Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,702
- 11,635
Kwa mujibu wa katiba yetu, bunge ndicho chombo kilichopewa mamlaka ya kuidhinisha bajeti ya serikali, na katika vikao vinavyoendelea huko Dodoma wamekua wakijadili bajeti ya wizara moja moja.
Katika hali halisi sote tunajua kuwa bunge letu ni 'rubber stamp' tu ya serikali, hakuna bajeti yeyote iliyowahi kupingwa na bunge hili, chochote kinachowekwa mezani kinapita.
Sasa kuna haja gani ya kuendelea kuuana kwa corona kwa kuendelea na vikao ambavyo kiuhalisia havitakua na mchango wowote kwenye mgawanyo wa bajeti? Nashauri waziri Mpango awasilishe bajeti kuu ya serikali haraka na ipitishwe kisha bunge livunjwe. Achaneni na mijadala ya bajeti za wizara mojamoja.
Kama shida ni posho basi lipaneni zote ambazo mgelipana kwa kipindi chote, hatuwezi kuwazuia na hutujawahi kuwazuia hata kama hatupendi mtumizi yenu ya hovyo ya fedha za walipa kodi masikini wa taifa hili.
Niwaambie tu ndugu zangu kuwa fikra za mwenyekiti hazijali kuhusu afya zenu, yeye amejitenga kule kijijini alafu ninyi wengine mnaambiwa pigeni kazi, 'kolona' isiwazuiea, mtapukutika kama kuku wa kideli. Mlinzi namba moja wa afya yako ni wewe mwenyewe, usipojijali usitegemee mwenyekiti kukujali.