Usafi hapa ni aje?

Usafi hapa ni aje?

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
05_10_wwms8v.jpg

Wavuvi wa samaki katika Soko la Magogoni, Dar es Salaam wakiuza kitoweo hicho kwa wachuuzi baada ya kurejea kutoka kuvua. Kwa sasa samaki wadogo ndio wanaopatikana kwa wingi sokoni hapo. (Picha na Fadhili Akida).

Unaweza kususa kununua samaki....miguu tena mpaka sehemu waliyowekwa samaki?:angry:
 
Mhh kazi ipo ila ukichunguza sana heri ya hiyo miguu kuliko huko baharini:brick:
 
Tanzania kila mtu anaendesha shughuli kivyake kwa kweli na watu wa profession mbali mbali hawatimizi wajibu wao hapo nilitegemea Maafisa wa Afya wawe wmeshafanya kazi lakini bureeeeeee kabisaaaaaaaaaa
 
kuna haja ya kubadirisha mazingira hata kwa kiasi kidogo japo pafanane na shughuliye
 
Si afadhali hapo Magogoni. Ulishafika machinjioni Vingunguti? Basi kama una kinyaa nyama utaiona kama mama mkwe wako. Na pale kuna ma bwana/bibi afya kibao.
 
kudra za mwenyezi Mungu tu zinatuponyesha ukifikiria sana na ukiona vinavyotokea unaweza kusema hauli tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom