Ushahidi wa LEMA dhidi ya Waziri Mkuu huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi wa LEMA dhidi ya Waziri Mkuu huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eliesikia, Feb 12, 2011.

 1. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Katika hali inayoonekana ni aibu kubwa atakayokumbana nao waziri Pinda basi kwa kipindi hiki ni kipute kikubwa.. Ni sawa na timu ya mpira inapopangiwa mechi na Barcelona..Ni lazima uingiwe kiwewe..
  Katika pitapita yangu hapa mjini katika kuhangaika angalau nipate mlo nilibahatika kukutana na watu mbalimbali ambao walidai Anna Makinda hiyo tar 14-feb-2011 atamwingiza waziri katika hali mbaya saana maana ushahidi wa Lema ni mkubwa na una nguvu ya kisheria..Mi nadhani huu ni wakati muafaka kushuhudia Pinda akiangua kilio bungeni kama alivyofanya alipobanwa na upinzani kuhusu kuruhusu watu wawaue wanaoua Albino.
  Ushahidi wa Lema uko hivi:

  1. Lema atamwambia waziri mkuu ni muongo kwa kusema CCM ina madiwa 16 na CDM 14 kwa kuwa diwani wa Sombetini Bwn Mawazo sio CCM tena ni CDM na Sombetini ward leader is vacant position. Kwa hiyo Pinda ni muongo kusema CCM wako 16 wakati akijua fika wako 14 maana Chatanda nae si diwani wa Arusha bali wa Tanga mjini.

  2. Kusema CDM ndo waliosababisha wananchi kuuliwa huo ni uongo kwa kuwa hapa aliombwa kutoa tamko kuhusu hao walioua na si CDM kushiriki maandamano. Kimsingi waziri Pinda alipindisha ukweli na kutuhumu safu ya CDM kwa mauaji wakati Polisi ndo waliopiga risasi wananchi. Kwa hili alidanganya UMMA kwa kushindwa kumtaja muuaji halisi wa wananchi.

  3. Kusema CDM hawakupewa kibali huo ni uongo kwa kuwa walipewa kibali na wakawafanya CDM waingie gharama zao kutayarisha maandamo kabla ya siku ya mwisho ambayo "taarifa za kiintelejensia" zilipochakachua... Hapa CCM walilenga kuitia hasara CDM kwa kuwa walijua fika kuwa ni gharama kubwa kulipa watu watayarishe maandamano kwa matangazo, ulinzi binafsi, nguvukazi, usumbufu na mengine mengi. Lakini CDM waliwaahidi kuwa kama walivyoamua watafanya maandamano na wao wangekuwa responsible endapo vurugu na uharibifu ungetokea..{imethibitika kipindi cha msiba nako walilazimika kuwaahidi polisi kuwa hakuna fujo wakati wa kuaga wale maiti wahanga}.. Kweli amani ilitwala mpaka uani na maliwatoni kote si ndani wala nje kila mtu na huzuni lakini bila fujo.
  NOTE: Si kweli kusema CDM walidhamiria kufanya vurugu ndo maana walipigwa na polisi kama waziri anavyodai.

  4. Kimsingi waziri alidanganya bunge kwa kuamua kumlaumu Mbowe kuwa angeweza kuzuia maandanamo wakati ukweli wananchi walikuja wenyewe pale Mount Meru Hotel bila kuitwa na mtu.. Waliamua kuongozana kwa amani na kiongozi wao.


  MYTAKE:
  Waziri mkuu asikubali kutumika kama chambo la kisiasa... Maana CDM walimsitiri wakati wa uchaguzi ili apite lakini anakuwa tambara bovu litakalobidi kufuliwa siku ya uchaguzi 2015... Hakuna kutoa ruhusa huyu jamaa apite bila kupingwa!!

  Waziri Mkuu ameanza kusikia haya madai ya msingi najua watasema ameghafilika pale bungeni lakini kiukweli si kulidanganya UMMA tuu bali pia ameongea uongo mkubwa kabisa tena wenye hulka ya kishabiki...
  ADHABU YAKE::
  CDM wamzomeee tuu pale bungeni wakati akikata kauli zake za uongo!!
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Siamini kama taarifa ya Lema itawekwa hadharani. Kitakachofanyika ni kwamba Makinda atatangaza kwamba ataikabidhi kwa kamati husika kwa hatua zaidi, na kutoka hapo itakuwa ikipigwa kalenda mpaka mambo yapoe.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumwache Makinda ajiwekee kamba shingoni na hakuna mtu kumsaidia...mwachieni, hivi ndivyo mipango ya Chadema inatakiwa iende. Tutataka Makinda mwenyewe ndio aanze kuuliza ushahidi wa kila kitu Waziri na ofisi ya raisi akileta majibu kwa bunge. This is good and I love it.
   
 4. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ccm Wameisha
   
 5. V

  Vancomycin Senior Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hata kama speaker akichukua ushahidi na kukaa nao ndo inaleta picha mbaya zaidi kwani watu wengi mpaka sasa wanajua pinda ni muongo
   
 6. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele eliesikia lakini hoja yako ya pili na ya nne hazitaweza kumsaidia Lema bungeni. Kwani kuna tofauti kati ya kusababisha na kuua. Kweli polisi waliua lakini kusema nani alisababisha inategemea nani unamwuliza. Na ni kweli Mbowe kama mwenyekiti wa chama alikuwa na nguvu za kuweza kuzuia maandamano. Lakini hakuona sababu kwa kuwa maandamano yalikuwa halali.

  Kisheria Maandamano yanasitishwa kwa barua sio kwa matangazo kwenye vyombo vya habari. OCD wa Arusha mjini hakuandika hiyo barua ya kusitisha maandamano. Hata hivyo Polisi walikuwepo maandamano yakianza na walikuwa na uwezo wa kuyazuia kabla hayajaanza lakini wakaamua kutofanya hivyo. Waliyasindikiza kwa takriban kilomita mbili na walipoona taarifa zao za kiintelejensia zinaumbuka kwani maandamano ni ya amani wakaamu kufanya kweli . Hivi polisi akiona mtu anataka kuua anasubiri mpaka aue ndio amkamate amshtaki kwa murder case au anamkamata kuepusha shari na kumshtaki kwa kosa la kukusudia kuua?

  Pinda amesema uwongo kwa kusema akidi ilitimia. Unahitaji mbili ya tatu akidi itimie kuweza kupiga kura kumchagua meya. Sasa kama madiwani wote wa Chadema hawakuwepo hiyo mbili ya tatu wanaitoa wapi? Barua ya kuwataarifu madiwani wa Chadema kuwa kuna kikao ilipelekwa usiku kwenye baa ya diwani Mallah na mhudumu akakabidhiwa na kuambiwa akimwona diwani yeyote wa Chadema akiingia kwenye hiyo baa basi amkabidhi hilo kabrasha. Mhudumu alikaa nazo siku mbili na kuaj kuwakabidhi baada ya vurugu kuisha tokea na Lema kupigwa na polisi. Ofisi za Chadema zinajulikana ziko wapi kwanini hawakupeleka huko ofisini?

  Pinda anasema uwongo kwamba maandamano yalisimamishwa kwa kuwa walitumia zaidi ya njia moja. Maandamano yalikuwa kwenye njia moja tu. Tena walifuata njia iliyoshauriwa na polisi. Ushahidi wa kideo ukionyesha viongozi wote wapo kwenye andamano moja upo.

  Pinda amedanganywa amebakia kusema uwongo. Makamba alitoa maagizo kwa mkurugenzi achakachue meya awe wa ccm. Mkurugenzi katika kutekeleza akatumia ubabe mwingi akachemsha, kulinda kibarua chake amedaganya wakubwa wake. Polisi nao wame overreact wamepiga risasi ovyo wameua watu wasio na hatia. Wanasema uwongo kuficha ukweli. Tunasikitisha. Watu tunaowapa dhamana ya kutuongoza hawawezi kuwa responsible for their actions. Kila pahali ni kufunika kombe mwanaharamu apite. Hata rais mwenyewe anatudanganya anasimama na kusema hawajui dowans wakati ndio waliomfadhila kuingia ikulu. Nae spika anahamaki eti waziri mkuu hawezi kulidangaya bunge, mara hii ameshamsahau Lowassa? Ushahidi wa ukweli uliotokea Arusha Lema atauweka hadharani lakini watazidanganya nafsi zao na kusema ni uongo, halafu watamwadhibu. Hata hivyo mwisho wa siku wananchi wenye nguvu ya umma wanaona na wanajua yupi ni mwongo na yupi ni mkweli. Wammwangalie Mubarak alijidangaya kwamba atatawala milele nguvu ya umma ikakataa sasa yuko wapi?
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama walivyosema wengine ndivyo itakavyokuwa. Kwamba Makinda atapokea ripoti na kuitunza kabatini na game limeisha. Watu hawa hawana adabu.
   
 8. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Count down..........................siku ya 34.............................siku za mwizi 40.

  CCM hawana chao tena kwa wananchi watabaki kuiba tu, hawaaminiki.
   
