Poluyakhtov
JF-Expert Member
- May 9, 2017
- 365
- 306
Habari wana JF,
Ngoja nisonge kwenye mada, kwa kipindi cha miezi ya hivi karibuni nilikumbwa na changamoto iliyohitaji fedha ya haraka. Basi katika pita pita zangu nikaangukia kwenye kampuni za mkopo mtandaoni ambazo ni PesaX pro na Zimacash. Nilikopa na kulipa kwa wakati.
Baada ya hapo nikaanza kupokea sms kutoka namba tofauti tofauti zikinisihi niombe mkopo kupitia app zao. Nilishangaa na nilipojaribu kuuliza namba yangu wameipata wapi?, jibu nililopewa ni kwamba kampuni ya mikopo ni moja isipokuwa wanatumia application tofauti.
Na nilipomwambia mtumaji wa sms kwamba ni kosa kunitumia jumbe za aina hiyo pasi na makubaliano ya kimkataba akawa anajibu kipuuzi. Niwafanyaje ili wapate somo la kutokumlazimisha mtu kukopa.Au nichukue pesa halafu nisiwalipe?