Usalama wa Taifa haujadiliwi

Usalama wa Taifa haujadiliwi

UKIFANYA JEMA KWANINI USISIFIKE??....HUWA WASAHILI HUSEMA SAMAKI MOJA....??.....HAPO HAINA MAANA WOTE WALIKOSEA ILA KWA MMOJA IMEKUWA ISHU!!....KUNA WATU HAWALALI USIKU NA MCHANA KUTAFUTA PESA KUISIMAMISHA USALAMA WA NCHI HII KUFANYA KAZI. TUNATEGEMEANA AS HUMAN BEINGS ALL CREATURES OF GOD!..AND IN FACT .... NANI KAMZIDI MUNGU KUSIMAMIA USALAMA WA HII NCHI KWA WATU WAKE WANAOTESWA BILA HAKI NA HAO SAMAKI WALIOOZA?
Bado hapo hamna la kujadili kabisa , Wanaokengeka hushuhhulikiwa kitaasisi sio lazima Mimi na wewe ujulishwe ili ufurahi.
Usimhusishe Mungu katika hili kwa kuwa mamlaka zipo na zinakibali machoni pake na hata kipindi cha Musa majeshi na ulinzi ulikuwepo... Tulizeni akili mambo haya hushughulikiwa kitaasisi na sio kwa post na matamko za kukufurahisha wewe na kikundi chako.
 
Mshaanza kuropoka tena... Acha kazi ifanyike, mtoto wako akikunyea haukati mkono wako, kosa la mtu moja usihitimishe kwa wote, watu hawalali kwa ajili yako unapata mda wa kupost hata Usiku kwa Uhuru kama huo..heshimu wanaojitoa maisha kulinda nchi yako.
BAWACHA Mnatukana POLISI, JWTZ, USALAMA, UHAMIAJI, JKT hivi kama mkipata nchi ( Mungu epushia mbali ) mtafanya kazi na nani ?
 
Walioko kwenye taasisi hii tunayoigharimia kwa kodi zetu, fanyeni mjadala wa kina na wa dhati na wenye afya kwa nini mmefikia hapo ambapo watu wameanza kuhoji utendaji wenu!
That is good thinking 'they should not take us for granted'
 
Umuhimu wa usalama wa taifa wao hawadiliwi wala hawaguswi sababu ya umhimu wao lakini hebu niulize kidogo umuhimu wao na wsnajeshi na Police kwani wote hawa ni wanausalama wa taifa hili mwa mm nijuavyo usalama wa taifa anafanya kazi kama taifa lina amani na vyombo vinavyoleta amani nchini jeshi na police kama jeshi halitakuwepo hawawezi kufanya kazi kwani kazi zao ni zakificho kwa maana ingine ni walinzi wa watawala na kama majukumu yao yakiwa magumu lazima walete taarifa upande wa police au jeshi kulingana na ukubwa wa inshu yenyewa mambo madogo wstayamaliza wenyewe!
 
Idara ya taifa imepoteza sifa baada ya kuanza kutumiwa na Chama tawala kwa ajili ya kuratibu ushindi wa Chama hicho kwa kutumia njia chafu na ndio haohao wapika majungu wanaoitwa kutokana na taarifa za kintelenjensia hiki kisifanyike na ndio wanaosababisha mauaji yatokee kwa raia kutokana na vyombo vya dola kutumia nguvu kulazimisha jambo fulani ambalo lilikuwa limeruhusiwa kufanyika lisitishwe.

Kwa kifupi ni idara ambayo inafanya kazi kimbeyambeya inawachonganisha raia na serekali iliyopo madarakani,inawachonganisha wapinzani na serekali,na inawachonganisha raia na vyombo vya dola,inakoleza moto Kati ya raia na vyombo vya dola,wakati huo moto unapokolea baada ya kukolezwa na wao vyombe vingine vya dola ndivyo vinavyobaki kuhangaika na moto huo, wakati wao wanakuwa wamejichimbia ndani ya mahandaki yao kutokana na aina ya kazi yao.
 
Kama ikithibika usalama wa taifa wanashiriki kutesa raia basi hakuna execuse yoyote!Wamewekwa kwa kulinda maslahi ya nchi na watu wake,kama wanakiuka jukumu lao basi hamna namna,lazima wajadiliwe!Subiri ndugu zako au wewe binafsi ukutwe na hayo ndio uje hapa useme hayo unayosema!
Kama wanatumia mwanya wa kutojadiliwa kufanya uhuni,wacha tuwaseme!Hata hili uliloongea ni sehemu tu ya kuwajadili!
Thadei Ole Mushi
April 11 at 6:19pm
TISS NI TAASISI NYETI SANA KWA TAIFA HILI.

Na Thadei Ole Mushi.

Idara ya Usalama wa Taifa haujadiliwi hadharani. Ni taasisi nyeti sana kwa mustakabali wa Nchi. Hata Bajeti yake huwa haijadiliwi hadharani.

