuwazuia hata kama hatupendi mtumizi yenu ya hovyo ya fedha za walipa kodi masikini wa taifa hili.

Niwaambie tu ndugu zangu kuwa fikra za mwenyekiti hazijali kuhusu afya zenu, yeye amejitenga kule kijijini alafu ninyi wengine mnaambiwa pigeni kazi, 'kolona' isiwazuiea, mtapukutika kama kuku wa kideli. Mlinzi namba moja wa afya yako ni wewe mwenyewe, usipojijali usitegemee mwenyekiti kukujali.
 
Naunga mkono hoja.
Hiyo mijadala haibadilishi chochote.
Wapitishe bajeti kuu warudi manyumbani mwao kila mtu akajilinde.
Baada ya Corona Bunge livunjwe.

2020
 
Acheni Watu waendelee na kazi jaman
Kwahiyo unadhani dunia itasimama kisa Corona?
Maisha yanaendelea watu wanasonga mbele tu
Nasisitiza Corona ni ugonjwa Mdogo ukiwa na familia yako umeme kwa Jina la Yesu tu.
Biashara imeisha
 
Pumba
Kwa mujibu wa katiba yetu, bunge ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kuidhinisha bajeti ya serikali, na katika vikao vinavyoendelea huko Dodoma wamekua wakijadili bajeti ya wizara moja moja.

Katika hali halisi sote tunajua kuwa bunge letu ni 'rubber stamp' tu ya serikali, hakuna bajeti yeyote iliyowahi kupingwa na bunge hili, chochote kinachowekwa mezani kinapita.

Sasa kuna haja gani ya kuendelea kuuana kwa corona kwa kuendelea na vikao ambavyo kiuhalisia havitakua na mchango wowote kwenye mgawanyo wa bajeti? Nashauri waziri Mpango awasilishe bajeti kuu ya serikali haraka na ipitishwe kisha bunge livunjwe. Achaneni na mijadala ya bajeti za wizara mojamoja.

Kama shida ni posho basi lipaneni zote ambazo mgelipana kwa kipindi chote, hatuwezi kuwazuia na hutujawahi kuwazuia hata kama hatupendi mtumizi yenu ya hovyo ya fedha za walipa kodi masikini wa taifa hili.

Niwaambie tu ndugu zangu kuwa fikra za mwenyekiti hazijali kuhusu afya zenu, yeye amejitenga kule kijijini alafu ninyi wengine mnaambiwa pigeni kazi, 'kolona' isiwazuiea, mtapukutika kama kuku wa kideli. Mlinzi namba moja wa afya yako ni wewe mwenyewe, usipojijali usitegemee mwenyekiti kukujali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri Wa wstaalamu ungezingatiwa, hawa wabunge wawekwe karantini kwa Siku 14 kisha wapimwe, wale wazima waendelee kupiga kazi ili kutimiza matakwa ya rais wote kuchapa kazi.
 
Bunge linapitisha PAST TENSE budget badala present tense budget.Hiyo pesa wanazopitisha watazipata wapi katika hali ya sasa?
Walitakiwa wajadiri bageti ya kupambana na Covid-19 kitu ambacho hawakufanya.
Usishangae ile supplementary budget ndio itakuja kuwa main budget. Kwa sasa wangetulia tu kwenye majimbo yao.
 
Back
Top Bottom