Urusi yasamehe afrika, umasikini umezidi afrika

Urusi yasamehe afrika, umasikini umezidi afrika

janja hiyo kaona bora aimarishe uhusiano na waafrika tu maana wakubwa wenzake wanamtenga kudadeki!!
 
Japo hii ni habari ya mwaka jana 2017, hizi ni pesa nyingi sanaaa saaana.
Maana amesamehe nchi kama CUBA, IRAQ, KOREA KASKAZINI na MONGOLIA kitu ambacho kinashangaza sana hasa kipindi hiki wakati Uchumi wake umeyumba sana saanaa. Ukiyabadilisha haya madeni ni bajeti ya Tanzania kwa miaka zaidi ya mitano haya ni matrilioni ya pesa nyingi sana na yanaonyesha ni jinsi gani nchi nyingi za Africa zilikuwa tegemezi kwa jumuiya ya Kisovieti ya Urusi. Kwa huu utegemezi basi nasema kuanguka kwa Urusi kilikuwa na madhara makubwa kwa nchi nyingi duniani, madhara makubwa sanaa sanaaa kiuchumi na kiusalama.

NB: Watanzania tujifunze kujitegemea aseee!

CC: Bukyanagandi , chige , Palantir , Maalim Shewedy , ze kokuyo , nankumene
Kama ulivyosema, hii issue sio mpya and for what I know, hii ni similar to 1995 IMF Program iliyofahamika kama Heavily Indebted Poorest Countries (HIPC) Initiative.

Under HIPC Initiatives, IMF na Washirika wake walisamehe madeni kwa selected countries kwa condition kwamba madeni husika yawe channeled kwenye mipango ya maendeleo especially elimu na afya.

Kwa IMF's HIPC Initiative, ndo ile hapa kwetu iliibua shule za kata na related programs kv MMES, MMEM, MMEKWA n.k bila kusahau injini kuu; MKUKUTA!

So, Russia nao wakaja na debts cancelation program yao similar to IMF's but different in implementation. Na hii ya USD 20 Billion for Africa, walitangaza kufuta tangu 2012 for selected African countries including Tanzania.

Kama ilivyokuwa kwa IMF, Russia nao wakataka madeni hayo yaelekezwe kwenye sekta za maendeleo though sijawahi kusikia pakiwa na known programs kama ilivyokuwa kwa IMF... hapa ndipo ninaposema similar to IMF but different in implementation though in public haioneshi kuna strings attached.

Kwa mfano, possibly for the same 2012 debt cancelation program; mwaka jana Russia walitangaza kufuta madeni ya zaidi ya Sh. 350 Billion kwa Ethiopia. Lakini hapo hapo kulikuwa na business deals kati ya mataifa hayo mawili!

Aidha, Russia hao hao, in 2013 walifikia muafaka wa kufuta USD 32 Billion kwa Cuba chini ya matarumbeta ya friendship!

Hata hivyo, miaka miwili baadae zikavuja habari za Russia kufungua tena ( reopening) Lourdes Facility... signals intelligence facility ambayo ilikuwa inatumika na Soviet against US wakati wa Vita Baridi!

Kama utakumbuka, mwishoni mwishoni mwa Utawala wa JK kuliibuka habari za Putin kutaka kuja Tanzania.

Endapo habari zile zilikuwa kweli na endapo Putin angekuja Tanzania basi bila shaka a nature of quid pro quo deal kati ya Russia & Tanzania kuhusu deni letu ndipo tungefahamu zaidi.

Sanasana kwa Afrika wanachoangalia sana in exchange ni investment opportunities especially in energy sector!

Pamoja na yote hayo, umeibua hoja ya how come now wakati Russia ipo kwenye misukosuko ya kiuchumi!

The answer is: Ikiwa nipo sahihi kwamba it's the same 2012 program basi haiwezi kuwa na effect kwa kuangalia misukosuko ya sasa kwa sababu deni husika lilifutwa kitambo!

That's one but second, hata kama wasingefuta sioni Africa ingelipa vipi na lini deni husika hasa ukizingatia ni deni tangu enzi ya Soviet... it's bad debt!

Kama ndivyo, naona ni smart move kwa Russia kupiga matarumbeta ya kutusamehe madeni kwa sababu hata wasingesamehe, bado possibility ya kulipwa ingekuwa ndogo... international political stunts!!

Kwa mfano Afghanistan peke yake waliwasamehe (nadhani) au walitangaza kuwasamehe USD 12 Billion!!

Sijui ni kwa namna gani Afghanistan wangeweza kulipa hilo deni!

Lakini wakati wanatengeneza international political stunts, kama kuna attached strings kwenye huko kusamehe; basi unakuta wanafaidika indirectly kwa kufuta madeni kuliko kukomaa kwamba wanadai wakati hawapati chochote!

All in all, kinachokera zaidi kwa madeni ya Russia kwa Africa, percent kubwa ilitokana na mikopo ya silaha za kivita!!

Hoja hiyo hapo juu inajibu suala la namna gani kudondoka kwa Soviet kumeleta madhara kwa nchi nyingi!

Effect ya kiuchumi kwa Africa inaweza isiwe kubwa sana kulinganisha na ukubwa wa deni lenyewe kwa sababu kwa kiasi kikubwa deni lenyewe lili-finance "military power"

But indirectly, tunaweza kuathirika kwa sababu I doubt kama hivi sasa atatokea "mjomba" wa kutupatia silaha kwa mkopo kama alivyokuwa anafanya Mjomba Soviet!! Matokeo yake, hivi sasa pesa ile ile tuliyotaka kuwekeza kwenye elimu, inabidi tumege kununua risasi za kukata kona wakati Uncle Soviet angetupatia in credit!
 
Madeni ya silaha hayo hakuna kingine toka kwa mrusi

Unarudia propaganda za MSM, labda nikukumbushe kitu: Bila silaha na mafunzo ya kijeshi kutoka Urusi Mataifa mengi ya Africa yangekuwa bado yapo chini ya Ukoloni wa Mataifa ya Magharibi au wewe hilo ulijui, nikiona waswahili wanabeza beza mchango wa Urusi nawashangaa sana, sijui hii inachangiwa na kutojua historia ya kweli kuhusu Taifa hilo kutokana na crusade ya media za baadhi ya nchi za Ulaya specifically UK, Ujerumani pamoja na kinara wao (USA) muda wote wana kitu kimoja akilini mwao nalo ni: kuizulia/chafua Russia - vyombo vya habari vya Magharibi vimefanikiwa sana kuchota akili za baadhi wasomaji/watazamaji wa MEDIA zao, hakuna anaye hoji kama habari zenyewe zina ukweli wowote au la?

Ukweli wa mambo ni kwamba katika Mataifa ya Africa, Asia na Latin Amerika hakuna ambaye hajui mchango mkubwa ulio wahi kutolewa na Russia kwa maendeleo na ustawi wao, nani ambaye hajui/hakumbuki misada ya kifedha vile vile na kusomesha bure vijana wengi kutoka Afrika na Mataifa mengine ya Dunia ya tatu kwenye Vyuo Vikuu vyao, mfano: madaktari bingwa, wahandisi: mitambo, ujenzi, umeme nk; Walimu wa nyanja za sayansi na teknolojia. Warusi walikwenda mbali zaidi wakajenga Chuo Kikuu huko Moscow (Lumumba) kwa madhumuni ya kuwashomesha vijana ambao wengi wao wamekuja kuwa Viongozi wa Mataifa yao hapo baadae.

Wamewahi kujenga viwanda vya nguo na nyuzi, madawa, ku-assemble matrekta na majembe, uchimbaji wa visima vya maji, kujenga Mashule ya Ufundi na Kilimo katika Mataifa mbali mbali ya Afrika, Asia na Latin Amerika, walileta mpaka walimu wa Sekondari na vyuo vikuu, walijenga one of the biggest Hydroelectric Generating stations in Africa namely Aswan Dam huko Misri na Akasombo huko Ghana - sijui kwa nini Rais Nyerere alijisahau kuomba Warusi wamjengee Mitambo ya kuzalisha umeme mto wa Rufiji (Stigler Gordge) Warusi wangejenga fasta kama walivyo jenga Aswan DAM, saa hizi tungekuwa mbali sana kwenye nyanja za uzalishaji umeme Mkubwa, badala yake washauri wa Baba wa Taifa wakamshauri akimbilie Magharibi mwisho wa siku mradi ukahujumiwa hakuna cha maana kilicho fanyika mpaka leo save ujio wa JPM. Bottom line is: tusiwe tunabeza beza vitu bila ya kufanya tafiti za kutosha.
 
Japo hii ni habari ya mwaka jana 2017, hizi ni pesa nyingi sanaaa saaana.
Maana amesamehe nchi kama CUBA, IRAQ, KOREA KASKAZINI na MONGOLIA kitu ambacho kinashangaza sana hasa kipindi hiki wakati Uchumi wake umeyumba sana saanaa. Ukiyabadilisha haya madeni ni bajeti ya Tanzania kwa miaka zaidi ya mitano haya ni matrilioni ya pesa nyingi sana na yanaonyesha ni jinsi gani nchi nyingi za Africa zilikuwa tegemezi kwa jumuiya ya Kisovieti ya Urusi. Kwa huu utegemezi basi nasema kuanguka kwa Urusi kilikuwa na madhara makubwa kwa nchi nyingi duniani, madhara makubwa sanaa sanaaa kiuchumi na kiusalama.

NB: Watanzania tujifunze kujitegemea aseee!

CC: Bukyanagandi , chige , Palantir , Maalim Shewedy , ze kokuyo , nankumene
$20 bilioni ni bajeti ya TZ for 5yrs? Lumumba acha mahaba yako kwa Urusi bhana, this is too much na huo ni uongo mkubwa, may be umepitiwa labda. Bajeti ya Tanzania 2017/2018 ilikuwa $13.4bilion (Tsh 31.75trilion). Japo iliyotekelezwa kwa mwaka huo ilikuwa $9.8bilion (Tsh 23.65trilion) sasa hapo inakuwaje hiyo pesa itumike kwa bajeti ya Tz for 5yrs? Achni mahaba ya kusifia uongo, hata kama tuko maskini ila sio kiwango cha kutumia $20 bilioni for 5yrs,hayo ni matusi.
 
Africa hata leo wazungu waseme watuachie Ulaya waje Africa,baada ya miaka 10 nakwambia waafrica tutaomba tena misaada ya kwa wazungu ambao tuliwaachia Africa.

Sijui Africa tuna tatizo gani
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Aliye turoga alikwisha kufa mkuu
 
$20 bilioni ni bajeti ya TZ for 5yrs? Lumumba acha mahaba yako kwa Urusi bhana, this is too much na huo ni uongo mkubwa, may be umepitiwa labda. Bajeti ya Tanzania 2017/2018 ilikuwa $13.4bilion (Tsh 31.75trilion). Japo iliyotekelezwa kwa mwaka huo ilikuwa $9.8bilion (Tsh 23.65trilion) sasa hapo inakuwaje hiyo pesa itumike kwa bajeti ya Tz for 5yrs? Achni mahaba ya kusifia uongo, hata kama tuko maskini ila sio kiwango cha kutumia $20 bilioni for 5yrs,hayo ni matusi.

Nimesema Kwa Ujumla wa hizo nchi zote (AFRICA, MONGOLIA, CUBA , IRAQ na NORTH KOREA) zote ndugu yangu mbona hamnielewi aisee...?? Tatizo liko wapi hapa ?? Hebu jaribu kuangalia Premise the Statement yangu. "Ukiyabadilisha haya madeni yapi "AFRICA, CUBA, MONGOLIA, IRAQ na KOREA KASKAZINI" yanakuwa bajeti ya Tanzania kwa miaka mitano...Tatizo hapa liko wapi ??? (Msinilishe maneno)
 
President Vladimir Putin said that Russia had canceled the debt of African countries in excess of $ 20 billion.

To help the African continent overcome poverty, Russia has decided to cancel more than $ 20 billion in debt contracted by African countries.

“As part of the initiative to help the poorest and most heavily indebted countries, we have canceled more than $ 20 billion in debt for the benefit of different African countries,” Putin said. Russian media.

The Russian leader announced the initiative following a meeting with Guinean President Alpha Condé.

Vladimir Putin added that in 2016, Russia had allocated $ 5 million to the African countries through the Organisation of African Unity The United Nations Food and Agriculture Organization.

Russia cancels all debts of African countries in excess of $ 20 billion


Afrika si masikini as a continent, isipokuwa uongozi wa kipuuzi na wizi unaofanywa na watawala wetu tena kwa makusudi tu ndiko kunafanya tuonekana kama tu masikini lakini si kweli. Viongozi wetu ndiyo wanaolifanya hili bara letu lidharauliwe na watu na they don't give a damn kuhusu wananchi wao kuteseka. Angalia karibia deni la bilioni 20 za kimarekani tumesamehewa waafrika, usikute asilimia kubwa ya hizi pesa wamekula wenyewe viongozi na watu wao wa karibu.
 
Unarudia propaganda za MSM, labda nikukumbushe kitu: Bila silaha na mafunzo ya kijeshi kutoka Urusi Mataifa mengi ya Africa yangekuwa bado yapo chini ya Ukoloni wa Mataifa ya Magharibi au wewe hilo ulijui, nikiona waswahili wanabeza beza mchango wa Urusi nawashangaa sana, sijui hii inachangiwa na kutojua historia ya kweli kuhusu Taifa hilo kutokana na crusade ya media za baadhi ya nchi za Ulaya specifically UK, Ujerumani pamoja na kinara wao (USA) muda wote wana kitu kimoja akilini mwao nalo ni: kuizulia/chafua Russia - vyombo vya habari vya Magharibi vimefanikiwa sana kuchota akili za baadhi wasomaji/watazamaji wa MEDIA zao, hakuna anaye hoji kama habari zenyewe zina ukweli wowote au la?

Ukweli wa mambo ni kwamba katika Mataifa ya Africa, Asia na Latin Amerika hakuna ambaye hajui mchango mkubwa ulio wahi kutolewa na Russia kwa maendeleo na ustawi wao, nani ambaye hajui/hakumbuki misada ya kifedha vile vile na kusomesha bure vijana wengi kutoka Afrika na Mataifa mengine ya Dunia ya tatu kwenye Vyuo Vikuu vyao, mfano: madaktari bingwa, wahandisi: mitambo, ujenzi, umeme nk; Walimu wa nyanja za sayansi na teknolojia. Warusi walikwenda mbali zaidi wakajenga Chuo Kikuu huko Moscow (Lumumba) kwa madhumuni ya kuwashomesha vijana ambao wengi wao wamekuja kuwa Viongozi wa Mataifa yao hapo baadae.

Wamewahi kujenga viwanda vya nguo na nyuzi, madawa, ku-assemble matrekta na majembe, uchimbaji wa visima vya maji, kujenga Mashule ya Ufundi na Kilimo katika Mataifa mbali mbali ya Afrika, Asia na Latin Amerika, walileta mpaka walimu wa Sekondari na vyuo vikuu, walijenga one of the biggest Hydroelectric Generating stations in Africa namely Aswan Dam huko Misri na Akasombo huko Ghana - sijui kwa nini Rais Nyerere alijisahau kuomba Warusi wamjengee Mitambo ya kuzalisha umeme mto wa Rufiji (Stigler Gordge) Warusi wangejenga fasta kama walivyo jenga Aswan DAM, saa hizi tungekuwa mbali sana kwenye nyanja za uzalishaji umeme Mkubwa, badala yake washauri wa Baba wa Taifa wakamshauri akimbilie Magharibi mwisho wa siku mradi ukahujumiwa hakuna cha maana kilicho fanyika mpaka leo save ujio wa JPM. Bottom line is: tusiwe tunabeza beza vitu bila ya kufanya tafiti za kutosha.
Dah! Mi ni bonge la shabiki la Russia kiasi kwamba miongoni mwa news subscription nilizonazo ni za Russia!

Lakini je, kwavile nina mahaba na Russia ndo niwe nafumbia macho some facts kuhusu Russia?!

Kwangu hilo sio sahihi! Mahaba yetu yasitufanye tuache kuzungumza ukweli!

In short, uliyosema ni kweli; sana tu kwamba Soviet imefanya mambo mengi sana kwa Africa... tena sana!

Hata hivyo, alichosema Mchizi sio propaganda za mataifa ya Magharibi bali ni ukweli! Inawezekana tatizo ikawa ni tone aliyotumia au jinsi alivyowasilisha mada yake!

Hata hivyo, hiyo haiondoi ukweli kwamba, kiasi kikubwa cha haya madeni ni gharama za kijeshi; hususani silaha za kivita.

Hata hivyo, baadhi ya nchi bado huwezi kuzilaumu linapokuja suala zima la madeni yao kutokana na gharama za kivita.

Msumbiji na Angola kwa mfano. Hata baada ya kumfukuza Mreno bado nchi hizo zikajikuta zinaingia kwenye vita ndefu dhidi ya vibaraka (RENAMO & UNITA respectively)!

That war had to be financed na Soviet wali-play major role kuzisaidia Msumbiji na Angola!

Hata baada ya White minorities wa South Rhodesia(Zimbabwe) kujitangazia uhuru from "mother British" na kutaka kuifanya Zimbabwe kuwa nchi yao; Wana Zimbabwe wenyewe kama akina Joshua Mkomo had to stand against these white minorities na Soviet wali-play major military role katika kuwa-support akina Mkomo.

Hali inayofanana na hiyo ilitokea pia kwa Namibia and South Africa.

Lakini pamoja na umuhimu wote huo, bado madeni hayo yatabaki kuwa ni madeni yaliyotokana na gharama za kivita na si vinginevyo! Na katu hiyo haiwezi kuwa ni western propaganda bali ndio uhalisia!

Kwa mfano, Mwandishi wa Tass News Agency,
Lyudmila Alexandrova anaandika:
Screenshot_2018-04-01-23-07-10.png


Tass ni Russian Federal government news agency na Mwandishi wake;
Lyudmila Alexandrova hapo juu anatueleza 90% ya hayo madeni yametokana na mikopo ya silaha za kivita!

Sitaki kuamini mwandishi anayeandikia government news agency alikuwa misinformed kuhusu taarifa za serikali yake mwenyewe! Serikali ambayo, hiyo 90% ingenoga sana kama ingeandikwa (kuwa) ilitokana na ujenzi wa barabara, reli, visima vya maji, mashule n.k lakini kwa bahati mbaya au mzuri; hiyo 90%, at least according to Lyudmila Alexandrova, imetokana na silaha na 10% inayobaki ndiyo ili-finance hayo matamu matamu uliyotaja!

And REMEMBER, hiki kilikuwa ni kipindi cha Cold War! Kuwa supported na Soviet na kupewa silaha it's all about ideology and not necessarily kwamba kila waliowapa silaha ilikuwa ni kwa ajili ya kupigania uhuru!!
 
Nimesema Kwa Ujumla wa hizo nchi zote (AFRICA, MONGOLIA, CUBA , IRAQ na NORTH KOREA) zote ndugu yangu mbona hamnielewi aisee...?? Tatizo liko wapi hapa ?? Hebu jaribu kuangalia Premise the Statement yangu. "Ukiyabadilisha haya madeni yapi "AFRICA, CUBA, MONGOLIA, IRAQ na KOREA KASKAZINI" yanakuwa bajeti ya Tanzania kwa miaka mitano...Tatizo hapa liko wapi ??? (Msinilishe maneno)
Hayo ni makadirio ambayo sio ya kweli, ingelikuwa vizuri kama na hayo madeni ya hizo nchi ulizozitaja ungeliyaweka kwa figures ili tuelewe, make mleta mada kataja Afrika tu, vinginevyo ndo kubunia kwenyewe. Uzi upi umeonesha Urusi kazisamehe hizo nchi ulizozitaja?
 
Africa hata leo wazungu waseme watuachie Ulaya waje Africa,baada ya miaka 10 nakwambia waafrica tutaomba tena misaada ya kwa wazungu ambao tuliwaachia Africa.

Sijui Africa tuna tatizo gani
Jibu ni moja tu: Tuna Rogue Presidents, hakuna kitu kingine.
 
Hayo ni makadirio ambayo sio ya kweli, ingelikuwa vizuri kama na hayo madeni ya hizo nchi ulizozitaja ungeliyaweka kwa figures ili tuelewe, make mleta mada kataja Afrika tu, vinginevyo ndo kubunia kwenyewe. Uzi upi umeonesha Urusi kazisamehe hizo nchi ulizozitaja?

Utasemaje Makadirio siyo ya Ukweli wakati hata hayo madeni hujui ni kiasi gani ??
Kwanini usitafute hizo takwimu za hayo madeni halafu uje kupinga hapa kuliko kupinga kitu usichokifahamu ??
 
Utasemaje Makadirio siyo ya Ukweli wakati hata hayo madeni hujui ni kiasi gani ??
Kwanini usitafute hizo takwimu za hayo madeni halafu uje kupinga hapa kuliko kupinga kitu usichokifahamu ??
Wewe ndo umepoyonga tu, make umeleta habari zako za CUBA sijui N.Korea kwenye uzi wa mtu mwingine. Changia kilichoandikwa sio kuleta yakwako. Hiyo N.Korea kwenye uzi huu imeelezwa wapi?
 
Watanzania tujifunze kujitegemea aseee!
Hiki ndicho kisa cha kuchagua JF ID hii (TUJITEGEMEE)! Ila kuna baadhi ya watanzania wenzetu hawataki kusikia habari hii.
Ila watajua tu umuhimu wa kujitegemea. Halafu muda huu ndiyo ulikuwa mzuri kwa Afrika na TAnzania hasa, kujitegemea maana 'wakubwa' ambao wangezorotesha juhudi zetu za kujitegemea wako busy na 'bifu' zao.
 
Africa hata leo wazungu waseme watuachie Ulaya waje Africa,baada ya miaka 10 nakwambia waafrica tutaomba tena misaada ya kwa wazungu ambao tuliwaachia Africa.

Sijui Africa tuna tatizo gani
Tatizo ni kupinga kila kitu, akipatikana mtu wa kuhamasisha kujitegemea anaonekana hana demokrasia, tunapenda kulishwa na lelemama bila kujituma kwa umoja.
 
Tatizo ni kupinga kila kitu, akipatikana mtu wa kuhamasisha kujitegemea anaonekana hana demokrasia, tunapenda kulishwa na lelemama bila kujituma kwa umoja.
Tatizo sio kupinga kila kitu Ila Africa haina Viongozi wazalendo Kama akina Putin.

Mtu inakuaje Mtu achote fedha akafanyie mradi au kununua kitu bila idhini ya Bunge,halafu watu wakihoji wanapigwa risasi

Viongozi wa wenzetu hawana kelele nyingi hawabwabwaji wanapiga kazi so Kama huku maneno mengi vitendo hakuna, Uchumi taabani...Putin alipoanza kuiongoza Urusi na hivi Sasa ile nchi imebadilika kabisa. Njoo huku kwetu kwa shitholes Sasa....
 
Hiki ndicho kisa cha kuchagua JF ID hii (TUJITEGEMEE)! Ila kuna baadhi ya watanzania wenzetu hawataki kusikia habari hii.
Ila watajua tu umuhimu wa kujitegemea. Halafu muda huu ndiyo ulikuwa mzuri kwa Afrika na TAnzania hasa, kujitegemea maana 'wakubwa' ambao wangezorotesha juhudi zetu za kujitegemea wako busy na 'bifu' zao.
Hili juzi nililiandikia Article fupi sehemu fulani....
Muda huu wa Chaosi ndiyo tunatakiwa tujipange...
Aisee nimefurahi kuona kuna mtu tuna mawazo yanaringana kidogo..!
 
Back
Top Bottom