Taasisi hii kwa hapa nchini mwetu imejizolea sifa nyingi sana kutokana na uimara wake. Kwangu binafsi naona si sahihi sana kuijadili hadharani kwa kufanya hivyo ni kukiuka mila na Desturi za taasisi hii.

MY TAKE: - UMUHIMU WA KITU HAUKIFANYI KITU KUWA JUU YA SHERIA KATIBA AMA HAKI ZA RAIA HURU NCHINI AKIWA NDANI YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE KISHERIA NA KIKATIBA PASI NA KUDHURU USALAMA WA NCHI NA RAIA.

KITENDO CHA KUNYANYASA RAIA HAKITAFUMBIWA MACHO MAANA NI RAIA WANAIPA UMUHIMA TAASISI HIYO KUWA YA KIPEKEE PALE TU INAPOJIHESHIMU KUHESHIMU RAIA NA HAKI ZAO KAMA WANANCHI NA KUDHIBITI VITENDO VYENYE KUHATARISHA DEMOKRASIA, AMANI, NA USALAMA WA NCHI.
 
Mshaanza kuropoka tena... Acha kazi ifanyike, mtoto wako akikunyea haukati mkono wako, kosa la mtu moja usihitimishe kwa wote, watu hawalali kwa ajili yako unapata mda wa kupost hata Usiku kwa Uhuru kama huo..heshimu wanaojitoa maisha kulinda nchi yako.
Una uhakika gani kwamba hawalali
 
Ndio ivyo tena TISS wamejidhalilisha mpaka wanajadiliwa kila mahali.
Wanajidhalilisha au ndio wanapata promo ya nguvu. Kipi walichofanya wakasemwa wameshindwa? Wabunge watovu wa nidhamu na viashiria vya uhalifu wanachapwa na kulia kama matondola. Haya ni mafanikio na kutoa somo kuwa hakuna anayeogopwa na hawa wazee wa kazi.
 
Usalama wa bashite..yaani hawa usalama bashite akigombana na demu wake wanabeba AK-47 saa tano kwenda kumtisha demu wa bashite yaani ni maajabu
 
Acheni kutufanya vilaza skuizi kuna internet.CIA na FBI pamoja na unyeti na nguvu zao lakini bado wamejadiliwa na kuchunguzwa seuze TISS,as long as mishahara na matumizi yao yanatokana na kodi zetu lazima wajadiliwe,tena wazi bila kificho,wao sio cult ama secret society,lazima wawe scrutinised.
cb402241e9f90affc6d6547931f3a680.jpg
 
Napata shida kubwa sana ya kutafakari haya yanayoendelea kwa sasa.
TISS naafiki wana weledi wa kazi zao wanazozifanya kila siku, ila inawezekana ndani yake wapo Maofis ambao licha ya kula viapo wanatumika kufanya zaidi ya kile wanachoruhisiwa kufanya , na hicho wanachokifanya si kwa maslahi mapana ya Nchi bali ni kwa maslahi ya wachache, hivyo ni ruksa kujadiliwa.
 
TATIZO lililopo ni TISS ya siku hizi imejikita katika mambo ya kisiasa badala ya usalama wa taifa.Pia wanafanya mambo bila intelijensia kabisa kias kwamba ata zuzu atajua ni wao ndio wamehusika.

Swali.Nani ana mamlaka zaidi katika Tiss kati ya Mwigulu na Bashite?
 
Ivi wakuu Kati ya Jeshi la ulinzi na taasisi ya usalama wa Taifa ,, kipi ni bora zaid katika nchi yoyote,,,,,me naona kama Jeshi la ulinzi wa mipaka na nchi ndio taasisi nyeti zaid ,,,maana ndani yake si pia wana vitengo vya ujasusi au, halafu wao sio WaPo kwajili ya wananchi wote ,,,me binafsi naona Jeshi ndio huwa ni taasisi ambayo yakupewa heshima mno,,,,maana wanakesha kuhakikisha nchi na mipaka ipo safe

