Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,639
- 220,424
Rafiki yangu wa karibu sana, ameoa na wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike. Huyu bwana kwakweli ni kama kaka yangu, tunashare mengi sana. Imebidi na mkewe pia awe rafiki yangu.
Tatizo linakuja bwana ananiambia mke wake nyumbani yuko rough sana, ananieleza dada zake wakija kumtembelea wana panga nyumba, wakiondoka wifi analalamika vitu vyake havioni.
Sijawahi kufika nyumbani kwao, ananiambia inabidi apange kwanza kabla sijakwenda. Katika maongezi nilimgusia dada mwingine bila kufahamu kama ninagusa hisia zake, nilimhadithia jinsi nyumba ya Victoria ilivyo safi, alinijibu "wanawapata wapi wanawake wa aina hiyo?"
Huyu kaka, siku akipata mwanamke msafi, ninadhani ndoa itapumulia mashine.