Ushaiona ha hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushaiona ha hii?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by ELNIN0, May 25, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula. Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

  Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza, ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.

  Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

  Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

  Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia Mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza
  akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake wa kike na mkewe anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

  Mama akasema nashukuru sana Mume wangu kwa hayo yote, Basi naomba nani nitubu kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

  Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mle ndani.

  Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza, Baba na Mama mnagombania nini humu ndani, badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule
  nnje?

  Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

   
 2. M

  Mswahela Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ah bwana hii ni ya zamani kidogo ilikwishatolewa na Fr Bahati pale Changombe mwaka juzi 2008.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  ipotezee mkuu - ngoja nikupe nyingine copy right yangu.....
   
Loading...