Ushahidi wa LEMA dhidi ya Waziri Mkuu huu hapa

huyu mama kawekwa pale ili wamwendeshe nae bila kujiuliza kwa nini anawekwa wakati nae alikuwa anamkubali sita kaingia kichwa kichwa, ngoja wachinje kichwa chake..:clap2::clap2::clap2::twitch::twitch::laugh::laugh::laugh::laugh:
 


MAMA SPIKA ANNA MAKINDA, BUNGENI KUHESHIMIWE TU 'NGUVU YA HOJA'
KWA WASHIRIKI WOTE; UMRI, VYEO NA USOMI TUKASUBIRIANE MITAANI


Bungeni ndiko pekee mahala ambapo hata nyau tu huthubutu kumtazama moja kwa moja mfalme usoni huku mchezo ukichezwa kwa maneno mdomoni, akili kichwani na maspika wakiwa ni refasrii na washika bendera.

Nasema bungeni ndiko mahala ambapo mchezaji wa kulipwa au kepteni kwenye timu asipokaa vizuri hulambwa chenga mara kibao na wachezaji chipukizi; wengine ambao hata majina bado hawa. Ndio!! Bunge ndio uwanja wa siasa penye mazungumzo ya kistaarabu tu (vijembe, kejeli, na mizengwe mahala pake sokoni) huku kukiw ni kwamba kinachotafutwa kwa kiasi kikubwa ni kushawishiana mwelekeo wa mambo, kuridhishana UKWELI ULIPO, na kutatwa matatizo ya jamii iliowatumeni mahala pale.

Hivyo, hali iliojitokeza kati ya viongozi wetu Waziri Mkuu na Mbunge wa Sumbawanga na mwenzake Mbunge wa Arusha, Gdbless Lema, majuzi bungeni Dodoma, lina mengi mazuri ya kutufundisha kadri bunge letu linavyoendelea kuseheni viongozi vijana na wasomi, kuliko kuishia tu kwenye kutuhumiana UTOVU WA LABDA NIDHAMU na hata wengine kuonekana kule kwamba kila kitiririkacho toka vinywani mwao siku zote kibakia na kuendelea kuwa ni UKWELI NA UKWELI MTUPU!!!

Tusisahau pia kwamba siku zote watu tumezingirwa na minada ya kila aina katika maisha tunayoishi. Wakati mnada wa wafanyabiashara wa mitumba ni Mchikichini kwa Makamba Dar, mnada wa nyama ni Vigunguti, Simu za Wizi pale makutano ya barabara za Independence na Makungnya, ya wambeya vijiweni, na mnada wa silaha haramu toka Rwanda ni pale Kijitonyama Breakpoint, kwao wao wanasiasa mnada wao wa kuuza na au kutetea mawazo chini ya misingi inayoeleweka ni bungeni.

Mpaka hapo kwaza nitangulize po ngezi zangu kwa wabunge wa CHADEMA kwa namna ya pekee wanavyochangia kuweka VIWANGO VYA KIMATAIFA KATIKA UENDESHWAJI WA BUNGE LA VYAMA VINGI ambyo kwa bahati mbaya hayakuzoeleka katika nchi yetu ambayo imekwepo chini ya mfumo wa chama kimoja. Pia, kwa namna ya pekee nimpongeze Mhe Godbless Lema kwa utetezi w nguvu anaouleta bungeni dhidi ya madai ya Waziri Mkuu. Wadadisi wa mambo wanahofia kwamba endapo kutabainika kwamba Mhe Pinda alitoa majibu rahisi kwa maswali magumu basi ofisi ya spika itamchukulia hatua gani?? Jamani wabunge wa CHADEMA mko deepu saaana!! Duu, kwa mtaji wa utetezi huo sasa hapa ni patamu mnoooooooo!! Na sasa tunasubiri kweli kweli mwenendo mzima baada ya hapa tuone inavyokwenda.

Kweli sasa bunge letu si kama enzi zao Marehemu Amran Mayagila,Komanya, Joseph Rwegasira au Fredrick Msuya ambako mbunge kazi yake ilikua ni kuingia pale mjengoni na kuanza kuchapa usingizi waka mjadala ukiendelea huku akitajwa tu jina na spika wa wakati huo, Marehemu Chifu Adam Safi kumuuliza maoni yake juu ya mjadala unaoendelea, mara utasikia mtu mzima kaibuka ndotoni na udenda ukichuruzika, na kusilibia tu jibu lolote lile kama vile 'MHESHIMIWA SPIKA NAUNGA MKONO HOJA ASILIMIA KWA MIA KAMA ILIVYOSEMWA NA MVUNGUMZAJI ALIYETANGULIA'.

Sasa hivi kweli karibu kila mbuge, hasa wale wa upinzani ni watu ambao ni wadadisi wakubwa na wa kudadavua kweli kila nukta n kituo azungumzapo mtu bungeni na hada huku majukwaani mitaani. Ni watu ambao ni wafuatiliaji wakubwa wa mambo, WENYE NIDHAMU KUBWA KWA 'NGUVU YA HOJA' ILA WATOVU WAKUBWA WA NIDHAMU KWA 'HOJA ZA NGUVU'; hata kama hoja za aina hiyo zinashilishwa mbunge mwenye umri mkubwa kuliko Mrehemu mpendwawetu Mzee Abdalla Fundikira, mwenye usomi zaidi ya Maprofesa Sarungi, Mwakyusa au Mwandosya, au mwenye cheo kikubwa cnini kama Mhe Rostam Aziz - kinachoheshimiwa ni nguvu ya hoja tu!!

