Jana jioni nikaona si vibaya na mimi nikajisogeza kunako Stesheni nijionee hali halisi na jinsi ambavyo treni yetu imeweza kw akiasi kikubwa kutatua tatizo la usafiri.
mnamo saa 1 kamili ya jioni nilikua pale stesheni.Nilionyeshwa sehemu y akununulia Tiketi nikapata moja.
baada y akuingia ndani nilikutana na Treni ya Kigoma ambayo inapaki sambamba na treni ya ubungo-stesheni.Muongozaji alitoa muongozo tusijekujichanganya.
Idadi ya watu niliyokutana nayo pale sio chini ya watu 1000. na watu wliendelea kuongezeka kadri muda ulivyokua unasogea.
Treni ilifika mnamo saa 1.30 ikiwa tayari na abiria nilipochunguza nikaambiwa walipandia kituo cha kamata.Kati ya watu 1000 waliokua stesheni ni takribani watu 400 tu waliopata nafasi.
Hali ilikua ni ya kugombania kupita kiasi na watu kujazana kwenye treni kuliko hata za India......
tuliokata tiketi ikawa imekula kwetu.Mbaya zaidi izo tiketi sio rasmi kwa maana kwamba>zinaprintiwa na mashine za selcom then wanaikata mara tatu ile printout wana ipiga mhuri.Ile tiket moja ya selcom inakatwa zaidi ya mara 3 hadi 4........sidhani kama huo utaratibu upo official,otherwise ni hujuma.
Ombi: mabehewa yaongezwe hasa muda wa jioni.....
Huu ni mwanzo mzuri
Kuongeza mabehewa si utatuzi wa mwisho ingawa unaweza kupunguza msongamano.
Wanatakiwa kuwa na mfumo wa kulipia kabla (pre-paid service) kwa njia hii hakutakuwa na Usumbufu na wasiwasi wa kupata au kukosa usafiri labda iharibike.
Njia hii inatoa uhakika wa idadi ya abiria dhidi ya uwezo wa mabehewa husika .
Kitu muhimu nikuzingatia muda wa treni kuondoka na kufika kila kituo kwa muda.