nimeupenda ufafanuzi wako.
je na nikihitaji laptop kwa matumizi ya engineering designs.. kama autocad na wenzie.. pia kwa shughuli za internet kama blogging ni ipi itafaa?
autocad ndio software yako kubwa zaidi? kama kuna nyengine kubwa kushinda autocad nitajie,
processor
tafuta processor yoyote ya intel 4th generation inayoishiwa na m kwa mbele
i3- 4000m au 4100m
i5- 4200m au 4300m
i7- 4600m
processor zinazoishiwa na m zinaruhusu ram hadi 32gb hivyo unaweza nunua laptop ya 4gb ram then ukaongeza mwenyewe, pia zina thermal design power kubwa hadi watts 35 hivyo hata ifanye kazi kubwa haiwezi kushuka ufanisi tofauti na aina nyengine ya processor. hizi zinazoishiwa na m gpu yake pia ni kubwa kwa ajili ya graphics.
display na graphics
autocad wanaruhusu kioo cha 720p ila wanarecomend cha 1080p, kama utatumia display ya 720p basi gpu inayokuja na processor itatosha mambo yako ila kama utataka kioo kizuri zaidi cha 1080p itabidi hio laptop iwe na graphics za nvidia.
ram
jamaa wanataka 4gb ila wanarecomend 8gb
windows
jamaa wanaouza laptop wana tabia ya kuekea watu 32bit, kwa kazi yako hakikisha windows ni 64bit kwani hii 64bit ina perfomance kubwa sana.
hapa itategemea na budget yako sasa kama hautaki kuspend hela nyingi
-laptop ya i3/i5 yenye 4gb ram na 500gb hdd kioo cha 1300x766 na windows ya 64bit
au kama hela ipo unaweza nunua
-laptop ya i5/i7 yenye ram 8gb kupanda na dedicated nvidia graphics, iwe na ssd badala ya hdd, kioo cha 1920x1080 pamoja na windows ya 64bit.
kwenye display pia una option ya kununua monitor, ukiwa nyumbani unachomeka laptop na monitor pamoja ili kufanya kazi za 1080p