US na EU kuwa kwenye vita ya kiuchumi na Tanzania ni Propaganda za kijinga sana

Yaani ni sawa na wewe una drive BMW X6 afu eti mwenye baskeli aina ya Swala anakulaumu wewe kwamba eti unamziba njia..yaani unamchomekea...useless!!

Marekani na Ulaya wametuacha nyuma miaka zaidi ya 500.
Kwa sababu wewe bado unalala kwenye nyumba ya nyasi au mabua na kuishia mlo moja kwa siku basi Watanzania wote wanaishi hivyo.
 
Kwanini Marekani imekuwa ikifutilia sana matokeo ya uchaguzi wa Tanzania au inaitumia kama kisingizio cha kuficha nia yake kwa Tanzania.

Jibu ni . Marekani inatumia matokeo ya uchaguzi wa Tanzania kuficha maslahi yao nchini Tanzania.

Marekani bado inajali hatima ya mradi wake wa kutatanisha wa Umeme wa Symbion kwamba Kampuni ya Ugavi wa Umeme (TANESCO) ilisitisha kandarasi yake mnamo 2016 baada ya kugundua kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikizichota pesa za walipa kodi kwa kuchaji mabilioni ya shilingi kwa siku wakati ikiipoteza TANESCO na kuharibu upatikanaji wa umeme nchini
Dawa yao ni kuwafungulia mashtaka ICC: crimes against humanity
 
Pole sana kwa kuishi katika ujinga wa kutupwa.

Hivi unajua uchumi wa China umeinuliwa na nani?

Hivi unajua kuwa katika top 20 ya nchi zenye madini mengi Duniani, kwa Afrika inaingia nchi moja 1. Hiyo nchi moja unaijua?

Kuna watu mna mahaba na ujinga. Na hakika mtabakia nao milele. Mnachokijua ni KKK - Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Maarifa hakuna, analysis zero.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeanza kusema mwaka huu wenzako tupo hapa kwa muda mrefu usione tunatoa vidonge vya uhakika.
 
Nakubariana na wewe Ila ingekuwa vizuri kwa hayo uliyosema pia ungependekeza kuwa na chama kimoja
Maana binafsi chokochoko za ya us zinatokana na namna ya uchaguzi ulivyokuwa si kutupangia kiongozi wa kuchagua
Tanzania hatuhitaji chama kimoja, tunahitaji vyama vinavyojitambua sio SACCOS ya Mlevi wa Konyagi au yule mwenye chama cha mfukoni. Watanzania msikwamishe na wezi wa kisasa wa mifukoni.
 
Kama "umma" hapa ni mabepari & mabeberu -- mfano, Bush, Obama, Blair, na Marekani & EU na washirika wao majahili, wamendea-rasilimali za wengine -- basi jibu ni NDIYO KWA HERUFI KUBWA!

Kanuni za kuongoza nchi yeyeto duniani ni mbili tu.
1.usisomeshe namba watu wako
2.usiwaguse wakuu wa dunia.

Ukiwasomesha watu wako namba wataungana na adui zako kukumaliza
 
Utakuwa huwajui, labda unawazungumzia Wadendeule. Fikiria kidogo kuhusu hali ya Libya na Venezuela na almost nchi zote zenye utajiri wa mafuta na madini, kisha tathmini mkono mlafi & mkatili wa mkoloni katika ukimwa na ubaya wake uliopindukia.

Kiongozi yeyeto anaeunganisha watu hata awe anamiliki raslimali gani katu hawezi sambaratishwa kwa kutumia watu wake
 
Kanuni za kuongoza nchi yeyeto duniani ni mbili tu.
1.usisomeshe namba watu wako
2.usiwaguse wakuu wa dunia.

Ukiwasomesha watu wako namba wataungana na adui zako kukumaliza
Tatizo hujaeleza maana??? Wapiga-dili, wala rushwa, mafisadi, makuwadi lazima wasomeshwe namba, watake wasitake. Pili, hakuna kitu kinaitwa "wakuu wa dunia." Acha woga wewe Mwafrika!
 
