Uropokaji wa Makamba utaisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uropokaji wa Makamba utaisha lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Dec 20, 2009.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,956
  Trophy Points: 280
  Kumfananisha Marehemu na dhahabu iliyopandwa? Sipati maana? navyojua mimi dhahabu hununuliwa, hutumika kwa urembo baada ya kuchimbwa kufinyangwafinyangwa kutengenezwa katika maumbo anayopenda muhusika, thamani yake hushuka na kupanda! sasa kama Dr Gama alikuwa dhahabu ni kumshushia heshima ina maana CCM ilimfinyangafinyanga ikamtumia ilivyotaka baada ya kumchimba na huyu bwana akaongezea wali-mpanda walivyotaka! Kha! Binafsi nathani alikuwa mtu safi na mchapa kazi! Hivi huyu Makamba ana wasaidizi? Huwa anaandika speeches au huwa ana-flow tu? Maana tunajionea mengi kila siku na yanakuja mengineyo! Fikra zake zimejaa fweza fweza tu zaidi ya utu!

  20th December 09
  JK kuhudhuria mazishi ya Gama

  Gideon Mwakanosya

  Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili mjini hapa leo mchana kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Dk. Lawrence Gama.
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma, alisema jana kuwa Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili leo saa 6:00 mchana ambapo ataelekea katika kijiji cha Amani Makolo atakakozikwa marehemu Gama.
  Hata hivyo, jana mamia ya wananchi walijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Gama mara baada ya mwili wake kuwasili mjini hapa. Mwili wa Gama ulipelekwa katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya Majimaji na kuagwa kwa heshima zote za kimila.
  Baadaye mwili huo ulipelekwa katika uwanja wa Majimaji ambapo viongozi mbalimbali wa chama na Serikali waliweza kutoa heshima zao.
  Akizungumzia utendaji wa Dk. Gama, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alisema marehemu alikuwa dhahabu iliyopandwa katika maeneo mbalimbali Tanzania na kwamba mchango wake hautasahaulika.
  Mwili wa marehemu Gama ulisindikizwa na Makamba ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emanuel Nchimbi.
  Marehemu Gama anatarajiwa kuzikwa leo mchana.  NIPASHE JUMAPILI
  http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11479
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Tanzania bwana, huu unafiki wa siasa utaisha lini? I mean yaani mwili ulisindikizwa na Makamba akishirikiana na Nchimbi? Incredible!

  Respect.


  FMEs!
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni kutokujua thamani ya utu wa mtu, kwani kwa hakika huwezi kumlinganisha mtu na kitu chochote. Utu wa mwanadamu uko juu ya thamani ya dhahabu, almasi na chochote kile mtu uwezacho kufikiria. Kumbe mheshimiwa yule alikosea kumlinganisha marehemu na dhahabu. Ni ajabu sana sijui alikuwa anawaza nini!
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,956
  Trophy Points: 280
  Kwani unafiki uko wapi? hawakumsindikiza kweli au?
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Sijawahi kuona thamani ya mtu inafananishwa na kitu hata kama ni cha thamani namna gani. Im sorry... but inategemeana ni nani ameongea... angeongea Kikwete wote tungeduwaa, lakini kama ni Makamba tushamzoea....
   
 6. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kuna watu na viatu, kwa hio kila mtu na tafsiri yake....binafsi sioni ubaya mzee Makamba alivyosema.Naona hapa hamumtendei haki mzee Makamba kwani nyie hio ni tafsiri yenu...sometimes jamani lazima tuwe fair sio kila kitu kucriticise just because kimesemwa na mwana CCM....
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Uliza walivyo-MSILIBA akiwa Gama akiwa hai.
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Uropokaji utaisha pale atakapo vuliwa hicho cheo alichonacho!
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,956
  Trophy Points: 280
  Subuthu, we unafikiri CCM kuna anayeweza kumtia kengele shingoni paka shume kama lile? Naskia ana mikopa ya wahenga wake!
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Wakati u hai hai ni ngumu hata kukujulia hali.Ukifa bwana watu walewale waliokuwa wanakusulubu ndo wanakuwa karibu na jeneza lako wakiimba sifa zote kubwa humu duniani.Unafiki siasa za Tanzania sijui nani aliziasisi. Ni azimio la arusha tu limeweza kufa lakini sio unafiki ndani ya siasa
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  uropokaji ni staili yake ya maisha/kuzeeka.

  ALIVYO NDIVYO ALIVYO!REST IN PEACE MZEE MAKAMBA
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  mama aliniambia kuwa uyaone..
  leo nayaona baadhi ya mambo.
   
Loading...