Ushauri BRT UBUNGO

Kero ya foleni hapa ubungo ni balaa hususani kwa wakazi wa kimara,mbezi na kuendelea. Yani ubungo ndo kitovu cha foleni na ukizingatia na ujenzi unaoendelea tabu tupu. Ushauri wangu kwa wajenzi ktk eneo la ubungo hapa wajenge masaa 24 usiku na mchana ili wamalize tatizo hili sugu japo kidogo tu.
Mie niliisha acha kwenda kazini na ki-low consumption changu long ago,maana kuna siku kilikuwa half tank nimetoka nacho ofisi kufika Kimara mwisho mafuta yamekauka wakati yalikuwa ni mafuta yangu ya siku 2 kwenda ofisi na kurudi home.Wacha kwanza nichange za Xmass na ada za watoto ntaanza kwenda nacho kazini kuanzia January.
 
Bora wangetuwekeaga li treni huku mbezi. Kwa hzi foleni mtu unakosa ela hivi hivi unajiona.

Bora ndugu yangu ukose hela inatafutwa wenzio tushapoteza roho ya mtoto kwa ajili ya foleni, mtoto wa mdogo wangu tumemuacha vizuri asubuhi anakunywa chai mara degedege limempata basi hiyo sumbuka yake mpaka tumepata maarifa wageuke waende tumbi mtoto kesha nyooka. Hospitali hizi ndogo walikuwa wanamkataa.
 
sasa ni saa ngapi?

Angalia muda kwa juu ya post yangu ndiyo utajua muda niliokuwa naseme nimefika, mfano wewe ulivoniuliza kwamba sasa ni saa ngapi ilikuwa saa Today 13:22 kwa hiyo angalia comment yangu nimecoment saa ngapi ili ujue ilikuwa saa ngapi
 
Back
Top Bottom