Ushauri BRT UBUNGO

Ushauri BRT UBUNGO

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
2,545
Reaction score
3,370
Kero ya foleni hapa ubungo ni balaa hususani kwa wakazi wa kimara,mbezi na kuendelea. Yani ubungo ndo kitovu cha foleni na ukizingatia na ujenzi unaoendelea tabu tupu. Ushauri wangu kwa wajenzi ktk eneo la ubungo hapa wajenge masaa 24 usiku na mchana ili wamalize tatizo hili sugu japo kidogo tu.
 
Kutoka mbezi kufika ubungo ni safari nzima ya morogoro-Dar
 
Nmesikia watajenga fry-over hapo ila sielewi cz hata maandalizi sijayaona
 
Kero kero kero
 
Mimi ndiyo nimefika hapa posta mpya tokea saa 0645 alfajiri nipo kituoni pale Mbezi Kibanda cha mkaa hakuna hata gari iliyokuwa inatokea,ni majanga plus majanga
 
Bora wangetuwekeaga li treni huku mbezi. Kwa hzi foleni mtu unakosa ela hivi hivi unajiona.
 
jana nilitumia 4 hrs temboni mpaka ubungo!aisee nilichukia hatari,japo wameanza kufanya ujenzi 24 hrs
 
Mimi ndiyo nimefika hapa posta mpya tokea saa 0645 alfajiri nipo kituoni pale Mbezi Kibanda cha mkaa hakuna hata gari iliyokuwa inatokea,ni majanga plus majanga
kesho simama hapo kibanda cha mkaa nitakupa lift ya pikipiki
 
Yaaani ni tabu tupu. Mke wangu asubuhi kapaki gari stop over akachukua pikipiki.
 
Siku za sikukuu na jumapili, mara nyingi huwa hawajengi barabara...lakini hawafungui barabara walizofunga..Kimara na Mbezi ni jahanamu kamili.

Pale Kimara Mwisho wametengeneza barabara mithili ya nyoka kwa jinsi ilivyopinda pinda... barabara ya mwanzo ilinyooka, wao wameweka "Spiral". Kile ni chanzo cha ajali siku za mbeleni. magufuri uko wapi...ndio mchoro ulio usaini ule?
 
Poleni wakaazi wa huko! Miye naonaga tu nikiwa kwa mibasi mikubwa asa nyie mnaotumia daily duu majanga!!
 
Nmesikia watajenga fry-over hapo ila sielewi cz hata maandalizi sijayaona

Nitaoga vumbi likitokea hili. Fly over haitokei tu kizembezembe bila kukubali kuhamisha vinu vya Tanesco. Eneo dogo sana
 
yaani hii foleni ni noma nimetoka Kimara saa 4 asubuhi lakini nimefika Ubungo saa 6 na nusu mchana
 
Back
Top Bottom