Kwani hao mwaka wa tatu hawana wadogo au ndugu zao wanaosoma/watakaosoma UDOM baadae? Kama kweli kuna madai ya msingi yanapaswa kuungwa mkono na wanafunzi wote bila kujali ni mwaka wa kwanza au finalist. Wanapaswa kufahamu kwamba hizo stahili wanazopata ikiwa ni pamoja na sh. 5000 za boom zilipiganiwa na watu wengine miaka ya nyuma lakini wao leo wananufaika. Hivyo nawasihi wanafunzi hao wa mwaka wa tatu wasiwe na ubinafsi..