Usalama wa bidhaa hii unatia mashaka

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Nimejaribu kuchunguza tube nyingi za dawa ya meno inayoitwa Whitedent za ujazo mbalimbali nimegundua kuna tatizo kubwa la kuonyesha muda sahihi wa bidhaa hiyo kuendelea kuwepo sokoni na kufaa kwa matumizi(expiry date) nilichogundua ni kwamba ni vigumu kuona usahihi katika hilo na ninaamini kinachofanyika ni makusudi; kwasababu, maandishi mengine yote yanasomeka isipokuwa hiyo expiry date huwezi kufanikiwa kuiona
Kimsingi expiry date ya bidhaa inatakiwa iandikwe mahali ambapo mtu anaweza kusoma kwa urahisi;

Cha ajabu tangu nianze kuziona hizi dawa sokoni hadi hivi leo sijawahi kufanikiwa kupata kwa urahisi hilo angalizo.

Na kosa kubwa linalofanyika ni kwamba inagongwa chini ya tube yenyewe ambapo haionekani vizuri na huwezi kutambua tarakimu zilizoandikwa hapo.

Halafu na tbs mamlaka iliyopewa dhamana ya kuangalia ubora wa bidhaa hapa nchini imebariki bidhaa kama hii tutumie hata bila kujua expiry date!
 
Kwa kweli ni bora kuacha kununua dawa isiyoonyesha expiry date. Yamkini ya kupata madhara ni kubwa kwa kutumia madawa yaliyoexpire.
 
Back
Top Bottom