Je mnaonaje bungeni tukazingatia zaidi heshima, adabu na unyenyeke mkubwa kwa NGUVU ZA HOJA PEKE YAKE (kwa maslahi ya wale waliotutuma bungeni kuwatetea) kama wajumbe rasmi bungeni, halafu baadaye sana tu kukaanza kuzingatia heshima, adabu na unyenyekevu mkubwa kwa umri wa mtu, elimu yake au cheo pindi tukishatoka nje ya bunge??

Hili ni muhimu sana na lazima liwe hivyo mheshimiwa spika kwa sabu ilikuondoa hatari ya waheshimiwa wabunge kubaguana kiumri, kiusomi, na au ki-vyeo kule mjengoni, ni bora tutambue ya kwamba wangiapo ndani ya bunge la ni kazi moja tu - UWAKILISHI WA WATU WAKE WITHOUT FEAR OF FAVOUR - hivyo dira yake kuu ya kutolea heshima, adabu na unyenyekevu ni NGUVU YA HOJA TUU, ili ubunge wake kama li-taasisi linalotegemewa na wengi sana nje ya bunge liweze kufanya kazi bila vikwazo vingi. Hapo ndipo taasisi za Uwaziri Mkuu na Ubunge wa Jimbo la Arusha au nyingine yoyote itaweza kufanya kazi kwa umurua wake stahiki.

Lakini pindi Ndugu Godbless Lema au Mr Sugu, Halima Mdee au David Kafulila anapokutana Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda aka 'Mtoto wa Mkulima' mwenzangu na mimi hapa basi hapo yale yoote heshima, adabu na unyenyekevu ZIWE MBEEELE KAMA TAI kama ilivyo ada katika jamii yetu ya ki-Tanzania, wazee kutambulika kwa kuwa wametuzaa, kisomo huingatiwa kwakuwa hutuwezesha vizuri zaidi kumudu mazingira yetu tunamoishi na vyeo vithaminiwe hasa wenye dhamana hizo wanapovitumia vizuri zaidi na kwa haki kwetu sote.

Mwisho, heshima, adabu na unyenyekevu zote kwa pamoja ni tamu sana ilioje kwa wanaozipata kila leo na hasa pale ambapo zote hupatikana kwa hiari zaidi!!!
 
..CCM watamwadhibu tu.

..Makinda hawezi kukubali kwamba Waziri Mkuu amelidanganya bunge.

..mimi nashauri Lema awasilishe ushahidi wake mbele ya waandishi wa habari na television.

..baada ya hapo ndiyo aende bungeni na kutoa ushahidi wake. lakini ategemee kuwa ushahidi huo utapuuzwa na wabunge wa CCM.

Nadhani, ni vema kuwasilisha ushahidi bungeni kwanza. Ukiona hujatendewa haki, ndipo uitishe waandishi wa habari, inakuwa na logic, siyo kinyume chake.
 
Lema anaweza kuwapiga chini CCM vibaya sana kwa kauli moja tu, kuwa atawakilisha ushahidi wake pindi kesi iliyopo mahakamani itakapoalizika kwani sheria iko wazi due to separation of power between legislative, judiciary and exective, suala lililo mahakamani inakuwaje speaker aliruhusu kujidiliwa bungeni? huu si ni uvunjaji wa sheria?

DOWANS wamesema haiwezi kujadiliwa bungeni kwa sababu swala lipo mahakamani je hili la arusha halipo mahakamani? attack them with their own weapon, tuwaone watatoka vipi zaidi ya speaker kuonekana ni incompetent, biased and with a lot of double standard

I like this observation. The moment this statement will be presented, is the very moment that madam speaker will start to feel the heat inside the house. it's going to be very interesting today.
 
Colleagues,

Sasa naamini kabisa kuwa ni mkakatit wa serikali kukaa kimya na kwa makusudi kabisa juu ya mauji ya Arusha.

Mtakumbuka kuwa wasemaji wa mwanzo kabisa wa serikali walikili kuwa haikuwa haki kwa jeshi la polisi kutumia nguvu hiyo na hata kusababisha mauaji. Rejea matamshi ya mwanzo kabisa ya Waziri wa Mambo ya ndani kwa vyombo vya habari na jinsi alivyosikitishwa na mauaji hayo na kuhaidi kuchukua hatua. Lakini pia kumbuka Tamko la Waziri wa Mambo nje (Membe) mara baada Rais kukutana na Mabozi.

Nilishangaa kuona Membe anakana matamshi yake mwenyewe na baadae anatishia kushitaki Gazeti la Mwananchi (hata sijui tishio hilo liliishia wapi). Na pindi tu nikaona TBC ikitoa mlolongo wa yaliyotuakia Arusha kwa upotoshaji wa umma likiwemo hata tamko la Membe kwa sababu TBC haikuonesha alichosema Membe bali sehemu nyingine ya picha ya matukio hayo.

Ninachokiona nikuwa serikali sasa imehamua kabisa liwalo na liwe Juu ya yaliyojiri Arusha bila kuwaambia ukweli wa Tanzania. Sitashangaa kuona hata hilo la Lema an Pinda linaisha bila hatua zozote kuchuliwa hata kama kuna unshaidi tosha.

Angalizo: Wabunge wa CDM muwe makini na kila mara yanayosemwa muwe na ushaidi nayo. Natoa angalizo hilo kwa sababu Spika atatafuta kila njia kuhakikisha kuwa wabunge hao wanaingizwa ktk 'impossible angles' kama ushaidi wa CDM's failure.
 
Back
Top Bottom