Fahamu vitu vya kuzingatia unapofanya DAILY SKIN CARE ROUTINE yako

Feb 9, 2023
5
9
Vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia unapofanya DAILY SKIN CARE ROUTINE yako yaani ASUBUHI na JIONI.

WAKATI WA ASUBUHI
Wakati wa asubuhi ngozi zetu huathiriwa sana na environmental damages kama vile jua,vumbi na taka zingine zilizopo hewani.Hivyo basi tunashauriwa kulinda ngozi zetu asubuhi dhidi ya izo Environmental Damages kwa kufanya yafuatayo:

1.Kutumia Sunscreen
Utumiaji wa Sunscreen utakulinda na kuungua na jua pia inapunguza kiasi kikubwa sana cha uchafu kama vile vumbi ku-attack uso wako.Faida nyingine ya kutumia sunscreen ni kukulinda na risk ya kupata kansa ya ngozi kutokana na kuungua na miale ya jua.

2.Kutumia Anti-Oxidant Ingredients
Utumiaji wa vitu vilivyo na anti-oxidant kama vile Vitamin C hapa tunazungumzia Vitamin C serum au Vitamin C moisturizer,Vitamin C huwa ni chakula kizuri sana kwa ngozi,itakupendezesha sana kwa kukupa uso wenye ung'avu mzuri bila kukubadilisha ngozi yako ila kuiboresha ngozi yako.

3.Ku-hydrate Ngozi
Utaweza ku-hydrate ngozi yako kwa kutumia moisturizer sahihi kutokana na aina ya ngozi yako, ku-hydrate ngozi yako itakufanya kuepuka kukakamaa au kufifia kwa ngozi yako

WAKATI WA USIKU
Wakati wa usiku ni wakati sahihi wa kutibu ngozi yako maana ngozi hujiponyesha zaidi nyakati za usiku,hivyo ni muhimu kutumia vitu vitakavyoponyesha ngozi yako wakati wa usiku ili ngozi yako ipone kwa haraka zaidi na kupata ile dream ngozi yako

-Mfano mtu unaesumbuliwa na chunusi ni muhimu kwenye routine yako usiku ukatumia vitu vyenye ingredients kama vile salicylic acid,benzoyl peroxide,tea tree n.k

-Kama unataka kuondoa makunyazi na dalili zote za uzee tumia bidhaa yenye Retinol usiku.

-Pia usiku ni muda mzuri wa kuondoa dead skin cells kwa kutumia ingredients kama salicylic acid,gycolic acid,lactid acid.Hizi zote Utumiaji wake unategemeana na aina ya ngozi yako.

Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi kuhusu ngozi yako na matumizi sahihi ya vipodozi kutokana na shida au aina ya ngozi yako.
Pia karibu ujipatie vipodozi origin kutoka UK.
Tupigie au tutumie meseji kupitia number +255 769 081 492
 
Back
Top Bottom