Urusi na miji ya siri

Urusi na miji ya siri

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,484
Urusi na Marekani ndio Dunia,kila mmoja wa wakubwa hawa ana vimbwanga vyake.
Inawezekana ni nchi chache sana zilikua zina miji ya aina hii.
Urusi ilikua ina miji ya siri,isiyokuwepo kwenye ramani ya Urusi na hata kwenye ramani ya dunia,ilkua ni miji ya siri ambayao Mataifa ya nje hayakupaswa kuijua na hata Warusi wenyewe,isipokua kwa watu maalimu tu.
Kazi kubwa ya miji hiyo ilikua ni sehemu yaani miji ilyotengwa maalumu ikiwa kumekuwa kumejengwa vituo maalum kwa ajili ya utafiti wa mambo ya kibaiolojia,kikemikali,matibabu,madawa,sayansi mbaalimbali,ujasusi,ubunifu wa vifaa vya hali ya juu sana vya kijeshi yaani silaha za hali ya juu,teknolojia ya hali ya juu,utafiti wa mambo ya anga za juu,mambo ya uchumi na mambo mengine wao waliyoona yanastahili kuwa ni siri.
Miji hii walipelekwa kwa siri sana vijana na wanasayansi wa kirusi tu na watafiti.Walichukuliwa kwa siri ama vyuoni ama kutoka ktk maeneo walikua wakiishi.kulikua kuna miji zaidi ya arobaini zama za USSR.Watu waliopelekwa huko waliishi hukohuko,kutoka ama kuingi ni kwa ruhusa maalum,walipewa kila aina ya huduma walioihitaji pamoja na raha ili wafanye kazi moja tu,utafiti kwa kila mmoja kulingana na fani yake.
Miji hii ilikua ikitambulika kwa anuani maalumu lakini kwa watu maalum,na wala watu wengi hawakua na ufahamu wa miji hii hata ndani ya urusi.Miji hii hadi leo bado ipo na inaendelea kuzalisha wataalamu wa vitu adimu duniani ila sijui kama bado ni siri.Wakati wa USSR kulikua na miji zaidi ya arobaini.Miji hii imekua ikilindwa vikali na makachero wa zamani wa KGB,pamoja na vikosi maalum vya SPETSNAZ. miji ii imekua ni mashamba madhubuti ya Urusi ya kuvuna Wanasayansi,na ndio kiburi na majigambo ya Urusi katika nyanja za sayansi na teknolojia,jeshi na ujasusi vimepatikana katika miji hii ya siri maarufu kama closed cities au secert cities bila kusahau star city.
 
Zamani sana Bibi yangu alipokuwa akisoma Urusi aliwahi kuniahadithia nilipomdadisi zaidi hii habari sikupata majibu ya moja kwa moja....
 
Kule Mtwara pia kuna kamji watu wengi hawaufahamu una mambo mengi na ya kutisha sana
 
hata hapa kwetu kule kunduchi kuna njia ya siri kuingia area 51 ya bongo
 
acheni utani bwana

Mkuu watu hawataki kujifunza,Hata hivyo Mwalim Nyerere alianzaisha kitu za namna hii katika maeneo kama matau hivi na vilikua ni siri na kuanza kuonesha matumaini,ila walipoingia wajuaji vituo vimeanza kufa na si siri tena.
 
Iran ina miji 6 ya siri ili kuweza kupambana na israel kikamilifu
 
Upo mji wa Siri hapa, kule Lindi Liwale unaitwa Ngende, huko balaa
 
Back
Top Bottom