‘Uranium suluhisho la umeme’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Uranium suluhisho la umeme’

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Oct 22, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mussa Juma, Arusha.
  UPUNGUFU wa umeme katika maeneo mengi nchini, unaweza kutoweka kabisa kama Tanzania itaanza kutumia madini ya Uranium na kutengeneza nyuklia ya kuzalisha umeme. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mionzi, Firm Banzi, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya kimataifa ya wataalam wa masuala ya mionzi mjini hapa, alisema hata hivyo, inahitajika maandalizi ya miaka 15 kuweza kutumia Uranium kuzalisha umeme.

  Banzi alisema matumizi hayo yakianza gharama za umeme zitapungua sana na suala la mgao wa umeme linaweza kuwa historia, kwakuwa Tanzania ni moja ya nchi chache duniani zenye akiba kubwa ya madini ya Uranium ambayo tayari yamegunduliwa katika maeneo ya mbalimbali ikiwepo, Namtumbo mkoani Ruvuma na Bahi mkoani Dodoma.

  Hata hivyo Banzi alisema kwa sasa hakuna wataalam wa kutosha katika suala la uchimbaji na uhifadhi wa mabaki ya Uranium hapa nchini. “Jambo hili linahitaji maandalizi makubwa kwani madini haya yana mionzi hatari sana, hatari yake siyo kuchimba tu bali hata kuhifadhi udongo wenye mabaki yake” alisema Banzi.

  Kaimu Mkurugenzi huyo hata hivyo, alisema tayari sera za madini hayo zimeandaliwa na zipo katika ngazi mbali mbali za serikali katika mchakato wa kufikiwa maamuzi.

  Awali akizungumzia mafunzo hayo, yanayoshirikisha wataalam kutoka nchi 19 Wanachama wa Shirika la Kimataifa la Mionzi , Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo katika kufanyia ukarabati vifaa vya kupima mionzi.

  Naye mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Yesaya Sungita alisema, kuna umuhimu mkubwa wa wataalam wa mionzi kuwa na uwezo wa kukarabati vifaa vyao vya kupima mionzi ili viendane na vigezo vya kimataifa.

  Alisema vifaa vya upimaji wa mionzi vinafanana hivyo ni muhimu kuhakikisha vinakuwa katika ubora ambao unatakiwa wakati wote ili vitoe majibu sahihi wakati wa uchunguzi.

  Wataalam hao, wanatoka barani Afrika na wanashiriki mafunzo ya siku tano, ambayo ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa kwa wataalam wa mionzi duniani, hasa kutokana na changamoto za kuongezeka kwa matumizi ya mionzi katika nchi nyingi duniani.
   
 2. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uranium sio suluhisho la umeme. Serikali inawadanganya Watanzania baada ya kushindwa kuondoa matatizo ya umeme kwa njia mbadala.
  Uranium ni janga la dunia nzima na sio Tanzania peke yake, Pollution inayotoka katika nuclear power plant imechangia kwa kiasi kikubwa
  mabadiliko ya hali ya hewa duniani na madhara yake sio tu kwenye sehemu ambayo wanazalisha umeme kwa kutumia Uranium bali ni kwa
  Dunia nzima. Mvua kubwa kunyesha na kuleta mafuko pamoja na vimbunga vikali ambavyo uharibu mazingira na kuuwa watu.
  Na joto kali katika utando wa O zone ambalo linasababisha barafu kuyeyuka juu ya Dunia North pole, na hata mlima wetu wa Kilimanjaro
  barafu iliyokuwa ikitanda imeyeyuka. Na afya za wale wanaoishi kuzunguka eneo la madini ya Uranium zitakuwa mashakani, Dunia sasa
  hivi ipo katika kufunga na kuondoa matumizi yote ya uranium katika uzalishaji wa umeme. Na ikiwa wataamua kuuza tatito liko pale pale
  na isitoshe watatengeneza mabomu ya atomic ambayo hayatachagua nani wa kumuuwa. Hiyo Uranium tuisahau kabisa na kuweka
  mbadala wa umeme kwa kutukmia Gas, Upepo, Jua pamoja na maji. Hakuna kinachoshindikana katika hivyo vinne bali ni uzembe wa
  viongozi wa Serikali ya Ccm.
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nikweli kabisa atujafikia kiwango cha kutumia umeme huo wakati bado tuna mabwawa makubwa na ya uawakika tuna makaa ya mawe ambayo yangeweza kutatua tatizo kabisa kuna upepo bado atujatumia kabisa na bado tunawaza urenium
   
Loading...