Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,695
- 49,945
Wakati mwingine nikisoma maandiko mbali mbali huwa najiuliza ule usanifu wa Lugha waliokuwa nao mababu zetu na wale manju waliosifika zamani umekwenda wapi? Hata nyimbo zinazotungwa siku hizi zina ukakasi sana wa lugha kiasi kwamba inahitji uvumilivu kuzisikiliza. Tatizo letu ni nini hasa, tuna upungufu wa misamiati ya Lugha ya Kiswahili au weledi wetu katika kusanifu lugha ni mdogo?
Wakati mwingine, Ashakum si matusi, huwa najiuliza hivi hawa vijana wa siku hizi wanapotongoza huwa wanatumia maneno ya aina gani? au ndiyo mambo ya "Inakuwaje?" au "vipi baadaye una nafasi?". Ukimsikiliza bi Shakila kwenye ule wimbo wa "Kifo cha mahaba" au "Macho yanacheka, moyo unalia" unapata starehe ya fikra kiasi kwamba ni mwenza mwenye moyo mgumu tu asiyeweza kuguswa na nyimbo hizo. Zama hizi kimetokea nini?
Sasa soma vitabu, hadithi za kwenye magazeti, au uandishi wa kawaida kabisa ndiyo balaa. Kuna jama yangu ni mhadhiri kwenye chuo fulani cha umma,ameniambia ukiwapa vijana wa siku hizi Karatasi wakuandike historia za maisha yao wenyewe, kisha uwaambie zifikie kurasa tano, basi kama ni Mwalimu au Mhadhiri utanuniwa Mwezi mzima. Hata historia za maisha yao hawana maneno ya kuzielezea!?
Kwa nini uwezo wetu wa kusanifu Lugha umepotea?
Preta wewe ni wa kizazi hiki hebu tusaidie!!