chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,117
Fastjet! Kwa kweli Tanzania hii inahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya usafiri wa anga. Nadhani Fastjet bila kutazamwa na serikali wamejiwekea uzio wa kutokamatika kisheria.
Usiku wa April 2, 2016, saa 3:15, Mdogo wangu anasimulia, tumeruka kutoka JNIA kuelekea KIA na tulipokaribia kutua control tower wakaripoti kuwa kuna hitilafu ya umeme hivyo hatuwezi kutua kwa sababu taa za runway zimezima. Tukarudishwa JNIA..tukaambiwa ndege inajaza mafuta turudi KIA kwa sababu tatizo limekwisha.
Wakati tunashangaashangaa tukashushwa kwenye ndege na kuambiwa kuwa masaa ya crew yamekwisha hivyo tusingeweza kuruka tena. Na wanasema ndege iliyopo ni ya April 3, 2016 saa 5 asubuhi. Utawala wa FasJet ulikataa kutoa nafasi kwa ndege ya saa 12 asubuhi KIA - Jomo Kenyatta Airport ambayo inaweza kubeba abiri wote tulioshindwa kutua KIA usiku wa jana. Maamuzi yote yanafanywa London..
Fastjet kwa kujidai wao ni "low cost" airline hawatoi malazi, nauli za kurudi majumbani, chakula wala viburudisho panapotokea kuahirishwa kwa safari.
Kwa hali hii: Je FastJet t inastahili kweli kuwa kwenye category ya "low cost airlines " ? Na haiwezi kulazimishwa kutekeleza matakwa ya sheria za kitaifa na kimataifa za uendeshaji wa huduma za usafiri wa anga na wawajibike kisheria kwa mteja?
Hapa Tanzania, Fastjet inaendeshwa kama local flight hivyo kupata faida maradufu ikilinganishwa na International flights.
Kwa nini abiria wanateseka hivi?
Tunasubiri Mheshimiwa Raisi awatumbue...