Usalama wa Taifa haujadiliwi

Usalama wa Taifa haujadiliwi

Mleta mada mbona unaogopa ??

Ulivyo hitimisha kwa miandishi mikubwa ndiyo nimeelewa kuwa u muoga.

Kama unataka kujadili UwT hebu weka jina na mawasiliano yako,

Kwa maana hapo umeleta taarifa ya mtu mwingine humu JF.

Asante.
 
Kabla ya kujadili usalama wa taifa ni muhimu kujua maana ya taifa.
Wengi hawajui taifa ni kitu gani na wakati mwingine hawawezi kutofautisha usalama wa viongozi na ule wa taifa.
Hata hivyo, vyote vina uhusiano wa karibu. Taifa ni zaidi ya viongozi.
 
Hawa watu wanafanya Kazi ngumu kuhakikisha mambo yanaenda sawa miaka yote hiyo,Leo hii tusiichafue taasisi kwa mambo yanaotendwa na watu wachache ambayo yanaweza kuwa sio maagizo ya kiofisi Bali tu utumiaji mmbaya wa jina LA ofisi.Kiongozi mpya ameingia ofisini tumpeni muda tumwache afanye Kazi zake za kiusalama,sisi tuendeleeni na [HASHTAG]#siasa[/HASHTAG] zetu za nyuma ya keyboard.
 
Thadei Ole Mushi
April 11 at 6:19pm
TISS NI TAASISI NYETI SANA KWA TAIFA HILI.

Na Thadei Ole Mushi.

Idara ya Usalama wa Taifa haujadiliwi hadharani. Ni taasisi nyeti sana kwa mustakabali wa Nchi. Hata Bajeti yake huwa haijadiliwi hadharani.

Taasisi hii kwa hapa nchini mwetu imejizolea sifa nyingi sana kutokana na uimara wake. Kwangu binafsi naona si sahihi sana kuijadili hadharani kwa kufanya hivyo ni kukiuka mila na Desturi za taasisi hii.

MY TAKE: - UMUHIMU WA KITU HAUKIFANYI KITU KUWA JUU YA SHERIA KATIBA AMA HAKI ZA RAIA HURU NCHINI AKIWA NDANI YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE KISHERIA NA KIKATIBA PASI NA KUDHURU USALAMA WA NCHI NA RAIA.

KITENDO CHA KUNYANYASA RAIA HAKITAFUMBIWA MACHO MAANA NI RAIA WANAIPA UMUHIMA TAASISI HIYO KUWA YA KIPEKEE PALE TU INAPOJIHESHIMU KUHESHIMU RAIA NA HAKI ZAO KAMA WANANCHI NA KUDHIBITI VITENDO VYENYE KUHATARISHA DEMOKRASIA, AMANI, NA USALAMA WA NCHI.
Tusiishi kwa mazoea. Tunaona magwiji wa vyombo vya intelijensia wakijadili ya kwao na kukosoa wanapokosea. Kwa nini wa kwetu tusiwajadili! Hii ya kutojadiliwa inavifanya vyombo vyetu kutenda watakavyo na wakati mwingine kukosa changamoto zitakazowafanya watende vizuri zaidi. Tukiendelea kuwaangalia wakitenda haya mabo ya kuteka (kama ni wao) na hakuna wa kuwakemea hadharani tutafika walikofika Argentina na nchi zingine za Amerika Kusini. Watawala mara nyingi ufurahia vitendo hivi maana vinatendwa kwa kisingizion cha kuwalinda na kulinda utawala wao.
 
Na ukiona watu wanaanza kujadili taasisi hii maana yake watu yamewafika shingoni, wajiangalie wamejikwaa wapi! Bashite anawaponza! Usalama wa mwenye vyeti fake hauakisi usalama wa taifa letu Bali unaashiria kuangamia kwa Taifa letu!
Ni hapo tu honestly!
 
Thadei Ole Mushi
April 11 at 6:19pm
TISS NI TAASISI NYETI SANA KWA TAIFA HILI.

Na Thadei Ole Mushi.

Idara ya Usalama wa Taifa haujadiliwi hadharani. Ni taasisi nyeti sana kwa mustakabali wa Nchi. Hata Bajeti yake huwa haijadiliwi hadharani.

Taasisi hii kwa hapa nchini mwetu imejizolea sifa nyingi sana kutokana na uimara wake. Kwangu binafsi naona si sahihi sana kuijadili hadharani kwa kufanya hivyo ni kukiuka mila na Desturi za taasisi hii.

MY TAKE: - UMUHIMU WA KITU HAUKIFANYI KITU KUWA JUU YA SHERIA KATIBA AMA HAKI ZA RAIA HURU NCHINI AKIWA NDANI YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE KISHERIA NA KIKATIBA PASI NA KUDHURU USALAMA WA NCHI NA RAIA.

