SoC01 Urasimishaji wa Huduma za Kodi kwa Wajasiliamali Wadogo wadogo kwa mfumo wa 'EFD KWA WOTE'

Stories of Change - 2021 Competition

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,361
5,881
Utangulizi

Urasimishaji wa Biashara ni shughuli muhimu kwa kuiwezesha nchi kukusanya kodi lakini pia kuwawezesha wafanya biashara ndogo ndogo kutoa huduma za kibiashara kwenye mfumo rasmi kwa kutimiza vigezo.

Moja ya eneo la urasimishaji wa biashara ambalo halijafanyiwa kazi ipasavyo ni kumtambua mfanya biashara ndogo ndogo au asiye wa kudumu katika mfumo wa kodi. Hiki kimekuwa kizuizi kikubwa cha kuwawezesha wajasiliamali wanaochipukia kuweza kutoa huduma kwenye taasisi, mashirika au serikali kwa kuwa hawako kwenye mfumo wa uotaji risiti za kodi kwa kuwa hawana mashine za EFD.


Mapendekezo

Mamlaka ya mapato ifungue dirisha la kuwahudumia wajasiliamali wadogo wadogo liitwalo ‘EFD KWA WOTE’ kwa kuwawezesha kupata risiti za EFD bila kumiliki mashine za EFD. Nitatoa mfano

Erika ni mwalimu wa shule ya msingi. Wiki ijayo amepata tenda ya kusambaza chakula kwenye mkutano ulioandaliwa na jumuiya ya wanawake, lakini Erika ana kikwazo kimoja tu kinachomkabili, hana uwezo wa kutoa risiti ya EFD ili kuweza kumpatia mteja wake.

Kwa mfumo huu wa ‘EFD KWA WOTE’, Erika atatakiwa awe na Tin number aende nayo TRA na mchangamanuo wa mahesabu uliojazwa kwenye fomu maalum itayotolewa na TRA. Iwapo Erika alinunua vitu vya kuhudumia semina hiyo kutoka kwenye super market, basi tayari atakuwa na risiti inayoonesha input tax. Mfano Alinunua vitu vya Sh laki moja na akalipa laki moja na kumi na nane elfu, risiti hiyo itaonesha input tax ya Tsh elf 18.

Ametoa huduma ya kulisha kwenye semina kwa Sh laki mbili na elfu thelasini na sita pamoja na kodi, basi atakwenda TRA na ile risiti aliyopewa super market inayoonesha input tax, na pia ataenda na profoma invoice au mkataba unaoonesha kuwa atapokea/ amepokea Tsh laki mbili na elfu thelasini na sita. Kwa kuwa alikwishalipa Tsh elfu 18, kama input tax, basi Erika atalipa tena Tsh elfu 18 nyingine kama ongezeko la thamanani (VAT) na TRA kwa kupitia dirisha la wajasiliamali wadogo wadogo, watampatia Erika risiti ya EFD ambayo yeye ataipeleka kwenye jumuiya ya kina mama hivyo kukamilisha muamala kwa viwango vya kihasibu na kikodi vinavyotakiwa.

Dirisha hili la ‘EFD KWA WOTE’ likifanya kazi kwa mfumo huu, litawaibua watu wengi amabo sio wafanyabiashara wa full time kutumia fursa za kibiashara za kusupply bidhaa ndogo ndogo kwenye makampuni, kwenye taasisi na serikalini kwa viwango vya kodi vinavyokubalika hivyo kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.
 
Wazo zuri, lakini kusajili eneo maalum la biashara inasaidia sana kupunguza utakatishaji fedha na kupeana kazi kwa upendeleo, vile vile inamlinda mnuuaji akitaka kurudi aliponunua vitu kwa sababu yeyote ile. Kama mtu yeyote mwenye TIN ataweza kuuza hivyo tutadhibiti vipi hayo?.

Kingine TRA wamerahisisha sana kutoa risiti kwa wafanyabiashara kama nilivyoandika HAPA sio bure bado kama ulivyopendekeza lakini naona wanaeleka huko.
 
Back
Top Bottom