Urgent vs Important. Wahitimu vyuo vikuu Vs Loan Board

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Members, Leo nimekutana na kijana aliyesoma udsm amechoka kukatwa asilimia 15 % kwenye Gross Salary yake kulipa deni lake la mkopo wa wanafunzi(HESLB)

Amebakiwa na deni la Milioni nne(4,000,000).Mshahara wake ni Milioni moja na laki sita yaani (Gross Salary 1,600,000)

Kila mwezi anakatwa kama 240,000 laki mbili arobaini ya loan board,

Alihitaji nimpatie Milioni nne akalipe deni Heslb na kuondokana na dhahama ya asilimia 15%

Chanzo cha kuandika mada hii ni kutokana na mawazo ya huyo kijana msomi

1.Mosi mimi nilikataa kumpa Milioni nne akalipe loan Board, Nilimshauri naweza mpa Milioni nne Afanye biashara, aizungushe izae apate faida ndio alipe deni lake

Future is uncertain, Unawezaje clear debt ya 4 million kwa kutegemea utarudisha toka kwenye mshahara?

Pili, Nilimshauri atofautishe vitu vya haraka na vitu muhimu

Milioni nne kwa kijana wa chuo na maisha wanayokupambana nayo sasa anaweza fanya jambo la msingi Katika biashara kuliko kuzitumia kulipa Deni lake

Mawazo ya vijana wa sasa yana changamoto kubwa sana, Zamani sisi hatukuwa na mambo ya Pizza, Chipsi kuku, Full bucket

Vijana wa sasa mambo mengi pesa ya Gross Salary Milioni moja laki sita anashindwa kuvumilia kulipa deni
 
Back
Top Bottom