Sijui kwanini chadema wanajidharau sana
Naona CHADEMA wameolewa wote na Amsterdam ndio maana wanashangilia kinoma kuona Mabwana zao wametoa checheeee😂😂

Bahati mbaya Mwamba halisi wa Africa JPM anawacheki tuu kwa kuwadharauu🤔😷
 
Haijawahi kutokea mtoto wa Miaka 10 kumtunishia baba yake misuli na akashinda.
NGOJA TUONE YETU MACHO
 
Huu utawala unatuvunjia mahusiano ambayo viongozi waliopita walihangaika kupata CONNECTION kwa muda mrefu.
Nyie wakina Kabudi mnaweza kutuburuza sisi(nyumbu) ila hao wazungu ni level nyingine kabisa.Achen mara moja kulicost taifa kwa kiburi chenu
 
Mlikuwa mnawacheka China few years ago sasa hivi China wako wapi? Nchi za kusini mwa Afrika zilikuwa ni makoloni ya wazungu na Tanzania ilizisaidia kujitawala, huu ujinga wao ndio umefika kikomo. Europe bila Afrika kuwalisha kutoka vyakula na mali ghafi hawana kitu. Labda kama bado umegubikwa na umatonya.

BTW internet pamoja na technology yote ya mawasiliano bila madini wanayochukua bure kutoka Afrika hawawezi kufanikiwa, nyinyi ndio mlioenda shule kusoma ujinga badala ya kupata elimu.


BTW mimi sivai mitumba vaa wewe, mkeo na familia yako.

Naona umehamia huku..

Kule jukwaa la GREAT THINKERS umrjaribu kuleta utopolo wako, kina Mag3 na Nguruvi3 wakakuingiza shule kidogo, lakini inashangaza kuwa kumbe bado hiyo shule haijakusaidia lolote...

Na hivi ni lini Tanzania imeanza kuwa chini ya utumwa wa mzungu?

Je ni kuanzia mwaka 2015 mara baada ya Magufuli kuingia madarakani?

Na ni utumwa upi eti unaouongelea wewe? Ule wa kuomba msaada wa fedha za kujengea vyoo? Ni ule wa kuomba budget support?

Ni huu wa kutegemea karibu 45% ya annual budget support ya nchi yetu kila mwaka kujazilizwa na wao?

Na hivi unaweza kutuambia tunaanza kuukataaje kwa mfano huo utumwa wa wazungu wa namna..?

Honestly, mimi sikuelewi unaandika nini tena kwa kutumia kalamu nyekundu...!
 
Kwa mtazamo wangu,ili uwashinde wazungu ni lazima ujitaidi kujitegemea angalau 95% zaidi ya hapo ni ngumu kuwashinda. Budget yetu 34%ni mchango wao, wasipotoa hiyo percent tunakuwa na deficit katika budget ya maendeleo.Na ukijitaidi kujitegemea bado watakufanyia figisu mpaka utawatafuta mwenyewe
 
Uchumi wa Marekani kweli ni wa kuja kupigana vita vya kiuchumi na nchi ambayo inasaidiwa kujengewa matundu ya vyoo?Nchi ambayo ina import wembe kwamba bado haina techinolojia ya kuunda wembe, nchi inayo import toothpick.

Tuna Techinolonia gani tunayo watishia Marekani au EU? si tunatumia Internet yao? hizi Facebook si za kwao?

Si tuna vaa mitumba kutoka kwao? how come tuvae mitumba yao then tuseme tuna vita na wao?

Ni hilo Bwawa la umeme? au Flyover ya Ubungo? ndo vitu tishio kwa Wazungu?

Katika Majimbo yote ya Marekani hakuna hata moja ambalo tunalikaribia na hatutarajii kulikaribia hata kwa miaka 200 ijayo, Jimbo kama California GDP yake ni kubwa kuliko nchi zote za Africa combined.

How come nchi ambayo inazidiwa pato na makampuni ndo ije ipigwe vita? BP wana turn over kubwa kuliko GDP yetu.

Marekani ana vita ya Kiuchumi na nchi kama China, EU na hao wakina Russia ila si chi kama Tanzania ambayo bado techinolojia ya kuuda pini bado hatuna.

Ulaya wana vita vya kiuchumi na nchi kama China, Russia na kadhalika na hata hivyo sio vita bali wanapambana kuhakikisha wanafaidika, China inapambana kuhakikisha inafaidika na EU na EU nao hivyo hivyo.

