Ushamba wa Mzee wa Mwandiga Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushamba wa Mzee wa Mwandiga Kigoma

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kazikubwa, Sep 19, 2012.

 1. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwijano alidhamiria kuja mjini Dar ili aungane na wenzake katika biashara yao ya kuuza vyombo vya nyumbani kwa kuvitembeza majumbani kwa mikopo. Baada ya kuuza ndizi na mahindi aliamua kupanda Treni kuja Dar. Kwa taarifa zenu, watu wa kigoma wakijaa treni yenye behewa 15 ujue waliolipa hawazidi behewa moja wengine hupanda bure kiujanja ujanja kwa kuwakwepa coaches attendants na wakagua tiketi (T.T).

  Aliamua kuto nunua nguo mpya hadi atakapofika Mji Kasoro Bahari (Morogoro) au Dar ili apate mapigo ya kisasa. Kama bahati vile, treni ilichelewa na hivyo kufika Moro asubuhi badala ya usiku. Hii ilikuwa fursa nzuri kwake kufanya shoping la kufa mtu. Alipoingia mjini huku akiwa na haraka ya kutoachwa na treni aliingia dukani kwa wasela na kununua chap chap.

  Alipokaribia station ya Pugu Dar aliamua kwenda chooni ili abadili nguo na kupiga vitu vya kisasa. Kabla ya kufungua bahasha alianza kuvua nguo zake alizovaa na kuzitupia dirishani huku treni ikiwa katika mwendo. Alikuwa akijitapa kuwa hawezi kuvaa malapulapu wakati anatinga jijini nusu saa tu ijayo.

  Mama nyangu, Mwijano amepatikana, alipofungua bahasha kumbe ilikuwa kanyaboya, walimwekea shumizi (vest) na matambara tu, jamaa alichanganyikiwa ile mbaya maana hana nguo tena, kilichojiri wewe buni....
   
 2. a

  ammah JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Old is gold!
   
 3. p

  pretty n JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heeh nahc cku hyo aliziona rangi zote
   
 4. MatikaC

  MatikaC JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,200
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  aliuziwa mbuzi kwa guniaaaaa....
   
 5. Mtanzanika

  Mtanzanika JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 2,213
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  alipata Diploma
  ...akifika Dar anakamata degree!!
   
Loading...