Usawa katika Maoni /Majadiliano Kwenye Mitandao Jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usawa katika Maoni /Majadiliano Kwenye Mitandao Jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Apr 21, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mpenzi wa Mitandao jamii na mtumiaji wa Dhati kabisa hapa Tanzania nimejiunga karibu mitandao yote ya jamii kwa kipindi cha miaka 7 iliyopita pia ni mwanachama wa mitandao mingine jamii ya afrika haswa Magharibi ,Mashariki na Nchi za Ulaya .


  Mitandao jamii imeleta mapinduzi makubwa katika ufanyakazi wa kawaida wa kampuni , serikali na watu binafsi kwa njia ya mtandao haswa katika mahusiano ya jamii hizo na kampuni zao , serikali na wananchi wake, mashirika mbalimbali na Taasisi .


  Lakini kwa siku za karibuni toka kuanza kwa mwaka huu tumeona nchi kadhaa duniani ambapo watu wametumia mitandao jamii katika kuwasiliana na kuandaa maandamano na kuondoa serikali madarakani lakini nchini Nigeria na Pakistan mitandao jamii imewahi kushutumiwa kufadhili mawasiliano kati ya magaidi haswa wale wanaotafuta watoto na wengi wa kuwafunza .


  Hali hiyo inaoyoendelea sehemu mbalimbali duniani sio ya kupuuza wala kuangalia kwa jicho moja , hii ni changamoto mpya kwa serikali , kampuni na mashirika ya kijasusi duniani haswa nchi ambazo hazijakuwa sana kimaendeleo ya teknologia kama Tanzania .


  Wiki hii tumeona malumbano kidogo kati ya Mwanachama wa Mtandao mmoja wa kijamii na Chama Tawala cha Tanzania ambapo chama hicho kimeelezea kusikitishwa na Mtandao huo wa Kijamii kutumika ndivyo sivyo hata kutuhumu kwamba kuna chama kimoja cha upinzani kinafadhili Mtandao huo .


  Kabla ya tukio hili kumekuwa na lile la Uwekaji wa Nyaraka za malipo kwenye mtandao huo toka shilika moja la umma nchini PPF , inasemekana aliyeweka Taarifa hizo hakuweza kuzitetea pindi alipokuwa anaulizwa maswali na mengine muhimu .


  Lililodhahiri ni kwamba Mitandao jamii mingi duniani haswa Majukwaa ya majadiliano inakuwa kutokana na kupata ushirikiano wa Karibu kutoka kwa watu wanaopiga mwelekeo wa vitu Fulani watu hao huamua kuweka mambo hayo kwenye mitandao kama ilivyo WIKILEAKS .


  Lakini ukweli mkuu ni kwamba mitandao mingi ya kijamii haswa majukwaa inaruhusu watu kutumia majina bandia na vile vile kuleta haki isiyo sawa haswa kwa watuhumiwa wa mambo kadhaa wa kadha .


  Kama nilivyosema hapo juu mtu ameweka Nyaraka za Maliyo ya PPF lakini pale anapoulizwa maswali anakimbia hajibu ni sawa na wikileaks wahusika wanapotaka kujua zaidi kuhusu nyaraka hizo hawapati lolote zaidi ya kupewa kile wikileaks wanachotaka walimwengu wapate .
  Tatizo langu sio kushambulia mitandao hiyo wala nini tatizo langu ni pale kunapokuwa hakuna usawa kwenye mitandao hii haswa kwa upande wa pili kushiriki mijadala hiyo bila kutukanwa au kushambuliwa binafsi kutumia majina hayo hayo bandia .


  Ushauri wangu kwa watu wote wanaotumia mitandao hii ni kujua kwamba Nchi yetu bado changa sana kwenye masuala ya Teknologia za mawasiliano tutumie uchanga huu kuwajibika kwa uwazi na uhuru zaidi kuliko wakati ambapo nchi itakuwa imebobea na bado kukawa na kasumba kama hizi za kuficha majina , kuleta nyaraka za siri , kushambulia upande mmoja na mambo mengine mengi .


  Suala langu la mwisho ni kuwaonya watu kutokuiga mambo yanayoendelea maeneo mengine ya dunia na kujifananisha na wao kwa mfano wengi wamekuwa wakijivunia mitandao hii ya jamii katika kuleta mapinduzi na aina nyingine ya uwajibikaji wakati vijijini kwao hata umeme hakuna lakini anataka kutumia mtandao jamii kufanya mabadiliko .


  Jamani hata tunavyoangalia kwenye luninga zetu au ma intaneti Waasi la Libya wanavyopambana na Serikali yao tumeona shimo hata moja kwenye barabara ? au kusikia mgao wa umeme kwenye nchi hizo ? wao walipotumia mitandao jamii vitu vyote hivyo vilikuwepo hawakuwa na shida nyingi kama sisi .


  Ndugu zangu , jamaa zangu na watu wangu wengine adui wako wa maendeleo ni wewe mwenyewe , jiangalie kwenye Kioo kitoe makosa yako kwanini kuleti maendeleo katika nchi yako na jamii yako sehemu zote wanazoandamana na kutaka mabadiliko walishajiletea maendeleo makubwa .


  Tusitake kufikia ilipo uchina sasa hivi ambapo wanachuja taarifa zote zinazoingia nchini humo kwa njia ya mtandao pamoja na jinsi watu wanavyotafuta vitu kwenye mitandao tutafute habari ya jinsi google ilivyofanyiwa uchina miaka michache iliyopita .


  Kuna nchi ya Iran ambayo ilipambana na mitandao jamii haswa Twitter kipindi cha maandamano baada ya uchaguzi wake na kufanikiwa kuyazima lakini mpaka sasa hivi mitandao hiyo jamii ndani ya nchi ya Iran imekuwa kama Laana .


  Kwahiyo Ndugu zangu watanzania wenzangu tuaje porojo tujenge nchi yetu kwa fursa tulizonazo sasa , mengine tunaweza kuyaacha zaidi kwenye majukwaa ya kisiasa kwa maana siasa haina adui wa milele , lakini wewe raia wa kawaida unahitaji mitandao jamii zaidi kwa ajili ya maendeleo yako .


  Huu uhuru tulionao sasa hivi wa kuwasiliana na kubadilishana mawazo tusiupoteze kwa vitu kama hivi .


  Wakati Serikali na wadau wa Teknohama wanajiandaa na kuwa na Sheria Mtandao ( CYBERLAWS ) kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi na miongozo kwa wafanyabiashara na watu wengine katika mitandao ni vizuri mifano hii isitumike kukandamiza baadhi ya watu na kunyanyua wengine lakini ni Wenye mitandao wenyewe ndio wakuamua kama wanataka kubanwa au la .


  YONA MARO
  0786 806028
   
 2. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe acha unafiki. Mbona mtandao wako wa Wanabidii hufuati hizo taratibu na badala yake unaendesha kama mali binafsi kwa kuwatoa wale wanaopingana na fikra zako? Au na wewe unatafuta millioni 200 kama walizovuta JamiiForums kutoka Tanzania Media Funds?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nilitegemea ndugu upongeze ujasiri wa hawa watu wachache, ndani ya Teknolojia changa kwa kuweza kuthubutu kuelimisha jamii kwa kiasi kikubwa namna hii!...Umetoa mfano mmoja tu wa PPF kuwa ulikuwa na mapungufu, lakini taarifa nyingine nyingi zinakuwa na vyanzo wazi kabisa na vinavyoeleweka....tusipende kutafuniwa sana kila kitu, wakati mwingine tutumie muda kushirikiana na waleta taarifa katika kufanya utafiti wa kina wa habari tunazoletewa!
  Habari ya kutumia majina bandia isionekane tatizo ili mradi kama taarifa zitakuwa ni sahihi na zenye maslahi kwa taifa...
  Hivi kwa mfano bwana Anonymous akipiga simu kuwa jengo fulani mtaani linaungua, na akakata simu na kuondoka, je taarifa hizohazitasaidia kuwa'alert watu wa Zimamoto?..Jina si muhimu kiasi hicho, japokuwa kuna wakati yapasa tuwe wawazi!  Napingana na wewe hapa kwa engo fulani juu ya hoja yako ya hapo juu!
  Tuna uwezo kabisa kuiga kwa wengine na kuyafanyia kazi kwa kutumia context yetu ya huku Bongo!...
  Ni kweli Teknolojia huku kwetu haijasambaa sana, lakini fikiria wakati wa kampeni za uchaguzi, ambapo wakubwa wa vyama fulani wanatumia mitandao ya simu ambazo zimeenea hadi vijijini, kuwaomba kura na kuwalisha uwongo na ukweli ili mradi tu kuwadanganya na kuwaahidi mashati na kofia.
  Hivyo kwa huku kwetu si lazima tutumie kompyuta, tunaweza hata kutumia simu kueleweshana mambo ya kufanya na hatua za kuziofuata!
  Lakini pia tunaweza kupashana habari baada ya wachache kuzisoma kwenye kompyuta, na hatimaye asilimia kubwa wakajua!
  Ndiyo maana juzi mitandao fulani ya jamii ikalaumiwa na vyama fulani kwa kusababisha wananchi kupata uelewa wa mambo fulani waliyokuwa hawayajui, na matokeo yake wakapiga kura according to elimu mpya waliyoipata kwa kompyuta(mitandao).
  Kwahiyo nakuhakikishia kuwa tunaweza kucustomize kiasi kidogo cha teknoloji tuliyo nayo kwenye mitandao , na ikawafaa watanzania wote na wakafanya mabadiliko!
  Nawasilisha!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanzania (then Tanganyika) ilipita uhuru sawa na Malaysia, but look where Malaysia is today! Hapa kwetu tunaonekana kuendelea zaidi kwenye fani ya UKUPE. Kila siku utasikia taifa letu ni changa, mara uwezo wetu ni mdogo, ili mradi ni udogo-uchanga -udogo-uchanga kila kukicha.

  Na huu USAWA katika kutoa maoni unao-asa watu ni USAWA wa aina gani hasa. What to do you consider to be usawa? zidumu fikra za mwenyekiti? or daily subscription to Uhuru newspaper?

  Hivi kwa nini tunaogopa fikra mbadala? All the government needs to do ni kuchukilia hii mitendao kama chanzo kimojawapo cha hisia na mawazo ya wananchi kuhusu utendaji wake. Nidhamu ya uoga itatumaliza.
   
 5. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Mkuu huna hoja,maana swala la uhuru wa kutoa maoni sio hisani ya awaye yote,ni haki ya msingi ya kila binadamu,natambua kuwa uhuru una mipaka,lakini pia natambua mipaka yoyote lazima iwe ya pande zote mbili
  kuiga kwa wenzetu kama wanafanya vizuri hakuna tatizo,twawezaiga then kuboresha
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,196
  Trophy Points: 280
  This is a thinly disguised, shamelessly hypocritical, mindlessly meandering frontal attack on freedom of expression and the time honored, Publius certified traditions of more anonimity for the people and transparency for the nitwit bigwigs.

  Usifikiri meanders zinaficha nia rasmi iliyojikita katika post yako. Control.
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,582
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Dogo unamatatizo, Kawaambie walio kutuma kuwa UMEGONGA MWAMBA!
   
Loading...