Ushauri:Baada ya ATCL tuhamie STAMICO

onyx

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
1,587
1,316
Wakuu heshima zenu,

Ningependa kutoa wazo ambalo linanijia kichwani mwangu namna ya kujikwamua na uchumi wa viwanda. Mkuu yeye ameonelea aanze kutengeneza ajira na kukuza uchumi kwa kuipa uwezo ATCL.Sio jambo baya, ni zuri pia, maana kupanga ni kuchagua. Ila ningependa kushauri baada ya kumalizana na ATCL tungewekeza pia STAMICO. Kwa wasiofahamu ni kwamba STAMICO ina maeneo mengi nyeti ya uwekezaji, ila tatizo ni mtaji. Nimeonelea kulizungumza hili nikiwa mdau wa sector ya madini kwa kipindi kirefu, kama tukiipa nguvu STAMICO, tutazalisha ajira nyingi, na pia serikali ingeingiza mapato mengi sana.

STAMICO ni shirika nysti sana, ila bado halijapatiwa fungu la kutosha kuweza kuchangia pato la taifa, na wana vyanzo vingi vya madini ila mtaji bado haujakidhi kuweza kuanzisha migodi na kuchangia pato la taifa.

Ni mtazamo tu
 
safi sana! haya ndio mawazo muhimu na yanaonesha kuwa nchi ina vijana ambao wanaweza kuwa 'think tank' ya taifa, kuliko mda wote kulalamika na rambirambi, bashite au kupinga kila kitu. STAMICO linaweza kuchangia kwa haraka kukua uchum kupitia sekta ya madini, vijana watapata ajira. Tena kwa mtazamo wangu, madini adimu kama tanzanite haikutakiwa kupewa wawekezaji, serikal ilitakiwa kumonopolize kupitia STAMICO. serikari iipe uwezo wa kifedha na ikiwezekana shirika lisukwe upya. wawekezaji wababaishaji, wasiolipa kodi tusingeweza kuwavumilia enda shirika letu lingekuwa imara.
 
Upo sawa mkuu
 
Back
Top Bottom