Urusi yadai ‘hatua ya kwanza’ ya mashambulizi ya Ukraine imekamilika

Aaaaaaah, Ukishindwa kupata ulichokitegemea kwa wakati, basi unaweka faraja kwenye kidogo ulichokichukia. Putin anataka kumaliza vita kiaina, vinamchosha, anajifariji sasa na Donbasi (Donesk na Luansick), ambazo kabla ya vita tayari alikua nazo.
Mkuu mambo mengine ni makubwa sana kwa uelewa wetu humu JF.
Donbas na Luhansk hazikuwa annexed na Russia kama Crimea ambayo tayari ilichukuliwa chini ya himaya ya Russia.

Sasa ukitaka kuelewa wanamaanisha nini wanaposema hatua ya kwanza ya mashambulizi yao imefikia malengo yao kuingia vitani sasa Russia wametangaza watu wa Luhansk watapiga kura ya maoni kuchagua kujiunga na Russia au hapana.
Maana yake sasa ameshamega kipande kingine cha Ukraine kuwa ehemu ya Russia.

Ndio maana viongozi wa Ukraine wanasema Russia anataka kuigawa nchi yao vipande viwili kama vile Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini.

Hiyo ni hatua ya kwanza tu kisha inaonekana ataanzia hapo kuanzisha uasi sehemu ya Ukraine iliyobaki na kuingiza majeshi kipande kilichobaki.

Poland wanasema Russia akishinda Ukraine ataendelea kuvamia nchi zingine za jirani. Hivyo anaomba wenzie wa EU na NATO waimarishe ulinzi wasitegemee ulinzi wa US tu.
 
Na vifaa vya kijeshi alivyopoteza na hoja nyingine ni za hovyo ni basi tu ili tu mtu atetee ujinga ni mzigo wa mavi Putin amefail huo ndo ukweli lengo ni kumuondoa zelensky na kumuweka kibaraka imeshindikana
Kwahiyo alienda vitani akitegemea ya kwamba hakuna mwanajeshi wake yeyote atakaye uawa?
Ya kwamba alienda vitani akijua ya kwamba hatopata hasara ya vifaa?

Yaani waTz nimewanyoshea mkono kwa ujuaji ,mtu hujui hata bunduki inashikwaje alafu unamfundisha Putin nn cha kufanya kuhusu vita?

Urusi chini ya Putin imesha pigana zaidi ya tatu na yote kashinda lakini licha ya kushinda bado alipoteza maelfu ya wanajeshi wake.
Hakuna vita yeyote unayo weza kupigana alafu ww ukatoka salama bila kupoteza vifaa na wanajeshi kama hipo itaje.
 
Donbass ilikua chini ya Russia tokea 2014 acha uongo Ukraine haitawali Donbass tokea 2014
Pale unapo jifanya mjuaji kumbe kichwani ni ziro.
Kabla ya vita haijaanza asilimia 65 ya mkoa wa Dombas ilikuwa chini ya serikali ya Ukraine likiwemo jiji la Maliopol ndio maana mpaka sasa mapigano yanaendelea kwenye huo mkoa ili waweze kuchukua udhibiti kamili.
 
Aaaaaaah, Ukishindwa kupata ulichokitegemea kwa wakati, basi unaweka faraja kwenye kidogo ulichokichukia. Putin anataka kumaliza vita kiaina, vinamchosha, anajifariji sasa na Donbasi (Donesk na Luansick), ambazo kabla ya vita tayari alikua nazo.
Usichokijua nikwamba Urusi hakuna na shida ya kuichukua Ukraine hata kidog ila alitaka kuondoa hatari mlangoni mwake basi na ndo mana ikawa operation na sio vita, na kahakikisha kaiondolea uwezo kweli kweli ukraine kwa sasa, sasa sijui utawekeza nguvu ktk jesi ama kuhakikisha unarudisha huduma sawa kwa wananchi wako kwa miaka 100 ijayo ama laah? ujenge miundombinu upa nk.

Donbas inakwenda na maji kama Cremia ilo wasahau kabisa.
 
Back
Top Bottom