KITENDO CHA KUNYANYASA RAIA HAKITAFUMBIWA MACHO MAANA NI RAIA WANAIPA UMUHIMA TAASISI HIYO KUWA YA KIPEKEE PALE TU INAPOJIHESHIMU KUHESHIMU RAIA NA HAKI ZAO KAMA WANANCHI NA KUDHIBITI VITENDO VYENYE KUHATARISHA DEMOKRASIA, AMANI, NA USALAMA WA NCHI.
Hawazeeki,hawafi,hawaumwi,hawana stress,Walijiweka wenyewe kwenye Taasisi hiyo,Hawakosei,nk 'TUSIWE NA MAWAZO MGANDO'
 
Walioko kwenye taasisi hii tunayoigharimia kwa kodi zetu, fanyeni mjadala wa kina na wa dhati na wenye afya kwa nini mmefikia hapo ambapo watu wameanza kuhoji utendaji wenu!
 
Kwa mwendo huu wa kuhusishwa na Utekaji wa Raia LAZIMA TISS WAJADILIWE.
 
Taasisi hii kwa hapa nchini mwetu imejizolea sifa nyingi sana kutokana na uimara wake.
Uimara wake unaujuaje wakati tasisi yenyewe haijadiliwi na kama haijadiliwi Ina maana kuwa hata utendaji wake haupimwi kwa kuwa utendaji wake ni wa gizani kama utendaji wa shetani.
 
Mleta mada yuko sahihi mia ya mia. Huwezi jadili usalama wa taifa jf wala facebook wala twita.

...Nini hasa maana ya usalama wa Taifa? huyu anayeitwa Taifa ni nani hasa? ni kundi la viongozi fulani/wateule? ni watanzani hawa hawa ambao wanalalamika kutekwa, kuteswa etc?? Ni nini hasa defination ya usalama wa Taifa??? Tunamaanisha nini hasa tumaposema ''Taifa'' liwe salama?? Je hawa wanaofanya kazi usalama wa taifa ni binadamu au ni malaika? Kama ni binadamu hawafanyi makosa? hawana makundi? upendeleo? hawashawishiwi kwa namna yoyote ile? Kama wanafanya makosa ya kibinadamu ni chombo gani hasa kinatakiwa kuwaweka kwenye mstari????
 
Mleta mada yuko sahihi mia ya mia. Huwezi jadili usalama wa taifa jf wala facebook wala twita.
Na mimi naungana na mleta hoja.Na.nyie usalama wa Taifa lazima mtambue watanzania wanabadilika kutokana na kasi ya dunia.Sasa TISS lazima mje na mbinu mbadala za kuweza kufanya.kazi katika dunia ya leo.Mbinu zenu hazitakiwi kufahamika kwa wasiohusika.Sasa hivi tukio linaonekana kabisa "haaa hawa ni TISS".Hiki ni kitu hatari.Mlikuwa vizuri miaka yote.Kama kuna baadhi wanatoa siri za taasisi nje,waondoeni mara.moja.
 
Mshaanza kuropoka tena... Acha kazi ifanyike, mtoto wako akikunyea haukati mkono wako, kosa la mtu moja usihitimishe kwa wote, watu hawalali kwa ajili yako unapata mda wa kupost hata Usiku kwa Uhuru kama huo..heshimu wanaojitoa maisha kulinda nchi yako.
UKIFANYA JEMA KWANINI USISIFIKE??....HUWA WASAHILI HUSEMA SAMAKI MOJA....??.....HAPO HAINA MAANA WOTE WALIKOSEA ILA KWA MMOJA IMEKUWA ISHU!!....KUNA WATU HAWALALI USIKU NA MCHANA KUTAFUTA PESA KUISIMAMISHA USALAMA WA NCHI HII KUFANYA KAZI. TUNATEGEMEANA AS HUMAN BEINGS ALL CREATURES OF GOD!..AND IN FACT .... NANI KAMZIDI MUNGU KUSIMAMIA USALAMA WA HII NCHI KWA WATU WAKE WANAOTESWA BILA HAKI NA HAO SAMAKI WALIOOZA?
 
Kna wapumbav wachache ni zero kbs,mtu unaakaa bila waswas,unaenda job bla waswas..unalala murua tna hku unagegeda bla waswas wakat Tiss 24/7 wapo busy...kujadil hii sekta jaman ooh..naishia apa..kusaka sfa za mitandaoni kutawaponza watu..wale sio polc o sungus..wale n spies,,over!!!
 
Ukiwa mtumwa wa wanasiasa kamwe hautoweza kuchanganua mambo....

Utageuzwa geuzwa km mpunbavu kila baada ya siku...

Leo kaongea bashe... we umelidaka bila hata uchunguzi unalikuza.... hii ndio tanzania.. kesho ataongea zito utalidaka utalitukuza... unasubir na lissu aongee lake... km kawaida utaruka nalo....

Ila haujui kaongea vile kwa nin wala kwa manufaa ya nani....
We bendera tu unafata upepo km mke wa pili..

Embu acha kushikiwa akili na watu wachache kwa itikadi zao binafsi.....

Kuwa mwepesi kusikiliza kila kitu... vichambue vifanyie utafiti ubaki na cream ya habar kamili...

Mtoto wa kiume unasubir bashe aongeee baada ya kutekwa roma then na we unadakia.


TISS sio shirika la nyumba.... TISS sio media hawako kwa ajil ya publicity.
TISS sio genge au forum km jamii...


TISS ni idara nyeeti inayofanya mambo yake kwa weled wa hali ya juu.... pasipo mim na weww ambao ni watu wa kawaida kutambua kinachoendelea....
 
Back
Top Bottom