Ushauri: Alisema baba yangu anamtaka, lakini sasa yeye ananitaka

Ushauri: Alisema baba yangu anamtaka, lakini sasa yeye ananitaka

apprentice1997

Senior Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
107
Reaction score
99
Habari za muda wadau, mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 18. Kuna jambo linanitatiza sana nikilifikiria nashindwa kulielewa lipoje.

Ishu ipo hivi, mwanzoni mwa mwaka huu nilikabidhiwa moja ya ofisi ya mzee niisimamie, mzee wangu ni mwalimu wa sekondari na hii ofisi ipo karibu sana na shule anayofundisha mzee, kutokana na kufahamika nikajuana na wanafunzi wanaofundishwa na mzee na mmoja wapo ni binti fulani hivi ambaye yupo kidato cha pili.Tulikuwa marafiki wa kawaida tu na baadae akaanza kuzidisha ukaribu na mimi kiasi cha kufikia hatua ya kuniagiza pedi na kuniambia hata mzunguko wake wa hedhi. Mimi nilichukua kawaida tu sababu nilikuwa nasimamia duka kwa hiyo nikaona ni moja ya kazi yangu kuhudumia wateja.

ilitokea siku moja nilikasirika nikaongea kwa ukali na mmoja wa marafiki zake huyu binti kiukweli niliongea maneno makali sana (sikutukana) na baadae nilikuja kuyajutia nikaomba msamaha kwake. Kabla sijajua kosa langu huyu binti wa form two alinifata na kunambia umefanya kosa kubwa nikamuomba msamaha na kumwambia sikuongea kwa nia mbaya na sikufikiria kuwa maneno yale yangekuwa mabaya mimi nilidhani labda nilikuwa namsaidia kumbe nakosea. Basi nikanyenyekea nikaomba msamaha kwa wote nikasamehewa.

Urafiki wetu ukazidi kukua kutokana na ukweli kuwa ameniambia ukweli basi mimi nikaona na mtu anayefaa kuwa rafiki tu pale shuleni kwao na nikamuamini. kutokana na yale mazoea akaanza kuniandikia vimemo na mimi nikawa navisoma nakumjibu kwa vimemo vile kwa kuwa muda wa kukaa ofisini kwangu ulikuwa mdogo na tungeweza kuhisiwa vibaya mimi na yeye. Ndipo siku moja akaniandikia kimemo na kuniambia kuwa kuna jambo linaendelea pale shuleni na linamtatiza kiasi cha kumfanya awe na maendeleo mabaya kimasomo, mimi nikamuomba aniambie akataka kusita baadae nikamlazimisha na kumuahidi kuwa nitachukua kila jambo kama lilivyo na wala sitapanic ndipo akaniambia kuwa baba yangu anamtaka kimapenzi na amekuwa akimsumbua sana, kiukweli iliniuma nikajikaza kiume ukizingatia binti mwenyewe yupo kidato cha pili.

Nikajikaza nisipanic nikamuomba msamaha sana, baadaye nilikuja kumweleza kaka yangu jambo hili na hakunipa jibu lolote. Basi baada ya kuniambia hivyo mimi nikaanza kuona aibu kiasi kukaa na yule binti na nikajaribu kumkwepa lakini yeye akawa anazidi kunisogelea akaanza kuniletea vimemo vyenye msg za mapenzi mara nyingi ananiambia kuhusu siku zake, ndipo ikatokea siku nilikuwa naumwa huyu binti alileta kimemo na kikawa kina msg za mapenzi, baadae baada ya kuja kuchukua majibu tukajikuta tumekulana mate, basi ikawa ndio hivyo hivyo akaanza kuleta vishawishi na kuonyesha dalili za kunitaka kimapenzi ikapelekea mimi na yeye baadae tukawa wapenzi ila hatukufanya mapenzi. Nakumbuka kuna siku kulikuwa na sherehe shuleni hivyo tukacheza mziki na siku hiyo nilijikuta nimemshika sehem mbaya sana mwili wake ikaishia hivyo.

Nilifikiria sana, kwanza huyu binti alisema baba yangu anamtaka iweje aje kuanzisha uhusiano na mimi kama ni kweli hilo tukio lilifanyika?. Anasema anamuogopa sana baba yangu lakini akakubari kuja dukani kwake usiku na kufanya hayo mambo ya kimapenzi na nikaamini pengine huyu msichana alimtumia baba yangu kama chambo cha kuninasa mimi na uwenda sio kweli kabisa hakutongozwa ila ni mbinu tu ili aweze kuwa karibu na mimi. Nikafikiria maisha yangu, heshima yangu na future yangu nikaamua kuachana na huyu binti na kujikita katika kufanya project zangu zinazonitangaza nikaanza kuandika kitabu changu cha kwanza. Kiukweli ule uamuzi ulinipa nguvu kubwa sana na nikafanikiwa kufanya hii kazi na hata nilipokuwa namuona sikuwa na muda nae kwa kuwa nilikuwa busy sana na niliamini ili nifanikiwe ni lazima niweke mambo yote pembeni na kweli nikafanikiwa kumaliza hiki kitabu.

Nikaondoka pale mahali na kurudi mjini yalipo makazi yetu na huyu binti bado anaendelea kunifatilia sana, kiasi cha kunambia yeye ni bikra mimi sikutishika nikaendelea na kazi zangu imefika mahala huyu binti anaazima hadi simu ya shule ili anipigie mimi na sielewi kwa nini anafanya hivi. Maswali ninayojiuliza ni kama yafuatavyo:
  1. Nini lengo la huyu msichana kwangu, kama anajua fika kuwa mimi siwezi kuendelea nae na bado ananisumbua?
  2. Kwa nini aliamua kuniambia kuhusu baba yangu, nikiamini kuwa jambo hili hakuna binti anayeweza kusema hasa kwa kuzingatia uhusiano uliopo baina yangu na baba yangu, Je alisema akiwa na nia mbaya au nia nzuri?
  3. Kwa nini alitaka kuanzisha mahusiano na mimi hata baada ya kuniambia kuhusu baba yangu, lengo lake ni nini?
  4. Kama jambo hili si kweli kwa nini aliamua kusema maneno haya, je nia yake ni kutugombanisha mimi na baba yangu?
  5. atafaidika nini endapo atakuwa na mimi?
Kwa tabia huyu binti anaonekana ni mcharuko na mtoto wa mjini.
ninatafakari ni jinsi gani niataupata ukweli, marafiki zangu waliniambia kuwa nikifanya nae mapenzi ataniambia ukweli wote je njia hii inaweza kuwa na ukweli. Kama haitawezekana nifanyeje niujue ukweli wote.
Moyoni mwangu nimesamehe na wala sina mawazo mabaya kabisa kuhusu baba yangu na sidhani kama jambo hili ni ukweli. Naombeni wadau mnifungue macho. Asante
 
achana naye mpotezee kabisaa, hayo maswali hayatakusaidia lolote
 
Mbona rahisi mdogo wangu,una mkepwa tu,akipiga simu upokei,wala ujibu msg,mwenyew atachoka..kingine usile mate ya mwanafunzi ogopa sana hao watoto..la sivyo miaka 30 itakuwa halari yako
 
Maswali yako yote 5,yanafanana!umegeuza lugha!
Wewe kama hautaki mwambie wazi,hamna namna nyingine.
 
Watanzania bwan, yaani hii habari unaona ndefu alafu ipo kwa kiswahili.

Vipi kurasa 200 za lugha ya malkia.
 
Bado unamtaka ila akili yako haijakaa sawa... Itakua mzee alichukua "teaching allowance" sisi wanaume katika papuchi hatuaminiki
 
Kuna haja ya kufanya uhakiki wa membaz na kufungua jukwaa la watoto
 
Back
Top Bottom