Urusi kuwapatia waitifaki wake silaha za kisasa kabisa

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Tamko la Putin kuhusu utayari wa Russia wa kuwapatia waitifaki wake silaha za kisasa kabisa.

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, Moscow iko tayari kuwapatia waitifaki wake wa Amerika ya Latini, Asia na Afrika aina mbalimbali za silaha za kisasa kabisa.

Putin ameeleza hayo alipohutubia hafla ya teknolojia za kijeshi za vikosi vya ulinzi vya Russia 2022.

Amefafanua kwa kusema: Russia inapendelea kustawisha katika pande zote mashirikiano ya kijeshi na kiufundi, ambayo ndicho kitu chenye umuhimu katika mpango wa kuwepo dunia ya madola kadhaa yenye nguvu. Moscow inathamini uhusiano wake na nchi za Amerika ya Latini, Asia na Afrika na iko tayari kuzipatia aina mbalimbali za silaha za kisasa kabisa.

Rais wa Russia ameendelea kueleza kwamba, "Tuko tayari kuwapatia waitifaki wetu aina za kisasa kabisa za silaha, kuanzia silaha ndogondogo mpaka magari ya deraya, mizinga, ndege za kivita na ndege zisizo na rubani."

Tamko la Putin la kuwa tayari kuziuzia silaha za kisasa nchi waitifaki wa Russia ulimwenguni kote ni ishara ya mageuzi makubwa katika sera za jadi za Moscow katika uuzaji silaha. Kabla ya hapo, Russia ilikuwa ikijiwekea mipaka maalumu katika kuzipatia nchi zingine silaha; na kwa kutoa mfano, Moscow ilikuwa haikubali kuziuzia nchi nyingine silaha zake za kisasa zaidi kama makombora yenye kasi kubwa zaidi kuliko ya sauti. Makombora hayo, kama ilivyoonekana pia katika vita vya Ukraine, yanahesabiwa kuwa ni silaha inayoweza kubadilisha hatima ya vita.

Mfano mwngine ni wa mtambo wa ulinzi wa anga na makombora wa S-500, ambao Moscow imeuunda kwa ajili ya vikosi vyake vya ulinzi na hadi sasa haijaiuzia nchi yoyote ile. Ukweli ni kuwa, viongozi waandamizi wa kisiasa na kijeshi wa Russia siku zote wamekuwa na wahka wa kuchelea teknolojia yoyote mpya ya kijeshi ya nchi hiyo isije ikaingia mikononi mwa Magharibi na hasa Marekani; na ndio maana hadi sasa imesita kuzipatia nchi zingine baadhi ya silaha zake za kisasa.

Lakini kutokana na matukio yaliyojiri karibuni, hali na mazingira hivi sasa yamebadilika kikamilifu Kwa upande mmoja kujiri kwa kujiri vita vya Ukraine, Wamagharibi wakiongozwa na Marekani, wamehisi hii ni fursa mwafaka ya kuweka vikwazo vikali zaidi na ambavyo havijawahi kushuhudiwa katika pande na nyuga zote dhidi ya Russia zikiwemo za kidiplomasia na kisiasa na kuifanya ndio ajenda yao kuu kampeni ya kuitenga zaidi na zaidi Moscow katika uga wa kimataifa.

Ni kutokana na suala hilo, ndipo Moscow nayo ikaamua ichukue hatua ya kujibu mapigo kwa kustawisha uhusiano wake na nchi za maeneo mengine ya dunia. Katika hatua ya kwanza, suala hilo limedhihirika katika kustawishwa uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na nishati wa Russia na nchi zingine kama China na India.

Pamoja na hayo, kwa kutilia maanani kwamba Russia ni nchi ya pili inayouza silaha kwa wingi zaidi duniani, ni wazi kuwa moja ya nukta kuu katika muelekeo mpya ulioonyeshwa na Moscow ni kutangaza sera mpya za uuzaji silaha, ambapo kwa kuzingatia hotuba ya siku ya Jumatatu iliyotolew na Putin hakutakuwa tena na kizuizi au mpaka wowote katika suala hilo. Kwa kuzingatia bei ya chini ya silaha za Russia pamoja na ubora wake kuna uwezekano mkubwa muelekeo huu mpya utazifanya baadhi ya nchi zivutiwe zaidi kununua silaha kutoka Moscow na hivyo kufunga mikataba mipya ya ununuaji silaha kwa nchi hiyo.

Kwa upande mwingine, na kwa kuzingatia kuwa hivi sasa Russia inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni kutokana na vikwazo vya Magharibi, nchi hiyo imekuwa na hamu zaidi ya kuuza silaha zake kwa nchi zingine ili kwa njia hiyo, mbali na kuendeleza na kustawisha soko lake la uuzaji silaha iweze pia kujipatia mapato ya fedha za kigeni. Kuhusiana na nukta hiyo, Putin mwenyewe amesema: Moscow iko tayari kustawisha uhusiano na ushirikiano kwa ajili ya kuunda zana mpya za aina mbalimbali na vilevile kushirikiana katika hali na mazingira sawa. Kwa kustawisha mashirikiano mapana ya kijeshi na kiufundi itawezekana kuzihakikishia usalama wa kuaminika nchi zenye uhusiano na ushirikiano duniani.

Suala jengine kuhusiana na nukta hiyo, kwa kutilia maanani jitihada za mtawalia zinazofanywa na Russia za kuanzisha dunia ya kambi kadhaa zenye nguvu, ni kupungua utegemezi wa nchi za dunia kwa silaha za Magharibi, ambao umeandaa mazingira ya madola hayo na hasa Marekani ya kuzitwisha nchi wanunuzi matakwa yao, hali inayozidi kuimarisha ubeberu na nguvu za Magharibi za kuhodhi na kutawala siasa za dunia.

Bila shaka kubadilisha Russia muelekeo wake wa uuzaji silaha hautayafurahisha madola ya Magharibi na hasa Marekani, ambayo katika miaka ya hivi karibuni imefanya jitihada kubwa kwa kutumia sheria yake ya vikwazo ya CAATSA kuzizuia nchi zingine zisinunue silaha kutoka Russia, ambapo kwa kutumia vitisho na mbinu ya kurubuni imeweza hata kuvurga baadhi ya mikataba ya mauzo ya silaha kati ya Russia na nchi kama Misri na Indonesia.
 
Thanks a lot, ufafanuzi wako wa kina hauna mfanowe, unajieleza vizuri sana sana - BRAVO.
 
Russia kaona anakaa na siraha ambazo zinakuwa kama Teknolojia yake ni ndogo anataka ayauze yote, vitu vilivyo kwenye soko ni zile HIMARS, Javelin na Thermo ballistic za Russia.
 
Hana namna zaidi yakutaka ku-survive tu....kabla ya vita ya Ukraine ulishawahi msikia Mrusi au Waziri wake amekuja Africa kwa ziara ya namna yoyote?

Kagombana na Wazungu wenzake sasa ndio anajifanya bega to bega

Hakuna mtu mbaguzi wa ovyo kama Mrusi ushawahi sikia tu hata kuna Muafrika anacheza ligi za huko

Odemwinge sidhani kama atasahau baada warusi kuwashukuru waingereza kumnunua nyani huyo

WAPAMBANE NA HALI ZAO WAACHE KULIALIA

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kawaida ukipewa heshima ya ukubwa ridhika na heshimu wenzako, ukianza ubabe ,uporaji ,ujinga,mwisho wako umefika directly USA analazimisha kuingia vitani, na hapo ndipo wenzake wanapomsubiri kwa hamu,
Silaha kubwa na mbaya zitaenezwa ,wababe wataongezeka,
 
Siraha hizo kubwa zenyewe ndio zile zilioiteka Ukraine kama bwana Putin alivyosema masaa 72

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
safi sana Russia.
amejua kabisa hela ya kutengeneza silaha hana na silaha alizo nazo hana uwezo hata wa kuzifanyia update.

anacho kifanya Russia ni kuuza 40% ya silaha alizo nazo. Hata zile silaha za kimkakati ambazo kiuweled huwa hazitakiwi kuuzwa kiholela.

ili apate fedha za kutosha kutengeneza silaha zaid.

maana uwanja umeinama kwa upande wake halafu Beki hazikabi.

Russia hakika ni magenius kwenye uchumi.
big up.
 
akil za mwafrika ndio maana hata mshale hamuez kuunda , hata litokee taifa hatar kias gan , madhara yatakukuta ww na sio hao unao wafikiria
~pole sana mtazamo wako hauwezi badili historia na dira ya dunia.
~unamtazamo hasi dhidi ya waafrika,tuna wataalamu wa industral engineering wengi tu kwani bidhaa unazotumia wewe na ukoo wako i.e azam products.mo products,nondo,cement si zinazalishwa hapahapa
 
Hana namna zaidi yakutaka ku-survive tu....kabla ya vita ya Ukraine ulishawahi msikia Mrusi au Waziri wake amekuja Africa kwa ziara ya namna yoyote?

Kagombana na Wazungu wenzake sasa ndio anajifanya bega to bega

Hakuna mtu mbaguzi wa ovyo kama Mrusi ushawahi sikia tu hata kuna Muafrika anacheza ligi za huko

Odemwinge sidhani kama atasahau baada warusi kuwashukuru waingereza kumnunua nyani huyo

WAPAMBANE NA HALI ZAO WAACHE KULIALIA

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kipindi Samuel Eto'o analipwa dau kubwa zaidi duniani, alikua anacheza kijijini kwenu et.
 
Back
Top Bottom