US alerts travelers to Tanzania: Exercise increased caution in Tanzania due to crime, terrorism, health issues, and targeting of LGBTI persons

w0rM

Member
May 3, 2011
68
164
Imewatahadharisha Wananchi wake juu ya kuongezeka kwa Uhalifu, Ugaidi, sintofahamu katika masuala ya Afya na kuwalenga Watu wanaohusika na mahusiano ya jinsia moja

Imedai Uhalifu wa dhuluma, kama vile kushambulia, unyanyasaji wa kijinsia, ujambazi na uporaji ni kawaida na Polisi wa Tanzania wanaweza kukosa rasilimali kupambana na uhalifu mkubwa

Aidha, imedai vikundi vya magaidi vinaendelea kupanga njama za kushambulia Tanzania na wanaweza kushambulia bila onyo au onyo kidogo, wakilenga Balozi, vituo vya Polisi, Misikiti na sehemu nyingine zinazopitwa mara kwa mara na Wageni

Katika hatua nyingine imesema mnamo Septemba 10, 2019 Shirika la Afya Dunia na Kituo cha Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa zilipata taarifa rasmi juu ya kuwepo kwa mtu aliyefariki siku mbili nyuma, na ugonjwa unaodhaniwa ni Ebola na mtu huyo alipokuwa Tanzania alitembelea Songea, Njombe na Mbeya

Lakini pia, tahadhari hiyo iliyotolewa na Idara ya Usafiri ya Marekani imedai Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wamekuwa wakikamatwa, wakilengwa, wakidhalilishwa na ama wakifunguliwa mashtaka yasiyowahusu na waliokuwa wameshikiliwa wakidhaniwa kujihusisha na mapenzi ya aina hiyo yawezekana walipimwa kupitia njia ya haja kubwa
******

Exercise increased caution in Tanzania due to crime, terrorism, health issues, and targeting of LGBTI persons.

Violent crime, such as assault, sexual assault, robberies, mugging, and carjacking, is common. Local police may lack the resources to respond effectively to serious crime.

Terrorist groups continue plotting possible attacks in Tanzania. Terrorists may attack with little or no warning, targeting embassies, police stations, mosques, and other places frequented by Westerners.

On September 10, 2019, CDC and the World Health Organization (WHO) were made aware of unofficial reports regarding the unexplained death of a person two days earlier from probable Ebola in Dar es Salaam, United Republic of Tanzania. This individual reportedly traveled around the country while ill, including to the cities of Songea, Njombe, and Mbeya.

Members of the LGBTI community have been arrested, targeted, harassed, and/or charged with unrelated offenses. Individuals detained under suspicion of same-sex sexual conduct could be subject to forced anal examinations.

Read the Safety and Security section on the country information page.

If you decide to travel to Tanzania:
  • Always carry a copy of your U.S. passport and visa and keep original documents in a secure location.
  • Be aware of your surroundings.
  • Do not leave your food or drink unattended.
  • Stay alert in all locations, especially those frequented by Westerners.
  • Visit CDC for more information regarding illnesses in Tanzania.
  • Avoid public displays of affection particularly between same-sex couples.
  • Enroll in the Smart Traveler Enrollment Program (STEP) to receive Alerts and make it easier to locate you in an emergency.
  • Follow the Department of State and the US Embassy in Tanzania on Facebook and Twitter
  • Review the Crime and Safety Report for Tanzania.
  • U.S. citizens who travel abroad should always have a contingency plan for emergency situations. Review the Traveler’s Checklist.
********

Aidha, awali Marekani ilitoa tahadhari kwa Wanaosafiri kuja Tanzania kuhusu uwepo wa Ebola, ambapo ilisema

 
Hawa marekani huwa wana hila tu na nchi zet,maana wao huonekana kuandaa mabaya yote yanayotukuta Kisha kujifanya wasaidizi wetu.na ndio maana katibu mkuu wa afya akaanza kulazimisha Tanzania itangaze tu kuwa mna EBOLA yaani Hawa dah
 
Hawa marekani huwa wana hila tu na nchi zet,maana wao huonekana kuandaa mabaya yote yanayotukuta Kisha kujifanya wasaidizi wetu.na ndio maana katibu mkuu wa afya akaanza kulazimisha Tanzania itangaze tu kuwa mna EBOLA yaani Hawa dah
Wakiona wameshindwa sehemu fulani, huwa wanaanza hizi ghiriba zao.
Mwenyezi Mungu atatulinda. Siamini kabisa katika haya wanayoyafanya
 
Halafu utakuta aliye andika hiyo makala ni Mtanzania..!!!! Yaani hajali kama anaadhiri sector ya utalii na kutatokea mazuzu yatashangilia....
Alafu Wamarekani si wapenz wakutembelea Tanzania na Africa, Wanaopenda kuja Tanzania ni wazungu kutoka ulaya si wa Marekani.
 
Tatizo letu ni wanasiasa hasa jiwe kukumbatia siasa za kuligawa taifa kati ya wapinzani na CCM. Tunashuhudia matendo machafu kabisa yakifanywa dhidi ya baadhi ya raia. Ni wazi kuwa hao Marekani wanatahadharisha raia wao kwa kuzingatia habari na matukio halisi yanayoyokea kwa watu mbalimbali.

Mifano ipo mingi, hasa ya matukio ya utekaji na mauaji ambayo hayajatolewa maelezo yanayoridhisha.

Kama maiti zinaweza kuokotwa kisha polisi wanadai kuna watu wasiojulikana, ni wazi kuwa nchi imekaliwa na magaidi ambayo yamewashinda polisi na majeshi mengine.
 
Yaani jamaa wanakera basi tu, watu tunaishi very peaceful halafu ndio tunaambiwa kuwa nchi yetu ina uoza wote huo.

Unaweza fikiri hao ni watu wa aina gani.
 
Unaficha taarifa na unakataa kutoa ushirikiano ukidhani unalinda maslahi ya nchi. Badala yake unajikuta ndio unajitangaza zaidi uonekane una tatizo, na hao uliodhani umewafichia habari ndio wanakuwa watu wa kutangaza usiyotaka watu wayasikie!

Kama hakuna tatizo, na hata kama tatizo ndio linaanza, kuna ubaya gani wa kutoa ushirikiano kwa Shirika kama WHO? Hata kama mtu huyo alikufa kwa Ebola, ikajulikana na kudhibiti sehemu alikopitia kuna ubaya gani?
Watalii wangeendelea kuja tu, wakijua hali inajulikana ilipo na kuna uhakika wa kudhibiti ugonjwa usienee.

Sasa, hao watalii watawekwa woga, kwa sababu tu hatukujua namna ya kushughulikia swala zima la mgonjwa yule.
HATUAMINIKI KWA LOLOTE! Hakuna mtu anyejitoa mhanga kwenda sehemu asiyojua usalama wake upo vipi akiwa huko.
 
Alafu Wamarekani si wapenz wakutembelea Tanzania na Africa, Wanaopenda kuja Tanzania ni wazungu kutoka ulaya si wa Marekani.
Matatizo yetu makubwa ni haya. Kuzungumzia jambo tusilolifahamu kabisa. Umeangalia takwimu za "Tanzania Tourism Board" ukajiridhisha ni sehemu zipi tunakopatia watalii wengi?

Mbona ni jambo rahisi tu kuzipata taarifa hizi..., au hata hujui kuitumia google?
 
Back
Top Bottom