CCM wakisema tuna vita vya kiuchumi na nchi kama Kenya nitawaelewa ila sio hao ambao huwa wanatujengea vyoo vya shule, wanatupatia ARV, wanatupa vyandarua.

Hizi Propaganda ni za kijinga na kuna wajinga wameaminishwa na wameamini, ni bahati mbay nchi ina kiwango kikubwa cha watu wasio weza ku reson.

In my opinion, this was more an emotional writing than a rational writing!

Nasita kuamini kwamba umesoma historia vizuri! Nini kiliwaleta wakoloni Africa (in general) na Tanzania (in particular)? Je, sababu zilizowaleta enzi hizo sasa hazipo?

Je, sisi Watanzania tukisema wakoloni walitunyonya napo tunafanya propaganda, kwa sababu economically, technologically, etc., walikuwa wanatuzidi na bado hata leo wanatuzidi?

Je, kunyonywa kwa mataifa masikini na mataifa tajiri kuliisha lini? Unajua kwamba baada ya ukoloni (colonialism) kilichofuata ni ukoloni mamboleo (neocolonialism)? The two have one thing in common: exploitation.

Sasa badala ya kuandika sana lakini ukiwa umeachia emotions to run the whole show, please take a pause and review our historical relationship with these so-called superpowers!

Obviously, we need them for one reason and they need us for a different reason. Our reasons for needing each other have never been exactly the same!
 
Tangu lini ninyi mkawa na swali la msingi wakati Bungeni Mr Hai kashindwa kuingia???
Mi siko upande huo wa mr Hai,
Mi nasimama na wanannchi wanaodhulumiwa na mkoloni mweusi.
Wazungu wanaona mmekula kodi zao tofauti na makubaliano. Huo ni ufisadi wa wazi kabisa bila aibu. Mmeifanya Tz NGO ya kuombea hela Ulaya halafu mnazitumia na madem zenu. €27m siyo hapa wewe mzee.
 
Kiukwei ndugu umeshindwa kuiongelea na kuishibisha hoja yako. Kumbuka asilia zaid ya 100 nchi zilizoendelea zinaishi na kutamba at our expenses. Leo hii Europe ikifungiwa mrija wakuinyonya Africa basi ndio mwisho wake. Hyo vta ya kiuchumi ni kwamba tunahitaji kujitegemea na sio kuingiliwa kwa mambo ata ya ndani digest it mkuu.
 
Mi siko upande huo wa mr Hai,
Mi nasimama na wanannchi wanaodhulumiwa na mkoloni mweusi.
Wazungu wanaona mmekula kodi zao tofauti na makubaliano. Huo ni ufisadi wa wazi kabisa bila aibu. Mmeifanya Tz NGO ya kuombea hela Ulaya halafu mnazitumia na madem zenu. €27m siyo hapa wewe mzee.
Wazungu wana hasira na Mr Mzungu & Bob waliowadanganya wangeshinda kwa kufanya machafuko na maandamano; miradi ya JPM ya ujenzi wa taifa imewachefua akili.
 
In my opinion, this was more an emotional writing than a rational writing!

Nasita kuamini kwamba umesoma historia vizuri! Nini kiliwaleta wakoloni Africa (in general) na Tanzania (in particular)? Je, sababu zilizowaleta enzi hizo sasa hazipo?

Je, sisi Watanzania tukisema wakoloni walitunyonya napo tunafanya propaganda, kwa sababu economically, technologically, etc., walikuwa wanatuzidi na bado hata leo wanatuzidi?

Je, kunyonywa kwa mataifa masikini na mataifa tajiri kuliisha lini? Unajua kwamba baada ya ukoloni (colonialism) kilichofuata ni ukoloni mamboleo (neocolonialism)? The two have one thing in common: exploitation.

Sasa badala ya kuandika sana lakini ukiwa umeachia emotions to run the whole show, please take a pause and review our historical relationship with these so-called superpowers!

Obviously, we need them for one reason and they need us for a different reason. Our reasons for needing each other have never been exactly the same!

Well said. Hiz ndio akili sio unaendeshwa kimuemuko
 
Back
Top Bottom