Usanii sadifu wa Mrisho Mpoto uundiwe tuzo au mtaala wa fasihi.

Massanda OMtima Massanda

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
1,056
561
Ndugu wagenzi wa fasihi, kama mlikuwa miongoni mwa waliotazama mazishi ya Marehemu Mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru, bila shaka Msanii mahiri wa ugani / tambo, Mrisho Mpoto aligusa nyoyo za waombolezaji na watazamaji wa mazishi yale kwa maneno mazito ya kizalendo na yenye hamasa kwa umoja na mshikamano wetu!
Binafsi nilingiwa na fikra tatu ambazo nadhani kama zitafanyiwa kazi zinaweza zikawa na matokeo chanya:
1. Fikra za uafrika na mshikamano wa waafrika (Africanism / Africanness / PanaAfrican panorama) ni muhimu kuziendeleza;
2. Kuna umuhimu wa sanaa aina hii ya akina Mpoto kuundiwa tuzo ya kitaifa au kibara (Afrika) ili kushindanisha na kuhamasisha uzalendo;
3. Sanaa za aina hii ziwekwe kwenye mitaala ya fasihi ili kuandaa kizazi chenye uzalendo wa dhati.
Tutafakari!
 
Back
Top Bottom