Urembo asilia ni salama zaidi kwa afya ya ngozi yako

Said Cosmetics

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
2,001
1,586
*EXOGENOUS OCHRONOSIS TATIZO LITOKANALO NA KUTUMIA CREAM ZA KUBADILISHA RANGI USONI*
Hii ni hali ya ngozi ambayo husababishwa na matumizi ya muda mrefu ya bidhaa za kubadilisha rangi ya ngozi;Hata kama HYDROQUINONE iko kwa kiasi kidogo mfano wa 2%...

Bidhaa za kung’arisha ngozi bado zinatumika sana sehemu mbalimbali duniani.Hii husababishwa na hali ya jamii inayozunguka ambapo rangi nyeupe huonekana kuwa nzuri kuliko rangi asilia aliozaliwa nayo mtu kwa lugha nyingine ukiwa na rangi nyeupe waonekana mrembo zaidi.

Hydroquinone ni kemikali ambayo hasa hutumika kwenye hung’arisha ngozi.Kutokana na side effects ambazo kemikali hii inasababisha kwa ngozi ilizuiwa isitumike kwenye kutengeneza vipodozi vya matumizi ya kila siku.Labda kwenye dawa za magonjwa ya ngozi kama malasma (ambao ni ugonjwa unaotakana na ngozi kuzalisha melanini nyingi sana zaidi ya inavotakiwa na kufanya ngozi kuwa na rangi nyeusi zaidi ya uhilisia)na hii dozi utapewa na daktari kwakipindi maalumu.

KWANINI:matumizi ya muda mrefu ya kemikali hii husababisha EXOGENOUS OCHRONIC LESIONS;muda wa utumiaji huenda sambamba na uharibifu ambao hutokea.Kwahiyo uharibifu zaidi kwa mtu ambae ametumia kemikali kwa miaka mingi zaidi ya wengine.

Wengi hatuna addiction ya madawa ya kulevya lakini tu waelvi wa urembo usiosalama.Kuna mtu miaka nenda rudi hawezi kuacaha kemikali kwa ngozi yake,na ukirejea juu ya madhara inaonesha tayari kemikali imeshaaribu ngozi yake sana na afya kwa ujumla.Wengi wamesikia juu ya madhara yanayosababishwa na kemikali hizi hasa kiafya kwa matumizi ya muda mrefu lakini bado hawataki kuacha.

*Ni muda sasa ufanye maamuzi kwamba ni bora uendelee kutumia uzidi kujiweka kwenye hatari kiafya na kwa ngozi yako au uache utumie bidhaa salama ambazo zitakupendezesha*

Wasiliana nami:
Kwa namba 0759827138
Whatsapp/text
IMG-20180922-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom