Hii sasa iko hivi, Juzi (Saturday) nikiwa kwenye arosto ya aviator nilimcheki mwanangu mmoja nilikua na mdai 150k akanielekeza nikaichukue nyumbani kwake(geto) kuna duka jirani huwa anaacha funguo .Yeye alikua kazini kariakoo ,sasa nilivyofika kwenye droo yake nikakuta kuna kama 2M hivi.
Roho ikalipuka kwa furaha, nikasema hapa nachezea hii napata zangu faida ya million then namwachia pesa yake kama kawaida.
Nikachukua 1.5M nikadeposit nikachukua na wine ya mwanangu nikaaa niaze kumramba mhindi kupitia aviator .
Ndani ya saa ikawa imebaki laki moja, hapo nasweti tu mapigo ya moyo yanaenda speed mno maana pesa sio ya kwangu na jamaa ananiamini mno.
Nikadepost na ile 500k iliokua imebaki nikiwa nimepaniki (makosa makubwa), kwamba nirudishe hata hela yake tu sasa.
Ndio unaona hapo imebaki 300k nazugia hapo .
Kilichotokea juu ya mimi na jamaangu ndio kilichonileta huku Jf na kuamua kufunguka hivyo,stori ndefu
Sasa imagine kama pesa ya mtu mwingine naifanya hivyo vipi hela yangu?
Mimi ni tour guide mkuu, karibu Nyerere national park (selous Game reserve)