Usajili wa simu afrika mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usajili wa simu afrika mashariki

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Sep 27, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Suala la Usajili wa Simu Afrika Mashariki  Mkurugenzi wa tume ya mawasiliano Tanzania kasema wako katika mchakato na tume nyingine za mawasiliano katika nchi za afrika mashariki ili kuwezesha simu zote zinazotumika ndani ya eneo hili zisajiliwe pamoja na line zake kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa mataifa hayo – kwamba hilo suala liwe ni lazima kwa kila raia na kampuni ndani ya jumuiya hii ili kuweza kupambana na vitendo vya wizi wa simu .


  Kweli napongeza sana suala la usajili wa Simu za viganjani na aina nyingine ya simu zinazotumika katika maisha yetu ya kila siku naamini pia sheria hii ikikamilika basi hata huduma zingine za matumizi ya simu na mawasiliano kwa ujumla yatashuka zaidi pamoja na kuboresha huduma za mawasiliano haswa vijijini ambapo kumeonekana na shida za mawasiliano na mawasiliano kati ya mtandao mmoja wa simu na mwingine kupunguzwa ndani ya nchi husika na katika jumuiya .


  Pili ni kutoa elimu zaidi kwa watumiaji mbalimbali wa huduma za mawasiliano haswa simu za mikono ambazo wengi wanatumia kwa kupiga kupokea na kutumia kwenye shuguli zingine za biashara kama kununua bidhaa au kushusha vitu Fulani kwa njia ya mtandao hii ni kwa sababu kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu masuala ya mawasiliano kwa watumiaji wengi haswa kwenye masuala ya uhalifu kwa njia ya mtandao na mengine mengi ambayo watu hutokea kuamini mara moja .


  Mfano kwa siku za karibuni kumetokea ule uwongo wa mtu kufa pindi anapopokea ujumbe Fulani wa simu au akiona rangi Fulani huu uzushi umesambaa sana na kuna watu wanaendelea kuamini hivi sasa tume ya mawasiliano ilitakiwa kuhakikisha wananchi hao wanafikiwa na kuambiwa ukweli pamoja na kutoa namba za bure za watu kupiga endapo wanapata tena ujumbe unaofanana na huo siku nyingine .


  Tatu ni kuangalia suala la wafanyabiashara wanaouza na kuagiza simu na vifaa vyake kutoka nchi za nje mfano nchini india wamepiga marufuku kabisa uingizwaji wa aina Fulani za simu ambazo ni bandia haswa toka nchini CHINA kitu kama hichi kingeweza kufanyika hata hapa kwetu au jumuiya nzima ya afrika mashariki watu wengi wameathirika na bidhaa hizi bandia hili suala ni la kushugulikiwa mapema .


  Pamoja na hiyo kumekuwa na ongezeko kubwa la simu za kisasa ambazo zimeibiwa maeneo mengine duniani na kuja kutumika hapa Tanzania baada ya kuzifanyia ujanja ujanja Fulani nyingi zinatoka afrika kusini hili ni suala ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi haraka sana kuna simu nyingi sana za aina hiyo zinapitishwa viwanja vya ndege na sehemu nyingine za mipakani .


  Nne ni suala la haki za wananchi mbalimbali ambao wametumika kwenye shuguli mbalimbali za mawasiliano kuanzia wale wasanii ambao nyimbo zao zinapigwa na kuingizwa kwenye simu kupitia njia ya mtandao wa simu wasanii wengi wamekuwa wanalalamika kuhusu kutokutendewa haki na baadhi ya kampuni katika masuala ya malipo na kulindwa kwa haki zao .


  Mwisho ni kuomba wafanyabiashara katika sekta ya mawasiliano wananchi na wadau wengine kushirikiana na Tume ya mawasiliano Tanzania katika kufanikisha shuguli mbalimbali pamoja na miradi kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku .


  Tusikate tamaa eti ule mradi ni wa serikali wewe haukuhusu , uhujumu kwa kuiba vifaa au kukaa kimya pindi unapoharibika au kuleta hitilafu wanaoadhirika ni wananchi wenzako na taifa lako kwa ujumla .


  Jumuiya ya Afrika Mashariki ni yetu  Kuilinda , kuitetea na kuiendelea ni wajibu wetu wote .
  YONA F MARO
  www.ictpub.blogspot.com
   
Loading...