Ushahidi Watz tuna IQ Ndogo!

Ushahidi Watz tuna IQ Ndogo!

Mkuu Mzee Mwenzangu, labda wewe wanaweza kukuelewa kwa mifano mizuri uliyoitoa. Nimejaribu sana kuwaelewesha lakini nimeambulia matusi.

Mkuu ungekuwa unafuatilia siasa za kimataifa ungegundua kuwa unachoongea ni PUMBA.
Anzia ugomvi wa Kenya na Uganda juu ya kisiwa ndani ya ziwa Victoria, Sasa hivi Ukrein na Urusi, Sudani Kusini na Kasikazni, Mali (bamako) na Tualregie.....
Kuna sababu mbili kubwa, maslahi ya taifa, kiuchumi, kiusalama..., masilahi ya viongozi wa pande zote mbili, fuatilia Muungano wa Unguja na Tanganyika ulikoanzia utakuta kulikuwa na maslahi pande zote, Nyerere aliona ili awe salama na Waingereza wake lazima aiweke Zenj mikononi, huku Karume akiwa na Wa komunist alikuwa na hatari ya kupinduliwa hivyo naye akaona bora aungane awe na nguvu.
Rudi katika historia naamini utaufuta huu uzi.
 
Ushahidi kwamba Watz tuna IQ ndogo ni huu kuhusu malumbano na Zanzibar! Kwa nini nasema hivyo, ukiangalia Zanzibar ina kilometa za mraba takribani 2600 (2600 km²) na Watu wasiofika Milioni moja (1,000 000) wakati Tanzania Bara ina zaidi ya kilometa za Mraba laki tisa(>900 000 km²) na watu wanaozidi milioni 40 (40 000 000) lkn tunapoteza Muda, Nchi nzima kujadili haki yetu ya kupata ardhi Zanzibar, tupoteza Muda kujadili eti kupewa haki sawa na Zanzibar ktk Muungano...

Hakuna Binadamu yoyote mwenye IQ kubwa ambaye anaweza kupoteza muda kujadili mambo yenye uwiano kama Huo! Nasema Dunia nzima hakuna, ni sisi tu!

Hivyo wanaotafuta mchawi wa kwa nini sisi ni Masikini jibu lipo nalo ni moja tu, IQ!
IQ ndio ya kulaumu, yaani uwezo wa kuona na kuamua ni mambo gani ya kuyapa Kipaumbele ktk Maisha ndio mwisho wa siku unaamua ni nani aweze kuendelea kiuchumi na nani azidi kubakia kuwa Masikini...

usiseme wantanzania tuna IQ ndogo sema wewe na ha jamaa zako na baadhi na ndugu zako mimi na jamaa zangu na ngugu zangu ni watanazania pia usitujumuishe na huo upuuzi wako mtu mwenye IQ ndogo ni wewe ambaye uwezi tumia logic tu kuna watanzania wangapi kwa idadi na wamedai wangapi wanataka ardhi zanzibar akili ya kushikiwa iyo
 
sio kwamba watu hawana IQ wanazo ila uzalendo hakuna kwa watu wengi sio ma prof wala wasio na shule tamaa ya wachache hata kama kitu ni sensitive hawafikirii long term planning
 
Wewe ndo una IQ ndogo. Issue ya Zanzibar ni sensitive sana. Kwa waona mbali huwezi ukaijadili kijuu juu tu. Huna data unaposema "Hakuna Binadamu yoyote mwenye IQ kubwa ambaye anaweza kupoteza muda kujadili mambo yenye uwiano kama Huo! Nasema Dunia nzima hakuna, ni sisi tu!. Kam unafuatilia vyombo vya habari utaelewa ni kwanini Urusi ana nchi za Europe na Marekani zinataka ushawishi wa nchi ya Ukrane hasa kisiwa cha Crimea. Ujiulize kwani vita ya Uingereza ilipigana vita kugombea kisiw cha Falkland wakati kisiwa hicho kipo karibu Km 12734 kutoka Uingereza. Kaka no reserch, no right to speak.

Umemjibu vizuri yeye ndo mwenye IQ ndogo, Zanzibar ni nchi, ina hadhi ya nchi kama ilivyo marekani pamoja na udogo wake, udogo wa kijiografia hakuifanyi Zanziba kuwa na hadhi ya kinchi, kwahiyo watanganyika wakidai usawa huo wa Muungano ni haki yao, kama ambavyo na wao Zanzibar wanadai maswala yao kwenye Muungano.
 
Lakini Mungu anawapenda sana vilaza ndio maana kawaumba wengi mnooooo.
Sasa sijui ana maana gani.
 
