Panda Barcelona kutoka Dar to Masasi town, Lala Masasi Town maana ni mji umechangamka sana na una nyumba nyingi za kulala wageni zenye hadhi, Hotel ndogo, Motel, lodges kali na guest kibao.
Ikifika jioni ita boda akupeleke (Uwanja wa fisi) nyuma ya ilipokuwa stand ya zamani. Hapo utakula Nyama choma za kutosha na kama ni mtu wa vyombo vinapatikana pia, ukitaka vyombo vya kutosha huku showshow za maana na mziki mnene unaweza kuingia pale Kibo Pub.. hapo ni Unyama zaidi mkuu.
Asubuhi nenda stand Mpya maeneo Mwenge (tokula) utakutana na basi za uelekeo wa Songea, Mbeya. Vuta chuma yako hapo Barakah Classic au Superfeo ndizo zinafanya vizuri njia hiyo. Hizo zote zinafika hadi Mbeya.
Ukianza safari utaipata miji midogo na mikubwa kama
Mangaka-Nakapanya-Tunduru-Namtumbo-Songea-Madaba-Njombe-Makambako-Igawa-Chimala-Igurusi-Mbeya City
Uwe na safari njema.