 9. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lema anaweza kuwapiga chini CCM vibaya sana kwa kauli moja tu, kuwa atawakilisha ushahidi wake pindi kesi iliyopo mahakamani itakapoalizika kwani sheria iko wazi due to separation of power between legislative, judiciary and exective, suala lililo mahakamani inakuwaje speaker aliruhusu kujidiliwa bungeni? huu si ni uvunjaji wa sheria?

  DOWANS wamesema haiwezi kujadiliwa bungeni kwa sababu swala lipo mahakamani je hili la arusha halipo mahakamani? attack them with their own weapon, tuwaone watatoka vipi zaidi ya speaker kuonekana ni incompetent, biased and with a lot of double standard
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..CCM watamwadhibu tu.

  ..Makinda hawezi kukubali kwamba Waziri Mkuu amelidanganya bunge.

  ..mimi nashauri Lema awasilishe ushahidi wake mbele ya waandishi wa habari na television.

  ..baada ya hapo ndiyo aende bungeni na kutoa ushahidi wake. lakini ategemee kuwa ushahidi huo utapuuzwa na wabunge wa CCM.
   
 11. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani hasira ya wananchi inazidi kupandishwa 100%.Jinsi viongozi wakuu wasivyotaka kuwaambia ukweli.Wananchi wapo kimyaa sio wajingaa bali wanafuatilia kila jambo linavyo kwenda,mwisho wa yote watapata jibu na hatma yake itafika.Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.Waziri kipenzi cha watu Mh.PINDA ndiyo huyoo anang'atuka kwa wananchi na kutekwa na mafisadi unadhani thamani ipo tenaa? Haya wee
   
 12. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Pia pinda alisema waliouliwa walikuwa 50 meter from police post wakati waliuliwa zaidi ya mita 500
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Sioni la ajabu lolote atakalo leta lema zaidi ya kulipamba "tamko la cdm kuhusu mauaji ya arusha"
  zaidi ya yote lema ataleta kisha makinda atatangaza umeletwa na unapelekwa kamati husika kwa hatua zaidi, kwisha maneno.
  Kilichotokea pale si kikubwa kama tunavyo dhania
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Alisema akisha wakishawasilisha ataongea na wandishi wa habari.....
   
 15. n

  nchasi JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Nasikitika sana, ufedhuli unaotaka kutokea juu ya mbunge hodari anayetetea maslahi yetu. PINDA si mtoto wa mkulima tena bali ni mtetezi wa mafisadi, anatumwa na kutoa taarifa amboyo imechakachuliwa. Wanazidi kuwafumbua macho watanzania ili wajue kuwa wao siku zote ni wapinga haki lakini waangalie ya MISRI NA TUNISIA yanakaribia Tz maana hasira zetu kwa sasa hakuna wa kuzituliza.
   
 16. s

  simanjiro Member

  #16
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  paulss, hapa kuna jambo kubwa.

  kwa kuzingatia misingi ya haki pande mbili zinapowasilisha arguments zake mbele ya muamuzi ni kwamba muamuzi ni lazima ajiridhishe kuhusu ukweli wa arguments hizo kabla hajatoa maamuzi.

  sasa basi kwa msingi huo, ninachokiona hapa ni kwamba kwa kuwa Mh pinda tayari amewasilisha hoja zake, na sasa Mh lema atawasilisha hoja zake ni jukumu la Makinda kujiridhisha kuwa hoja za pinda zilikuwa za ukweli na lema ni muongo. katika kufanya hivyo mimi naona Spika atalazimika aidha kuunda Tume ya Bunge au kulitaka bunge litoe azimio la kuitaka serikali kuunda tume huru ya majaji kuchunguza swala hilo.

  kwa hiyo jambo kubwa lililopo hapo ni kwamba CCM imejifunga goli la kisigino, Makinda alikosea kureact kwa kumtaka Lema athibitishe hilo swala.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  that is where i always question your analytical skills

  never underestimate CDM bwana pweza
   
 18. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  wasipomuadhibu lema hata kama wataficha ushahidi watakuwa wamethibitisha wenyewe kuwa pinda alisema uongo.
   
 19. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Huyu mama ni kilaza hamna mfano
   
 20. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mnategemea nini kutoka kwa viongozi Pinda na Makinda ni wabunge batili kwa mujibu wa katiba ya nchi hii inayotumika!!!!!!!!!!!!!!!!! Sana sana ni kutumia mbinu za kigaidi kulinda maslahi ya waajiri wao ambao ni mafisadi??????????? Nchi imekwisha- kuwaza ya Tunisia na Misri katika mazingira ya Tz ni ndoto!!!!!!! Tunisia na Misri kujitoa muhanga ni order of the day-hapa Tz kila mmoja anaogopa kuleta ukombozi kwa kuhofia kukanyaga miili ya waliokufa!?!!!!!!!!!!!?????????????Pole TZ!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...