Waliotimuliwa Udom waibuka, watoa ya moyoni

Feni05

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
290
250
IN SUMMARY

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.
Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.
“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.
“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.
“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.
Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.
“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.
Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,540
2,000
Serikali ya magu ukisikia imelitumbukiza basi (taifa) mtaroni usishangae abiria (mwananchi) maana kasi yake imezidi kiwango na bahati mbaya kabisa yeye anajua kukanyaga wese tu hali hajui nature ya barabara anamopita wala anakoenda.
Abiria tuombe msaada wa trafiki gari likapumzike kituoni au afungiwe speed governor
 

strong ruler

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
4,815
2,000
Walio ichagua tena ccm kuendelea kuongoza tanzania tena na tena wana la kujibu mbele za Mwenyezi Mungu.
 

medisonmuta

JF-Expert Member
Oct 10, 2014
1,277
1,500
Lakini hiyo kozi ya walimu wa masomo ya sayansi iliwekwa maalum kwa waliopata daraja la 1&2 tu katika kipindi cha JK. Imekuaje wamebeba hovyo wanafunzi wasio na sifa.
 

King Ngwaba

JF-Expert Member
May 15, 2016
15,955
2,000
Hili la Udom Nahisi JPM na NdaliC wameingia Choo Cha Kike na mwisho Watatumia Bendera Yao Ya Kijani Kutunyamazisha Kwa Mabavu.
 

kibila

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
532
250
Kwenye ili Mkuu wa nchi na waziri wamechemka sana swala hapa lilikua ni kuwalipa walimu wao wanafukuza wanachuo hii ni hatari magu lazima awe anafanya uchunguzi kabla ya kuchukua hatua sio kukurupuka tu akienda ivi ataihatubu inchi hii
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,059
2,000
Ukiona ngoma inavuma sana bhasi i karibu kupasukaaa...

Kweli wahenga hawakukosea
 

ismailyy

Senior Member
Jul 26, 2014
123
195
Lakini hiyo kozi ya walimu wa masomo ya sayansi iliwekwa maalum kwa waliopata daraja la 1&2 tu katika kipindi cha JK. Imekuaje wamebeba hovyo wanafunzi wasio na sifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom