Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 11,328
- 17,832
Mkuu mambo mengine ni makubwa sana kwa uelewa wetu humu JF.Aaaaaaah, Ukishindwa kupata ulichokitegemea kwa wakati, basi unaweka faraja kwenye kidogo ulichokichukia. Putin anataka kumaliza vita kiaina, vinamchosha, anajifariji sasa na Donbasi (Donesk na Luansick), ambazo kabla ya vita tayari alikua nazo.
Donbas na Luhansk hazikuwa annexed na Russia kama Crimea ambayo tayari ilichukuliwa chini ya himaya ya Russia.
Sasa ukitaka kuelewa wanamaanisha nini wanaposema hatua ya kwanza ya mashambulizi yao imefikia malengo yao kuingia vitani sasa Russia wametangaza watu wa Luhansk watapiga kura ya maoni kuchagua kujiunga na Russia au hapana.
Maana yake sasa ameshamega kipande kingine cha Ukraine kuwa ehemu ya Russia.
Ndio maana viongozi wa Ukraine wanasema Russia anataka kuigawa nchi yao vipande viwili kama vile Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini.
Hiyo ni hatua ya kwanza tu kisha inaonekana ataanzia hapo kuanzisha uasi sehemu ya Ukraine iliyobaki na kuingiza majeshi kipande kilichobaki.
Poland wanasema Russia akishinda Ukraine ataendelea kuvamia nchi zingine za jirani. Hivyo anaomba wenzie wa EU na NATO waimarishe ulinzi wasitegemee ulinzi wa US tu.