Mwanariadha huyo mweney umri wa miaka 30, ataaga riadha wakati anastaafu mwezi Agosti baada ya mashindano ya World Championships mjini London baada ya kuanza kuwaaga mashabiki wakae huko Kingston Jamaica.
Mshindi huyo mara nane ya medali ya dhahabu aliashinda kirahisi mbio za mita 100.
Bolt alikimbia kwa kasi ya sekunde 10.03 mbele ya mashabiki 30,000 waliocheza densi na kupeperusa bendera huku fataki zikirushwa.
Mshikilizi huyo wa rekodi ya mita 100 na 200 alibusu uwanja baada ya kumaliza mbio hizo.
Waziri mkuu wa Jamaica Andrew Holness na rais wa chama cha kimataifa cha riadha Sebastian Coe pia walihudhuria.
"Ni vyema kuona kuwa kila mtu alikuja, hii inaonyesha kuwa nilichokifanya kwenye spoti ni kikubwa," alisema Bolt
Bolt ameshinda mbio za mita 100, 200 na na dhahabu ya 4x100 katika mashindano matatu ya olimpiki yakiwemo Beijing 2008, London 2012 na Rio 2016.
Chanzo: BBC swahili