Ushahidi wa jinsi udini ulivyo kithiri ndani ya chadema!!

Status
Not open for further replies.

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,818
Wana-JF!

Inaposemekana kuwa CHADEMA ni chama cha kikanda na kidini, sio kwamba maneno hayo yanatoka kwa hisia tu,lah hasha, bali ni mfumo uliopo huko CHADEMA katika utoaji wa fursa za uongozi ndio wenye ubaguzi wa dini na ukanda.

Mfumo uliopo CHADEMA sio ule wa usawa katika kutoa nafasi za watu kugombea, ni mfumo wenye kuangalia mambo fulani fulani ambayo kwenye jamii yetu ya kitanzania hayana umuhimu, lakini ndani ya CHADEMA upewa kipaumbele!

Leo sitakuwa na mengi sana, ila nimeweka vielelezo kwenye huu uzi, ili basi nyinyi wenyewe mjionee hali halisi ilivyo huko CHADEMA katika usawa wa utoaji fursa, yaani bila kuangalia dini ya mtu, ukabila ama ukanda wa alikotoka mtu.

Vielelezo vyenyewe ni majina ya wabunge wetu wa CHADEMA (wale wa majimboni na viti maalumu), wanaJF ni wakati sasa wa kujua ukweli kuhusu chama kinacho endesha mambo kwa minajili ya kidini, kikabila na kikanda kwa vithibitisho.

Wabunge wa majimbo ni hawa wafuatao;

Freeman Mbowe, John Mnyika, Halima James Mdee, Highness Kiwia, Ezekia Wenje, mchungaji Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi, Vicent Nyerere, John Shibuda, mchungaji Israel Natse, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Said Arfi, Philemon Ndesambulo, Joshua Nassari, Prof. Kulikoyela Kahigi.

Wabunge wa viti maalumu ni hawa wafuatao;

Lucy Owenya, Esther Matiko, Mhonga Luhanywa, Anna Mallac, Paulina Gekul, Conchesta Rwalumulaza. Wengine ni Suzan Kiwanga, Grace Kiwelu, Suzan Lyimo, Christowaja Mtinda, Anna Komu, Joyce Mukya, Leticia Mageni Nyerere, Naomi Kaihula, Chiku Abwao, Rose Kamili, Christina Lissu, Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano, Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga.

Hitimisho,

Kwa uchambuzi makini na yakinifu wa hiyo orodha, utagundua kuwa kuna ubaguzi mkubwa wa utoaji wa fursa kwa waislamu ukilinganisha na fursa walizopata wakristo. Hivyo basi, katika hali kama hii ya karibu 90% ya wabunge ni wakristo na 10% tu ndio waislamu,CHADEMA inaponyooshewa kidole kuwa ni chama cha kidini isikatae na kubisha.
 
umeongea ukweli mkuu sema wa tz hatupendi kuambiwa ukweli ila kama chadema wakiweka sawa hz changamoto za udini na ukabila kitakua tumaini jipya la wa tz
 
Wana JF,

tunawasikia wengine wakisema kwamba CDM ni chama chenye udini sanaaaaaaaa, kwahivo wamekileble kuwa ni chama cha kidini

sio waislamu tu, au wakiristo tu wanaolalamikia hayo ni watu wengi na hilo wanalihisi linaweza kuleta tz mpya kabisa ikiwa CDM itaweza kupenya kwenye tundu ya sindano na kushika madara katika 2015 on wards
 
Ni ukweli wa wazi kabisa, CDM ni Chama Cha maaskofu, mapadri na makasisi. Asilimia 93 ya viongozi wote wa CDM ni wakristo, na wengi wao ni viongozi wa dini
 
Wana JF,

tunawasikia wengine wakisema kwamba CDM ni chama chenye udini sanaaaaaaaa, kwahivo wamekileble kuwa ni chama cha kidini

sio waislamu tu, au wakiristo tu wanaolalamikia hayo ni watu wengi na hilo wanalihisi linaweza kuleta tz mpya kabisa ikiwa CDM itaweza kupenya kwenye tundu ya sindano na kushika madara katika 2015 on wards

Avatar yako ni dawa za kulevya hoja yako ina mwelekeo huo huo hongera.
 
Hiyo ni propaganda ya ccm,huku chadema tupo waislam kibao."kalagabakho".
 
Wana JF,

tunawasikia wengine wakisema kwamba CDM ni chama chenye udini sanaaaaaaaa, kwahivo wamekileble kuwa ni chama cha kidini

sio waislamu tu, au wakiristo tu wanaolalamikia hayo ni watu wengi na hilo wanalihisi linaweza kuleta tz mpya kabisa ikiwa CDM itaweza kupenya kwenye tundu ya sindano na kushika madara katika 2015 on wards

Una kilalu?
 
Nenda LUMUMBA ukalambe chako.
 
Walevi wameshaanza kutusumbua na mada zao zisizo na mashiko!
 
Wana jamvi!

Haya mambo ya kubebana iwe kwa namna ya undugu, ukanda, udini ama mahusiano ya kindoa, kiuhalisia uwa haya kwepeki hasa kwenye shughuli zetu wanaadamu.

Nimekuwa nikisia lawama kwa CCM kuwa ni chama cha wenyewe, ikiwa na maana kwamba kama huna mtu ambae tayari ni kigogo, basi wewe huna chako.

Mtazamo huu umekuwa ukienezwa sana na viongozi na mashabiki wa CHADEMA, kwa upande mmoja ni kweli lakini sio mara wote kuwa mpaka uwe na mtu wako ndio uwezd kupata fursa ndani ya CCM.

Ila kwa muda sasa nilidhani wenda ni CCM tu ndio yenye ukiritimba huu, lakini nilipo fanya tafiti, nikagundua kuwa ni suala la kawaida, kwani hata CHADEMA kuna mambo haya ya kubebana kwa namna kama nilivyo orodhesha kwenye aya no. 1.

NANI KAMBEBA NANI CHADEMA?

WanaJF, katika mchakato wa kutoa viti maalumu CHADEMA, ndugu Tundu Liss ambae ni mbunge wa Singida mashariki, alipiga debe kuhakikisha dada yake anapata viti maalumu ambae ni CHRISTINA LISSU, ambae sasa ni mbunge viti maalumu Singida.

Dr Slaa amembeba Josephine Mashumbusi ambae ni mkewe, kwanza kwenye kupata ajira lakini pili kwenye mchakato wa kumpendekeza agombee jimbo la Kawe. Kwa wale msio fahamu, kuna mkakati una endelea wa kumuengua mwanadada machachali Halima Mdee ili asigombee Kawe na nafasi hiyo apewe Josephine. Nadhani wote tunajua kuwa Josephine ndiye mchumba wa Dr Slaa.

Mzee Mtei na Mbowe, hapa kuna mahusiano ya muda mrefu tu, kwani baada ya mzee Mtei na wazee wenzake kuona wao wamechoka, wakaamua kumkabidhi Mbowe chama hicho ingawa kiuhalisia Mbowe hana mvuto wa kisiasa, ila Mzee Mtei hakuwa na budi kumpa kwa sababu ni mkwe wake.

Kuna wengi tu walio bebwa mpaka huko BAVICHA ila nadhani kwa hawa mtakuwa mmepata picha kuwa hali hii ya kubebana sio tu CCD, bali ni kote.

Hivyo basi, propaganda hii ya kubebana naona haina mashiko na niwaonye mashabiki wa CHADEMA na viongozi wenu kuacha kuitumia dhidi ya CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom