Urusi kutoa jibu kali kwa Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,438
Russia yaionya Israel kufuatia kutunguliwa ndege yake katika anga ya Syria
Kufuatia ajali ya kutunguliwa ndege ya Russia katika anga ya Syria wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hiyo, Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa inayo haki ya kujibu mapigo kwa Israel kutokana na tukio hilo.
Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergueï Choïgou ametoa onyo kwa Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni Avigdor Lieberman na kumweleza kwamba Moscow inaibebesha Tel Aviv dhima kamili ya vifo vya wanajeshi wake 15.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza leo kuwa ndege moja ya kijeshi aina ya Ilyushin 20 (IL20) ikiwa na watu 15 ndani yake ilipotea kwenye rada karibu na kituo cha anga cha Hamimim mkoani Lattakia kaskazini magharibi mwa Syria.
Mbali na kubainisha kuwa ndege yake hiyo iliyotoweka wakati wa mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lattakia ilitunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa marubani wa Kizayuni waliitumia ndege hiyo ya Russia kama ngao wakati wa mashambulio yao hayo katika mji wa Lattakia.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza bayana kwamba kwa mtazamo wa Moscow hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni ya kiadui na imefanywa bila nadhari kwa makusudi, hivyo Russia inayo haki ya kutoa jibu dhidi ya hatua hiyo ya Tel Aviv...
4bpt2373c6410d19bj3_800C450.jpg
 
Russia yaionya Israel kufuatia kutunguliwa ndege yake katika anga ya Syria
Kufuatia ajali ya kutunguliwa ndege ya Russia katika anga ya Syria wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hiyo, Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa inayo haki ya kujibu mapigo kwa Israel kutokana na tukio hilo.
Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergueï Choïgou ametoa onyo kwa Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni Avigdor Lieberman na kumweleza kwamba Moscow inaibebesha Tel Aviv dhima kamili ya vifo vya wanajeshi wake 15.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza leo kuwa ndege moja ya kijeshi aina ya Ilyushin 20 (IL20) ikiwa na watu 15 ndani yake ilipotea kwenye rada karibu na kituo cha anga cha Hamimim mkoani Lattakia kaskazini magharibi mwa Syria.
Mbali na kubainisha kuwa ndege yake hiyo iliyotoweka wakati wa mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lattakia ilitunguliwa na vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa marubani wa Kizayuni waliitumia ndege hiyo ya Russia kama ngao wakati wa mashambulio yao hayo katika mji wa Lattakia.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza bayana kwamba kwa mtazamo wa Moscow hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel ni ya kiadui na imefanywa bila nadhari kwa makusudi, hivyo Russia inayo haki ya kutoa jibu dhidi ya hatua hiyo ya Tel Aviv...View attachment 870496
Mzee wa mahaba... Wajaribu waone
 
Kutumia dege la taifa kama Russia kama ngao katika mazingira hatarishi kama yale na ukafanikisha malengo yako huku ukimvuruga adui ni akili ya ajabu sana.

Hao marubani wa kizayuni kwa hakika wanastahili medani ya juu kabisa katika mambo ya kivita. Wameliletea taifa lao heshima kubwa sana; maayatollah kule Tehran wanachungulia na kusepa na vipedo vyao maana hawaamini kilichotokea.
 
Hakuna cha jibu Kali .Hao wanajuana sana.Note my words.Hapo waliofanywa zuba ni hao waarabu wako wa Syria na Waajemi.Mashambulizi yote ya Israel nchini Syria ,Urusi imeyabariki!
Urusi imebariki wanajeshi 14 na ndege yao kudunguliwa?wamewatoa wenzao kafara?
 
Hawa Jamaa mi hua nawaita wazee wa Mipasho kuanzia Klemlin mpka Tehran

Uki amua kujibu jibua haswaaaa kwa vitendo sio maneno maneno kama msemaji wa Simba
Bwana Manara!!!
 
Hiv yale machumachuma yenu s200, s300, s400 bado yapo Syria?
Vitukuu vya Daudi vimeliganda dege la kirusi kwa nyuma waka ambaa nalo wakapiga then wakasepa huku mdege wenyewe ukitunguliwa. Dah! ha ha ha; inaleta raha sana kwa kweli.
 
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kusikitishwa kwake na na vifo vya raia wa Urusi waliokowemo ndani ya ndege iliyoangushwa kwa bahati mbaya na vikosi vya serikali ya Syria.

Netanyahu amemwambia Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa Syria ilipaswa kulaumiwa kwa kuiangusha ndege hiyo.

Maafisa wa Urusi awali waliishutumu Israel kwa kuhusika na kitendo hicho ambacho ilidai wangekilipiza kauli ambayo ilipingwa vikali na Netanyahu ambaye alisema kamwe vikosi vyake havijihusishi na matukio kama hayo.

Netanyahu kushtakiwa?Watu 39 wafa baada ya jumba kulipuka Idlib Syria

Putin ameelezea tukio hilo kuwa ni la bahati mbaya na vikosi vyake havitarudi nyuma katika kuiunga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Source:bbc
 
Well said mkuu,labda nijazie jazie kidogo kwamba actually Putin amejitahidi kutumia lugha ya kidiplomasia alipo ongezea kwamba: kuanzia sasa modus operandi ya ulizi wa anga la Syria utafanyiwa marekebisho makubwa sana - hapo naona Israel na washirika wao wakuu wanapewa onyo kiaina - Waisrael wakijaribu tena kushambulia karibu na airbases za Urusi nchini Syria basi ndege za Israel na washirika wao zitatunguliwa na jeshi la anga la Urusi lililopo Syria, wanaweza kwenda mbali zaidi na kuhujumu miundo mbinu ya ulizi was anga la Israel-jamaa hawa msiwachukulie poa hata kidogo - ni wakimya kiasili lakini wakihamua kuchachamaa wataishangaza Dunia.
 
Hiv yale machumachuma yenu s200, s300, s400 bado yapo Syria?
Zile siraha s 400 huwezi tumia sehem kama syria maana ukiziwasha tu basi israel hawezi operate ndege zake maana rada zinaweza kushika hadi ndani ya nchi hiyo kwahiyo ndo mana tunaona israel anarusha tu vindege vyake nje na ndani ya israel.
 
Ukweli mchungu Israel mwiba mbaya sana kwa waarabu na ukitaka kujua kwanini kanga na kuku wanafanana ila kanga anaruka wajaribu tu siku wakinukishe na Israel
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom