Ununuzi wa injini na behewa za abiria na mizigo kwa matumizi ya reli ya kisasa - SGR

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595

UNUNUZI WA INJINI NA BEHEWA ZA ABIRIA NA MIZIGO KWA MATUMIZI YA RELI YA KISASA - SGR

Shirika la Reli Tanzania - TRC limetoa ufafanuzi juu ya ununuzi wa injini na behewa za abiria na mizigo kwa matumizi ya reli ya kisasa - SGR kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano TRC jijini Dar es Salaam Juni 15, 2022.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi. Jamila Mbarouk ameeleza kuwa TRC inafanya manunuzi ya behewa za mizigo, behewa za abiria, seti za treni za kisasa pamoja na vichwa vya treni ya umeme kwa mgawanyo wa awamu mbili.

Bi. Jamila alisema kuwa awamu ya kwanza ya ununuzi wa vifaa vya uendeshaji wa mtandao mzima wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa SGR Dar es Salaam - Mwanza yenye urefu wa kilometa 1,219 ambapo muda wa manunuzi ni miezi 36 hadi 48, pia manunuzi ya pili ni ya vichwa na behewa kwaajili ya majaribio na endeshaji wa awali ambapo muda wa manunuzi ni miezi 9.

“Manunuzi yamefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011, pamoja na marekebisho ya mwaka 2016 na kanuni za mwaka 2013 na marekebisho ya kanuni ya mwaka 2016” alisema Bi. Jamila.

Aidha, Bi. Jamila alieleza kuwa katika kuhakikisha uendeshaji wa awali unaanza mara baada ya majaribio, TRC ilisaini mkataba wa muda mfupi wa ununuzi wa vichwa vya treni ya umeme viwili na behewa 30 za abiria vitakavyofanyiwa ukarabati kutoka kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki.

Hata hivyo Bi. Jamila aliongeza kuwa kampuni ya Eurowagon imeshindwa kutimiza matakwa ya mkataba huo ambao ulitakiwa kukamilika mnamo mwezi Novemba, 2021.

“Ujenzi kipande cha kwanza Dar es Salaam - Morogoro upo hatua ya mwisho, hivyo TRC iliamua kusitisha mkataba kwa barua mnamo tarehe 25, Februari , 2022” alisema Bi. Jamila

Vilevile Bi. Jamila alisisitiza kuwa TRC inaendelea na jukumu la kumalizia ukarabati bila gharama na vifaa vinatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2022.

Naye Mkurugenzi wa Ujenzi na Miundombinu Mhandisi Machibya Masanja alisema kuwa TRC ilisaini mikataba ya manunuzi ya behewa mpya 1,430 za mizigo kutoka kampuni ya CRRC ya nchini China, behewa mpya za abiria 59 kutoka kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology Limited kutoka nchini Korea ya kusini, seti 10 mpya za treni za kisasa zenye jumla ya behewa 80 na vichwa 17 vipya vinavyotumia nishati ya umeme kutoka kampuni ya Hyundai Rotem ya nchini Korea kusini kwaajili ya uendeshaji wa reli ya SGR.

“Gharama ya mikataba ni shilingi Trilioni 1.18 na ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji “ alisema Mhandisi Machibya.

Mhandisi Machibya alieleza kuwa mikataba hiyo ya ununuzi imetolewa katika kampuni mbalimbali ambazo zilitaja bei nzuri ya manunuzi.

Pia Mhandisi Machibya alisema kuwa ujenzi wa SGR unajengwa kwa ufanisi na kuhakikisha usalama kwa wananchi kwa kujenga vivuko katika njia ya reli ikiwemo kivuko cha wanyama, binadamu na vyombo vya usafiri.

“Usanifu na ujenzi wa SGR tumezingatia mazingira halisi ya mtanzania“ alisema Mhandisi Machibya.

Ujenzi wa SGR kwa awamu ya kwanza Dar es Salaam - Mwanza unaendelea vema na mchakato wa manunuzi ya mkandarasi wa ujenzi wa awamu ya pili kwa kipande cha Tabora - Kigoma unaendelea.
 
Asante kwa taarifa hii muhimu, ya Juni 15, 2022, ambapo mimi ni mchangiaji wa 5, yaani bandiko la hoja muhimu kama hii wachangiaji 5!, lakini pandisha bandiko la Mondi na Zari au Wema, utashangaa!.
P
 
MADAI
Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).

Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.

TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.

Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020

Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)

EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRC kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)

Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRC hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.

TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC

Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.

TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.

View attachment 2424063
Hapa ninachokisoma na kinachokanushwa ni vitu viwili tofauti, kwanza Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba ya mwaka '1947'!.
2. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!.
3. Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.
4. Jee hivyo vichwa viliundwa lini, wapi na vimetumika muda gani kabla sisi hatujauziwa?.
5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani na inakarabatiwa kwa bei gharama gani?.
5. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?.
6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.
7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, jee kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.
8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.
9. Tulivinja mkataba wa Dowans, watu wakajiapisha "over my dead body", tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.
10. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo mitumba!.
11. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans tuliovunja, kwa gharama zile zile na tukawalipa!.
12. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule, huku nyuma, sio tuu tumelipa, bali pia tumeinunua ile mitambo kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni mtumba hatununui, sasa ni mali yetu na malipo yote yaliisha fanyika chap chap!, ila Watanzania hatuambiwi!.

Tuambiwe tuu ukweli!.

I cant believe tumenunua mabehewa mitumba na vichwa kutumika kwenye reli iliyotugharimu trillion sita, hapa mtu lazima afungwe na kutapishwa 10% zote, wamezidi kuona watanzania wajinga, hii haiwezekani
 
Asante kwa taarifa hii muhimu, ya Juni 15, 2022, ambapo mimi ni mchangiaji wa 5, yaani bandiko la hoja muhimu kama hii wachangiaji 5!, lakini pandisha bandiko la Mondi na Zari au Wema, utashangaa!.
P

Ww mwenyewe wakati wa hiyo taarifa ilipotolewa hukuchangia, ulikuwa kwenye taarifa hizo hizo za kina Zari. Watu wanaona bora hizo taarifa za kina Mondi za udaku, kuliko hayo mambo ya serikali yenye uongo mwingi wa kusaka kiki za kisiasa.
 
Back
Top Bottom