Wewe ndo una IQ ndogo. Issue ya Zanzibar ni sensitive sana. Kwa waona mbali huwezi ukaijadili kijuu juu tu. Huna data unaposema "Hakuna Binadamu yoyote mwenye IQ kubwa ambaye anaweza kupoteza muda kujadili mambo yenye uwiano kama Huo! Nasema Dunia nzima hakuna, ni sisi tu!. Kam unafuatilia vyombo vya habari utaelewa ni kwanini Urusi ana nchi za Europe na Marekani zinataka ushawishi wa nchi ya Ukrane hasa kisiwa cha Crimea. Ujiulize kwani vita ya Uingereza ilipigana vita kugombea kisiw cha Falkland wakati kisiwa hicho kipo karibu Km 12734 kutoka Uingereza. Kaka no reserch, no right to speak.

Unaweza kusema pia Russia (Putin) wana IQ ndogo kung'ang'aninia Crimea?
 
thinking outside the box, leo umefungua watu macho, shida ni hawa Wazanzibar tuongea ongea bila kujua takwimu hizo kuwa after another 50years watakuwa hawana pa kwenda hivyo wangejifanya wajingaa siku ziende kizazi chao kipate makazi bara
 
Kisiwa cha Migingo hapo Lake Victoria, kinawatoa roho Kenya na Uganda! Hilo ni suala la IQ pia! Japan na China walikuwa wanagombea kisiwa kisichokaliwa kabisa, kina ukubwa wa KATA YA KKOO, je hawana IQ kubwa pia?

Point ni kuuvunja muungano, then tukae miaka 50, tutajua kama kulikwa na umuhimu wa huo muungano au Lah!?

Nyie hamuelewi kugombea umiliki na muungano ni mambo tofauti embu fikirieni vyema wote mliotoa mifano ya uingereza ufaransa Crimea na kadhalika
 
Ukisema Watz tuna IQ ndogo nakataa, kama umesoma mambo ya Genetics, haiwezekani sote genes zetu ziko identical, lazima kuna utofauti ukizingatia tunatoka katika matabaka tofauti, pia dada na kaka hawaoani. Sema baadhi ya Tatanzania

sawa lakini sample imeonekana kama watz wakawachagua watu kuwawakilisha wakawa wanafanya upuuzi kama wanaoufanya viongoz wetu IQ yetu inapimwa kwao kwasababu wao ndio wawakilishi wetu
 
Ushahidi kwamba Watz tuna IQ ndogo ni huu kuhusu malumbano na Zanzibar! Kwa nini nasema hivyo, ukiangalia Zanzibar ina kilometa za mraba takribani 2600 (2600 km²) na Watu wasiofika Milioni moja (1,000 000) wakati Tanzania Bara ina zaidi ya kilometa za Mraba laki tisa(>900 000 km²) na watu wanaozidi milioni 40 (40 000 000) lkn tunapoteza Muda, Nchi nzima kujadili haki yetu ya kupata ardhi Zanzibar, tupoteza Muda kujadili eti kupewa haki sawa na Zanzibar ktk Muungano...

Hakuna Binadamu yoyote mwenye IQ kubwa ambaye anaweza kupoteza muda kujadili mambo yenye uwiano kama Huo! Nasema Dunia nzima hakuna, ni sisi tu!

Hivyo wanaotafuta mchawi wa kwa nini sisi ni Masikini jibu lipo nalo ni moja tu, IQ!
IQ ndio ya kulaumu, yaani uwezo wa kuona na kuamua ni mambo gani ya kuyapa Kipaumbele ktk Maisha ndio mwisho wa siku unaamua ni nani aweze kuendelea kiuchumi na nani azidi kubakia kuwa Masikini...

Mkuu, rais wetu ana shahada ya uchumi na pia ni Docta. Alipoulizwa kwanini nchi yake ni masikini akasema na yeye hajui tena anashangaa. Unataka kutuambia na yeye ana IQ ndogo? Kuna jamaa mmoja huwa anapenda sana kujitapa kuwa yeye ni mchumi daraja la kwanza na ametangaza hadharani kuwa wakitafutwa watu watano wenye akili nyingi hapa Tanganyika eti na yeye hatakosekani. Huyu sidhani kama mtaelewana. Huyu ni mtaalamu na mfadhili wa kutengeneza kesi za ugaidi, iwe jua au baridi yuko na skaf yake shingoni kana kwamba shingo ni nyembamba haiwezi kubeba kichwa.
 
Haya yamekujaje tena.

Nilitaka mkuu anifafanulie maana nchi hii imejaa madokta na maprofesa wa kumwaga tena wengi wako katika bunge na baraza la mawaziri, sasa ndio nikashangaa kama na wao wapo kundini ndio nikampa mfano wa hao "wasomi" wawili!
 
Back
Top Bottom