Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,350
Mashindao ya Olympics ni mashindano makubwa ya kimataifa na ya hadhi ya juu duniani yanayojumuisha mataifa mbalimbali kutoka mabara yote duniani lakini mataifa mengi zaidi yakiwa ni kutoka Ulaya. Mashindano haya hufanyika kila baaada ya miaka 4. Tofauti na mashindano mengine haya mashindano huwa na vipengele vingi na washindi wengi ambao huweza kujipatia medali za hadhi mbalimbali
Mzozo mkubwa umezuka mwaka huu kuhusu ushiriki wa mataifa mawili ya Urusi na Belarus katika mashindano hayo ambayo yatafanyika mwaka 2024 nchini Ufaransa katika jiji la Paris. Mataifa zaidi ya 40 hasa ya Ulaya yamepinga ushiriki wa Urusi na Belarus kutokana na uvamizi unaoendelea huko Ukraine.
Mataifa hayo wameenda mbali zaidi wakitishia kutoshoriki ikiwa kamati inayoanda mashindano hayo haitasikiliza madai yao ya kuziondoa Urusi na Belarus.
Poland imetoa wazo mbadala la kuunda timu za wakimbizi na watu walio uhamishoni ambao ni Raia wa Urusi na Belarus wanaopinga uvamizi wa Ukraine na tawala za kidikteta za mataifa hayo kuyawakilisha.
Zelenskyy naye ametoa kauli nzito kushinikiza madai hayo akisema Timu za Urusi na Belarus katika mashindano hayo zitawakilisha vurugu au mateso. Ikiwa hili litafanikiwa itakuwa ni hatua nyingine ya Urusi kuendelea kutengwa zaidi na sehemu kubwa ya ulimwengu.