Usahihi: Rais hajasema lijengwalo ndio bomba refu zaidi duniani

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,181
2,944
Habari waungwana,

Kuna hoja kubwa imesmbaa kuhusu Rais 'kuchemsha' wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa bomba la mafuta kwa kulitaja kuwa likikamilika litakuwa bomba refu zaidi duniani kitu ambacho hakukisema na naomba nimnukuu alichosema.

"Hapatakuwa na bomba refu la aina hii, lenye jumla ya kilometa 1,445 linalosafirisha crude oil lakini crude oil yenyewe inayosafirishwa inakuwa heated...... bomba refu kwa taarifa nilizonazo liko India la kilomita 600, kwa hio hili la kilomita 1,445 litakuwa la kwanza inawezekana duniani"

Kuongezea tu
  1. Ilikuwa ngumu Rais kukosea kwa sababu kabla alitaja mabomba tuliyonayo Tanzania na mojawapo alilotaja ni TAZAMA pia akasema lina kilomita 1,710 zikiwa zimezidi tayari za bomba la Uganda.
  2. Kuna watu huwa tunasubiri serikali ikosee nasi tufanye ajenda na kutogusia kabisa ajenda kuu, utofauti wa itikadi na tambo za kisiasa usituachanishe kwenye mambo ambayo yanatufaidisha sote pamoja pia kuwakumbusha tu bomba hili halikujileta kwa sababu tayari mkataba ulishasainiwa lipite Kenya, kuna watu wakafanya juhudi lipite Tanzania ili wananchi wa nchi hii wafaidike kwa namna moja ama nyingine.
  3. Bomba halina hasara hata kama makadirio yanayosambaa mtandaoni yasipofikiwa hata robo yake. Hatulipii ujenzi wake, bomba sio madini kusema labda yanachuliwa na hayatarudi zaidi pia litaongeza mzunguko wa fedha nje ya kodi na fedha za serikali kuanzia ujenzi wake pia wakati likiwa operational.
  4. Mwisho nami nikosoe kidogo, taasisi nyeti kama ya Urais kupiga vijembe nchi jirani tena ambayo hamna mgogoro wowote 'unaoonekana' sidhani kama ni nzuri kwa afya ya ujirani wetu. Comment ndogo iliyofanywa hadharani huko nyuma ilivuruga mahusiano na taifa mojawapo jirani, Kama kuna mgogoro wa chinichini acha ubaki hukohuko au usuluhishwe ulipo(chinichini) sio kuufanya uwe 'Official'
Kwa wale wanaoamini vyombo vya habari vya nje kuthibitisha kauli ya Rais wao wa ndani, hawa hapa Reuters wakiongelea bomba letu kutoka kwa waganda=>Uganda, Tanzania sign deal for world's longest heated pipeline.

Na kwa wale wasioamini katika maandishi, nimeambatanisha video, ndani ya DK 2 za mwanzo utakuwa umesikia alichosema Rais Magufuli.

 
Back
Top Bottom