Tafiti dunia nzima, afu utagundua stability ya Nchi inatokana na Idara ya Usalama wa Taifa ya Nchi husika. Pia vyombo vyote vina umuhimu yaani Intelligence Organization pamoja na Jeshi. Labda nigusie kidogo tu, Kila chombo kina majukumu yake, Mfano Jeshi kazi yake ni ulinzi wa mipaka ya Nchi, lakini wakati wa amani lina majukumu yake pia na ndio maana unaona Jeshi halihusiani na raia mara kwa mara kama ilivyo usalama wa raia(Polisi) ndio maana ni vigumu kwa Jeshi kulaumiwa kwa kuwa hali-deal na raia moja kwa moja kama ilivyo TISS na Polisi. Idara ya Usalama wa Taifa ni chombo muhimu kwa ustawi wa Taifa, labda niseme hivi, Idara ya Usalama wa Taifa yoyote ile ni Serikali ndani ya Serikali, kwa maana hii katika Ofisi nyingi kuna maafisa Usalama wamepenyezwa huko, mfano Jeshini, Wizara mbalimbali, BOT kuna maafisa Usalama(Rejea-Mkurugenzi wa sasa wa TISS alikuwa BOT hapo zamani na baadae NIDA) n.k, kwa hiyo kila ofisi ya Serikali au Private Organization kubwa utawakuta Maafisa Usalama wa Taifa wapenyezwa huko japo huwezi kuwajua kwa kuwa ni kama staff wa hapo au wanakuwahata mabosi wa sehemu hizo. Sababu ya kupepenyezwa huko ni kuhakikisha Nchi inakuwa salama. Kwa sababu mfano ktk Oranization kibwa za kimataifa Nchi za kigeni hupenyeza majasusi wao kama walivyo Peace Corps wa USA so ni jukumu la maafisa Usalama walio katika Sehemu hizo kuwabaini na kuwazuia kwa sababu wao wamefundishwa kuwatambua. Bahati mbaya sana wengi hawaoni mazuio yanayofanywa na Idara hii maana hawatangazi kuwa wamefanikiwa kuzima jaribio hili na lile kama ilivyo Jeshi la Polisi linapokamata majambazi, ndio maana Idara hiyo huwezi kuona umuhimu wake moja kwa moja.
Pia Idara ya Usalama inafanya kazi na vyombo vingine likiwemo Jeshi, kwa msingi huu, Idara ya Usalama wa Taifa wapo hadi Nje ya Nchi, wanapopata taarifa ya Nchi kutaka kuvamiwa, taarifa hizo zitawasishwa Nchini na Jeshi litajulishwa na kujiweka tayari. Ni mengi sana ya kuandika,ila nihitimishe kwa kusema vyombo vyote hivi ni muhimu kwa kila kimoja na majukumu yake kwa ustawi wa Nchi.
 
Katika nchi ambayo Twiga amepanda ndege kabla ya watanzania wengi, na mtuhumiwa mkuu akafanikiwa kutoroka-lazima Usalama wa Taifa uhojiwe. Katika nchi ambayo kwa miaka 10 mfululizo makampuni ya madini hayalipi kodi yoyote kwa kisingizio cha kutopata faida, usalama wa taifa unatulazimisha kujiuliza maswali.

Usalama wa Taifa ambao kazi yao kuu ni kupambana na wapinzani kana kwamba waharibifu wa tunu zetu kitaifa wako upinzani tu, lazima wahojiwe. Usalama wa taifa unaohusishwa au kuhisiwa kutesa watu wanaopaza sauti juu ya dhuluma mbali mbali ambayo ni haki yao kikatiba, hauwezi kupewa heshima ya kukaliwa kimya. Usalama wa taifa ambao mfumo wake wa kutoa ajira ni wa kutia shaka, kwamba mtoto wa maskini asiye kwenye system(mfano watoto wa viongozi wa chama na serikali wilaya, mkoa na taifa) hawezi kupata fursa ya kuitumikia, lazima wahojiwe-japo mioyoni mwetu kama hatuwezi kuhoji hadharan.

Kuhoji usalama wa taifa haina maana hatuthamini jitihada kubwa sana zilizofanywa wakati wa harakati za kukombozi. Wengine ambao tulikuwa wadogo tuliweza kutambua mfumo imara wa usalama na kupashana habari kuhusu matukio yenye kutia shaka juu ya usalama wetu. Katu hatukuwahi kuwahisia mabaya watu wa taasisi hii. Natambua siasa zetu zimebadilika, bado taasisi yetu inalazimika kutambua kuwa mtu hawi adui kwa kupenda upinzani tu au kwa kuhoji serikali ili mradi anafanya kwa hivyo kwa staha kwa viongozi.

Tunaoipenda idara hii, tungependa inajikita ktk ujasusi wa uchumi. Kwa ukanda wetu, nchi kama Kenya na Rwanda ni tishio kiuchumi, japo vilevile waweza kuwa washirika wazuri. Ningependa kuona longterm strategy za kudeal nao. Pia, kuna wakati taasisi hii imewavumilia sana viongozi wa dini wachochezi kana kwamba inawatuma. Kwa nchi yetu, dini ni most divisive issue-isichezewe kwa maslahi ya kisiasa.
 
Kwa mwendo huu wa kuhusishwa na Utekaji wa Raia LAZIMA TISS WAJADILIWE.
Sijui mtu akishutumiwa kutenda kosa e.g. muuza madawa na kuitwa kuhojiwa ni kosa la wanausalama?. Mtu KUKAMATWA kwa tuhuma, hili nalo ni KUTEKWA?.

Swali lingine, je kama Demokrasia na amani inavunja usalama wa nchi na kuangamiza taifa tufanyaje kuokoa Nchi?. Ni kweli Dar sio salama kwa mafisadi na wauza unga. Fahamu tu kuwa TZ inafahamika Duniani kwa maunga. Serikali hii itawaudhi sana wauza unga na mafisadi.
 
Back
Top Bottom